Kilwa Road baada ya kumalizika imeanza kuharibika!

Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli akiongea kwa msisitizo wakati alipoongea na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Wizara hiyo kuhusu upanuzi wa barabara ya Kilwa Road yeny kilomita 5.1 kwa kiwanga cha lami itakayojengwa na mkandarasi Kajima Corporation. Barabara hiyo inarudiwa kujengwa kwa mara ya pili baada ya kampuni hiyo kubonronga katika ujenzi wa awali, Waziri Magufuli ameongeza kwamba Mkandarasi ataondoa tabaka la lami katika urefu wa Kilomita 5.1 na tabaka jipya la lami lenye unene wa sentimeta 7 akitumia lami yenye kiwango cha ugumu cha 40/50 na kokoto za ukubwa wa milimita 20. Yaani zege la lami (Asphalt Concrete) lenye kokoto za ukubwa wa milimita 20 (AC20), lami iliyoimarishwa zaidi itafikiriwa kutumika sehemu za barabara zenye kubeba mzigo mkubwa zaidi, katika picha kulia ni Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mh. Masaki Okada. Source: Mjengwa blog
 
hatimaye machinjio ya barabara yetu ya kilwa/mandela (uhasibu) yamekumbukwa kwa kuwekewa taa za kuongozea magari baada ya muda mrefu kuwa eneo la hatari. RIP ndugu zetu wengi waliopoteza maisha pale
 
Hongera zenu, ila hapo kwenye machinjio orijino karibu na kiwanda cha pombe vipi na zenyewe zimewaka?
 
nasikia jana ziliwashwa? Pamoja na za chang'ombe na buguruni? Baada ya kuwa pambo kwa takriban mwaka sasa kama sikosei?
 
Kule kuthubutu kwa Waziri wa Ujenzi ndiko kunakonifanya kumpa heshima kubwa sana John Magufuri nadhani kuliko mawaziri wengine kwa mwaka huu wa 2011-2012...

Magufuri alikataa kupokea barabara ya kilwa road wakati alipochaguliwa kuwa Waziri wa ujenzi akitokea kwenye Wizara ya Uvuvi, alifanya hivyo kwakuwa barabara hiyo ilijengwa chini ya kiwango.

Watu walikuwa kama hawamuelewi kwakuwa barabara ilikuwa bado mpyaa (KIPYA KINYEMI) ubovu wake ulikuwa hauonekani lakini baada ya muda kidogo walijionea na leo hii barabara hiyo imeanza kubanduliwa rami yake kwaajili ya kurudiwa kujengwaa kwa kiwango stahiki...

Mungu ibariki Tanzania Mungu wabariki wazarendooo.
 
ubabaishaji kila sehemu, huyu mjenzi wa hii barabara mbona amekuwa kero.....?kuanzia pale bendera tatu amekwangua lami yoote hadi mivinjeni, yapata mwezi sasa hakuna matengenezo yoyote, unatusababishia usumbufu mkubwa watumiaji wa barabara hiyo, KAMA ULIKUWA HUJAJIANDAA KWANINI ULIKWANGUA HIYO BARABARA...........?
 
Pale panaonesha ubabaishaji wa hali ya juu...kwa mwenddo ule barabara si itaisha 2050
 
mjenzi ni yule aliyetoa fungu kubwa la posho , ile inayoitwa 10 percent ! Japo hakuna ujenzi wa barabara nchi hii , mara zote wamekarabati tu zilezile za wakoloni .
 
kiukweli kama ningekuwa na uwezo ningefukuzilia mbali yule mkandarasi , nisingeishia hapo tu , bali ningemrundika rumande ! Haiwezekani aondoe raha halafu alete kero !
 
Nashangaa sana mabongo lala wanamsifu yule pombe eti mchapakazi wakati barabara inajengwa chini ya kiwango alikuwepo tu kakodoa macho afu anakuja kwenye tv eti mkandarasi atarudi kwa gharama zake haoni mradi ukichelewa hata kama anarudia kwa pesa zake ni tayari anatupa hasara
 
Nashangaa sana mabongo lala wanamsifu yule pombe eti mchapakazi wakati barabara inajengwa chini ya kiwango alikuwepo tu kakodoa macho afu anakuja kwenye tv eti mkandarasi atarudi kwa gharama zake haoni mradi ukichelewa hata kama anarudia kwa pesa zake ni tayari anatupa hasara

hana lolote , aliuza hata kota za polisi !
 
Kama nilielewa vizuri huko nyuma, barabara hiyo itajengwa na Japan, na hao wajapan wana/me-kamilisha kumpata mkandarasi na Mheshimiwa wetu mmoja alisema wao wanaendelea na kusafisha maeneo hayo ikiwa pamoja na Tazara. Kwa hiyo huenda ndio usafishaji huo umeanza ila mvumilie tu kumsubiri mkandarasi toka JPY. Habari ndio hiyo.
 
ubabaishaji kila sehemu, huyu mjenzi wa hii barabara mbona amekuwa kero.....?kuanzia pale bendera tatu amekwangua lami yoote hadi mivinjeni, yapata mwezi sasa hakuna matengenezo yoyote, unatusababishia usumbufu mkubwa watumiaji wa barabara hiyo, KAMA ULIKUWA HUJAJIANDAA KWANINI ULIKWANGUA HIYO BARABARA...........?



Pole. Ila Tanzania ya leo kila kitu ni usanii. Utashangaa kuna wafuatiliaji hapa lakini nobody does anything kwa kuwa tu mkuu wa nchi hawawajibishi watendaji. Hapa angekuwa Kagame haki ya nani huyu mkandarasi pamoja na msimamizi wa huu mradi anafungwa mpaka kieleweke. Hapa Tanzania watu wanafanya usanii.
 
Back
Top Bottom