Kilimanjaro: Binti adaiwa kumuua mama yake kisha kumng’oa macho

Kama ni yeye mhusika inaonekana ana sifa za u psychopath. Kama si ivyo she has psychologically trained herself to be a serial killer ,au ni tu movie twa hollywood tulimpa guts 😂😂😂😂
 
Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Kindi Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro anadaiwa kumuua mama yake mzazi, Marietha Mushi (62) kwa kumnyonga na shuka, kisha kumpiga na kitu kizito kichwani na kumng’oa macho.

Habari zinaeleza kuwa mama huyo alikuwa na ulemavu wa mkono jambo linalodaiwa kuchangia ashindwe kujitetea wakati akishambuliwa na binti yake huyo.

Akizungumza na Mwananchi Digital Jumanne Julai 6, 2021 mkuu wa Wilaya ya Moshi, Said Mtanda amesema tukio hilo limetokea Julai 5, 2021 eneo la Kibosho Sambarai.

"Mtoto amemuua mama yake na mtoa taarifa ambaye ni kaka wa marehemu ameeleza kuwa alibaini kuuawa kwa dada yake kwa kunyongwa na shuka kisha kupigwa na kitu kizito kwenye paji la uso. Alisema aling’olewa macho na huyu mwanaye wa kike ambaye anasoma kidato cha nne,” amesema Mtanda.

Amesema mwanafunzi huyo amekamatwa na uchunguzi wa Polisi unaendelea

Source: Mwananchi Newspaper
Wachaga Sio watu kabisa

USSR
 
Binti mdogo halafu kamuua mama yake,kamnyonga,halafu baada ya kufa kampiga na kitu kizito,halafu kamtoa na macho,hapa uchunguzi wa kina unahitajika kwanini ampige na kitu kizito baada ya kumnyonga,na hayo macho kwanini kayatoa kama lengo lilikuwa ni kumuua tu...?
Huyo Mama kauwawa na wauwaji wa kweli ambao wanajuwa jinsi ya kupoteza ushahidi, ndiyo maana wamenyofowa macho!! Ngoja niishie hapa nisije nikaharibu Upelelezi wa wenyewe bure!!
 
Exactly
Sisi ni wanyama nyie ni binadamu
Pathetic!!!
Mnavyobaguana mkiwa huko Moshi Mara huyu ni mrombo mkibosho Mana dhambi ya ukabila itakula mpaka ukiwa mrombo utaanza kuangalia Koo kiubaguzi.mtabaguana mpaka family level.
Kwanza ivi Kuna wachaga kwani Kuna kabila la kichaga kweli Mana wilaya moja makabila Kama kumi tofautitofauti.
Mie hata mchaga bure sioi
 
Uchunguzi ufanyike aisee... Mama ni mlemavu mtoto ni binti tena form four amng'oe mama ake macho it doesn't make sense kuna mtoa kafara hapo maiki za media na camera zao hazijammulika
...Kweli, Hata haingii akilini Mkuu. Binti wa Form Four, hawa hawa Mabinti zetu tunavyowajua, apate ujasiri wa kumnyonga mama yake mzazi kilema kwa Shuka kisha apate tena Ujasiri wa kumn'goa macho maiti??
Hii ifuatiliwe vyema. Kuna la zaidi hapa....
 
Binti km alikuwa anatizama filamu basi kawa mwalimu hasa wa hizo filamu mpk kamtoa macho Mama.
 
I think she was insane at material time

Back
Top Bottom