Kilwa Road baada ya kumalizika imeanza kuharibika!

Kilwa Road baada ya kumalizika imeanza kuharibika!

Kiukweli hiyo barabara sasa hivi haifai isitoshe ndio njia inayopitisha magari mengi ya mizigo lakini barabara ni ya tope.wamebomoa lami wameshindwa kujenga wameamua kuiacha.inatukera kwa kweli
 
Na kuna ule utaratibu wa kufunga barabara ikifika jioni eti magari ya kutoka kilwa road yasiingie mjini.unakaa kwenye foleni masaa mawili .......kweli uongozi wa temeke ujipange upya
 
Huu ni upuuzi mwingine,inakuwaje ufanye jambo la athari kubwa kama hili na viongozi mko mnapita barabara hiyo hiyo? Nini maana ya uongozi?

Huyu mkandarasi kama alikuwa hana uwezo wa kukarabati barabara hii ilikuwaje mkampa tenda hiyo? Amechimbua lami sasa ni miezi miwili, hajengi wala hakuna dalili ya kujenga.

Kuanzia Saba Saba Ground hadi Mtongani ni maafa kwa wanaotumia barabara hii. Kipindi hiki cha mvua ndio maafa makubwa .

Tunahitaji matengenezo ktk barabara hiyo kodi mnakusanya kila leo.

Mkandarasi ni Skol,ile ya mzee Mlaki,inahusishwa na vigogo wakubwa kuwa wamiliki,tender nyingi za dar na mikoa ya karibu huwa wanapewa wao,si jambo baya kwani ni kampuni ya wazawa,sema kama kilwa road wanachemka,wawajibishwe,kazi zao zingine ziko bomba sana tu!
 
Jaman tusipende kuwalaumu sana Wakandarasi, tatizo serikali haina hela ya kuwalipa wakandarasi, wafadhili waligoma kutoa
 
Back
Top Bottom