Rais Dkt. Samia aineemesha Mikoa ya Kusini

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hasaani amekamilisha ziara yake Mikoa ya Mtwara na Lindi, iliyoanza Desemba 15 hadi 20, 2023. Ziara hii imekuwa ziara yenye mafanikio makubwa sana kwa wananchi wa Mtwaea na Lindi kutokana na yale ambayo ameyafanya Mhe, Rais katika ziara hiyo.

Ziara iliyochukua takribani siku saba za faida kuwahi kutika kusini mwa Tanzania, huku ikitazamiwa kuwa ndiyo ziara iliyokuwa muda mrefu tangu serikali ya awamu ya sita iingie madarakani. Katika ziara hiyo, Mhe, Rais amezindua na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo hospitali ya rufaa ya kanda ya kusini, bandari, kiwanja cha ndege, chujio la maji na barabara.

Rais Dkt Samia amezindua hospitali ya rufaa ya kanda ya kusini iliyojengwa kwa zaidi ya shilingi Bilioni 24 yenye vifaa vya kisasa, ikiwepo mashine ya CT Scan na X Ray tatu ambazo zina thamani ya shilingi Bilioni 7.5.Pia fedha zote za dawa zinatoka kwa asilimia 100 na sasa ametoa shilingi Bilioni 17 kwa ajili ya ujenzi wa Bohari ya Dawa kanda ya kusini. Waliyo wengi wanajiuliza amewezaje, siri kubwa ya mafanikio ya Rais Dkt Samia ni kusikiliza hoja za Watanzania na kuzifanyia kazi.

Rais Dkt. Samia ameendelea kuifungua Mtwara kwa kuzindua mradi wa chujio la kuboresha ubora wa maji yanayotumiwa na wananchi wa Mtwara lililogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 3.4 mradi ambao utaongeza huduma ya upatikanaji wa maji safi na yenye Ubora. Hii ni baada ya kuonekana wananchi wake na wapiga kura wanapata changamoto ya maji safi na salama, ndipo alimua kuelekeza kiasi hicho ili kuboresha miundombinu ya kusafisha maji lililokuwepo awali ni ya tangu mwaka 1958. Sasa mradi huu utakuwa na uwezo wa kuchuja maji kiasi cha lita 12,500,000 kwa siku.

Rais Dkt Samia anaendelea kuingia katika mioyo ya Watanzania kutokana na matendo yake. Katika ziara yake pia, aliitembelea bandari ya Kilwa akiwa na lengo la kuwainua wanawake na vijana katika sekta ya uvuvi na kilimo cha mwani. Kupitia mkutano wake aligawa boti za kisasa 160 kwa wavuvi, ikiwa ni mradi wenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 280. Ikiwa boti hizo zimetolea kwa mkopo wa masharti nafuu na unalenga kutoa ajira na kuongeza kipato cha jamii na serikali kwa ujumla. Boti ndogo zitatumiwa na akina mama kulima mwani na kubeba mizigo, na zile kubwa zinakwenda kwenye kina cha maji marefu kwaajili ya uvuvi.

Katika kuelendelea kuboresha mazingira ya wananchi wake, Rais Dkt Samia ametoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 11.5 zitakazowasaidia wavuvi. Malengo yake ni makubwa sana kwa nchi yetu kwani kupitia bandari hiyo inakwenda kuinua uchumi kupitia sekta ya uvuvi kutoka asilimia 1.8 hadi kumi kufikia mwaka 2036. Ambapo katika bandari hiyo kutakua na karakana ya meli, sehemu ya kuegesha meli kubwa kumi zenye urefu wa mita 30. Aidha, meli kutoka maeneo mbalimbali duniani, kuegesha mitumbwi isiyopungua 200, sehemu ya kuegesha mashua na kutoa fursa ya kutoa ajira kwa vijana takribani 30,000, kuhifadhi samaki tani 1300 kwa wakati mmoja.

Rais Dkt Samia ameamua kutekeleza ahadi yake aliyoitoa kipindi cha kampeni ya kujenga barabara ya barabara ya Mtwara – Mnivata yenye urefu wa km 50, ni sehemu ya barabara ya kusini itokayo Mtwara – Newala hadi Masasi kupitia wilaya za Tandahimba na Newala yenye urefu wa km 210. Barabara hiyo inatajwa kupitia maeneo ya kimkakati katika mtandao wa barabara ambako korosho hulimwa kwa wingi katika Wilaya za Tandahimba na Newala, hivyo itaunganisha wakulima na masoko kupitia Bandari ya Mtwara na Kiwanja cha ndege cha Mtwara kwenda katika maeneo mengine ya ndani na nje ya nchi.

Hadi kukamilika kwa mradi huu, jumla ya shilingi 78,401,225,420.37 zimelipwa kwa Mkandarasi, shilingi 4,614,877,406.77 zimelipwa kwa Mhandisi Mshauri na Shilingi 70,435,260.94 zimelipa fidia ya mali na ardhi kwa wananchi walioathiriwa na mradi kwa mujibu wa sheria. Aidha, kulingana na usanifu, sehemu isiyo na makazi, barabara hiyo imejengwa kwa upana wa mita 9.5 ambapo mita 6.5 ni njia ya magari na mita 1.5 kila upande ni mabega ya barabara kwa ajili ya watembea kwa miguu. Sehemu za makazi barabara imejengwa kwa upana wa jumla wa mita 10.5 ambapo mita 6.5 ni njia za magari na mita 2.0 kila upande ni mabega ya barabara kwa ajili ya watembea kwa miguu.

Ziara ya Rais Dkt Samia SuluhuHassan imefana sana kwa wananchi wa Kusini, kwani hayo ni baadhi ya matunda waliyoyapata kutokana na uongozi wake. Watanzania tumuunge mkono Rais wetu, kwani kaonesha yeye ni kiongozi anayefanya kwa vitendo na siyo maneno maneno, na maendeleo yanaonekana.

20230917_200327.jpg
 
Hivi kuna ulazima wa kumuita huyu Mama Daktari kweli?
Nakumbuka kuna bandiko fulani niliwahi kusoma mahali, linasema Mwalimu Nyerere peke yake alikuwa na PhD za heshima zaidi 20! Lakini hakuwahi kuitwa/kujiita Dokta/daktari katika maisha yake yote hapa duniani!

Shida iko wapi kwa sasa!! Hata Mwinyi na Mkapa nasikia waliwahi kutunukiwa hizi shahada! Ila ilipofika kwa Mzee wa Msoga, mambo ndipo yalipoanza kubadilika! Utamsikia mtu naomba kuchukua nafasi hii kumshukuru Daktari...... kwa kuupatia hela za kujengea bla bla!!! Kweli?
 
sawa, a
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hasaani amekamilisha ziara yake Mikoa ya Mtwara na Lindi, iliyoanza Desemba 15 hadi 20, 2023. Ziara hii imekuwa ziara yenye mafanikio makubwa sana kwa wananchi wa Mtwaea na Lindi kutokana na yale ambayo ameyafanya Mhe, Rais katika ziara hiyo.

Ziara iliyochukua takribani siku saba za faida kuwahi kutika kusini mwa Tanzania, huku ikitazamiwa kuwa ndiyo ziara iliyokuwa muda mrefu tangu serikali ya awamu ya sita iingie madarakani. Katika ziara hiyo, Mhe, Rais amezindua na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo hospitali ya rufaa ya kanda ya kusini, bandari, kiwanja cha ndege, chujio la maji na barabara.

Rais Dkt Samia amezindua hospitali ya rufaa ya kanda ya kusini iliyojengwa kwa zaidi ya shilingi Bilioni 24 yenye vifaa vya kisasa, ikiwepo mashine ya CT Scan na X Ray tatu ambazo zina thamani ya shilingi Bilioni 7.5.Pia fedha zote za dawa zinatoka kwa asilimia 100 na sasa ametoa shilingi Bilioni 17 kwa ajili ya ujenzi wa Bohari ya Dawa kanda ya kusini. Waliyo wengi wanajiuliza amewezaje, siri kubwa ya mafanikio ya Rais Dkt Samia ni kusikiliza hoja za Watanzania na kuzifanyia kazi.

Rais Dkt. Samia ameendelea kuifungua Mtwara kwa kuzindua mradi wa chujio la kuboresha ubora wa maji yanayotumiwa na wananchi wa Mtwara lililogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 3.4 mradi ambao utaongeza huduma ya upatikanaji wa maji safi na yenye Ubora. Hii ni baada ya kuonekana wananchi wake na wapiga kura wanapata changamoto ya maji safi na salama, ndipo alimua kuelekeza kiasi hicho ili kuboresha miundombinu ya kusafisha maji lililokuwepo awali ni ya tangu mwaka 1958. Sasa mradi huu utakuwa na uwezo wa kuchuja maji kiasi cha lita 12,500,000 kwa siku.

Rais Dkt Samia anaendelea kuingia katika mioyo ya Watanzania kutokana na matendo yake. Katika ziara yake pia, aliitembelea bandari ya Kilwa akiwa na lengo la kuwainua wanawake na vijana katika sekta ya uvuvi na kilimo cha mwani. Kupitia mkutano wake aligawa boti za kisasa 160 kwa wavuvi, ikiwa ni mradi wenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 280. Ikiwa boti hizo zimetolea kwa mkopo wa masharti nafuu na unalenga kutoa ajira na kuongeza kipato cha jamii na serikali kwa ujumla. Boti ndogo zitatumiwa na akina mama kulima mwani na kubeba mizigo, na zile kubwa zinakwenda kwenye kina cha maji marefu kwaajili ya uvuvi.

Katika kuelendelea kuboresha mazingira ya wananchi wake, Rais Dkt Samia ametoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 11.5 zitakazowasaidia wavuvi. Malengo yake ni makubwa sana kwa nchi yetu kwani kupitia bandari hiyo inakwenda kuinua uchumi kupitia sekta ya uvuvi kutoka asilimia 1.8 hadi kumi kufikia mwaka 2036. Ambapo katika bandari hiyo kutakua na karakana ya meli, sehemu ya kuegesha meli kubwa kumi zenye urefu wa mita 30. Aidha, meli kutoka maeneo mbalimbali duniani, kuegesha mitumbwi isiyopungua 200, sehemu ya kuegesha mashua na kutoa fursa ya kutoa ajira kwa vijana takribani 30,000, kuhifadhi samaki tani 1300 kwa wakati mmoja.

Rais Dkt Samia ameamua kutekeleza ahadi yake aliyoitoa kipindi cha kampeni ya kujenga barabara ya barabara ya Mtwara – Mnivata yenye urefu wa km 50, ni sehemu ya barabara ya kusini itokayo Mtwara – Newala hadi Masasi kupitia wilaya za Tandahimba na Newala yenye urefu wa km 210. Barabara hiyo inatajwa kupitia maeneo ya kimkakati katika mtandao wa barabara ambako korosho hulimwa kwa wingi katika Wilaya za Tandahimba na Newala, hivyo itaunganisha wakulima na masoko kupitia Bandari ya Mtwara na Kiwanja cha ndege cha Mtwara kwenda katika maeneo mengine ya ndani na nje ya nchi.

Hadi kukamilika kwa mradi huu, jumla ya shilingi 78,401,225,420.37 zimelipwa kwa Mkandarasi, shilingi 4,614,877,406.77 zimelipwa kwa Mhandisi Mshauri na Shilingi 70,435,260.94 zimelipa fidia ya mali na ardhi kwa wananchi walioathiriwa na mradi kwa mujibu wa sheria. Aidha, kulingana na usanifu, sehemu isiyo na makazi, barabara hiyo imejengwa kwa upana wa mita 9.5 ambapo mita 6.5 ni njia ya magari na mita 1.5 kila upande ni mabega ya barabara kwa ajili ya watembea kwa miguu. Sehemu za makazi barabara imejengwa kwa upana wa jumla wa mita 10.5 ambapo mita 6.5 ni njia za magari na mita 2.0 kila upande ni mabega ya barabara kwa ajili ya watembea kwa miguu.

Ziara ya Rais Dkt Samia SuluhuHassan imefana sana kwa wananchi wa Kusini, kwani hayo ni baadhi ya matunda waliyoyapata kutokana na uongozi wake. Watanzania tumuunge mkono Rais wetu, kwani kaonesha yeye ni kiongozi anayefanya kwa vitendo na siyo maneno maneno, na maendeleo yanaonekana.

View attachment 2757120
sante kwa taarifa
 
Back
Top Bottom