Binti aomba msaada aendelee na masomo kidato cha tano

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
432
999
1690524637312.png

Morogoro. Binti mmoja mkazi wa Mafisa, manispaa ya Morogoro, Amina Abdul amewaomba wadau wa elimu, viongozi pamoja na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia kupata vifaa na mahitaji mbalimbali ili aweze kwenda shule ambako amechaguliwa kujiunga na kidato cha tano.

Amina ambaye amemaliza kidato cha nne mwaka 2023 katika shule ya Sekondari Kihonda iliyopo manispaa ya Morogoro na kufaulu kwa daraja la kwanza katika mchepuo wa biashara, amechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule ya Sekondari Bukongo iliyopo wilaya ya Ukerewe jijini Mwanza.
Fomu ya mahitaji ya mwanafunzi hii hapa

Namba ya kutoa msaada inayopatikana 0782976551 au 0715185912 mama yake mzazi.
Hata hivyo, kutokana na hali duni ya maisha ya wazazi wake, ameshindwa kununua vifaa na mahitaji muhimu ya shule yaliyoorodheshwa kwenye fomu ya kujiunga na shule hiyo.
Mbali ya kuomba msaada huo, Amina ameomba pia kubadilishiwa shule ili aweze kusoma mkoani Morogoro ambako ataweza kuwa karibu na wazazi wake ambapo baba yake anaugua kwa muda mrefu.
“Baba yangu anaumwa kwa muda mrefu, babu yangu mzaa mama amepofuka macho kutokana na ugonjwa wa presha ya macho, mhudumiaji mkubwa kwenye familia yetu ni mama. Kwa hiyo, hana uwezo wa kumudu gharama za mahitaji yanayohitajika,” amesema Amina.
Msichana huyo amesema katika kipindi chote alichokuwa anasoma, alikuwa akilazimika kufanya biashara ndogondogo siku za mwisho wa wiki ili aweze kupata mahitaji mbalimbali yakiwemo madaftari, sabuni, sare za shule na nauli ya kwenda shule na kurudi nyumbani.
“Nilikuwa nauza karanga na biashara nyingine ili niweze kumsaidia mama kupata mahitaji yangu ya shule, kiumweli nimesoma katika mazingira magumu sana. Hata hivyo, nashukuru nilifaulu vizuri na hatimaye nimechaguliwa kujiunga na kidato cha tano,” amesema.

Amina amesema kuwa bidii yake aliyoweka kwenye masomo ya biashara anatamani kuwa mhasibu, anamuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia kwa kumpatia ufadhili ili aweze kusoma.
Akizungumza na Mwananchi, baba mzazi wa binti huyo, Abdul Salum amesema huyo ndiyo mtoto ambaye anaamini atakuwa na msaada kwake kwa kuwa ana moyo wa kusoma na amekuwa mtoto mtiifu na mtulivu.
“Nina watoto wawili, mmoja alipewa ujauzito akiwa kidato cha pili na wa pili ndiyo huyu ambaye namuona ana moyo wa kusoma, hivyo naiomba Serikali inisaidie kumpatia vifaa na mahitaji yaliyoorodheshwa kwenye fomu aweze kutimiza ndoto zake.
“Mimi hapa nilipo ni masikini sina hata cha kuuza Ili nimpeleke mwanangu shule na akikaa hapa mtaani ndoto zake zitapotea,” amesema Abdul.
Amesema anaamini kuwa binti yake huyo akisoma anaweza akapata kazi na atakuwa mkombozi na msaada kwake kama mzazi na familia kwa ujumla.
Mzazi huyo amesema kama atatokea mdau au kiongozi atakayeguswa kumsaidia binti yake anaweza kuwasiliana naye kwa namba ya simu – 0782976551 au 0715185912

CREDIT: MWANANCHI
 
View attachment 2701141

Yule mbunge wao anayetoa basi kusafirisha mtu akifa hili la elimu kwake sio muhimu sana. Babu Tale vipi?
 
Nitamkumbuka kwa message ya: Imethibitishwa umepokea. Watu wa aina hii hufanikiwa sana.
 
Jibu la kipuuzi mno kwenye shida, ni kawaida ya mazuzu wa middle class wa kitanzania kuona kinachotokea kwa jirani yake kwake hakitamtokea,mada zingine ukiona hauna mchango wa maana just shut up
Tuliambiwa tukichagua kijinga tutaambulia ujinga. Sasa kutaka kujua Mbunge wake kafanya nini juu ya kadhia ya huyu binti unasema nimechangia kipuuzi. Narudia tena kuuliza yule anaye toa magari kwenda kuzika hili la elimu kwake sio muhimu.
 
Hana kanisa au msikiti anaosali maana nadhani mahitaji yake ya shule hayawezi zidi 300000 kwa nusu muhula
 
Tuliambiwa tukichagua kijinga tutaambulia ujinga. Sasa kutaka kujua Mbunge wake kafanya nini juu ya kadhia ya huyu binti unasema nimechangia kipuuzi. Narudia tena kuuliza yule anaye toa magari kwenda kuzika hili la elimu kwake sio muhimu.
No no mkuu, msaada sio kwa matajiri tu kuutoa, usiifanye issue ya mtoto huyu kuwa ya kisiasa, aliyetoa tamko hilo alikua ni politician!,uongo mkubwa usiokua na aibu, mtoto huyu anahitaji msaada, mkuu mimi na wewe tusaidiane hata kuchangia 25%ya vifaa vya shule
 
Tuliambiwa tukichagua kijinga tutaambulia ujinga. Sasa kutaka kujua Mbunge wake kafanya nini juu ya kadhia ya huyu binti unasema nimechangia kipuuzi. Narudia tena kuuliza yule anaye toa magari kwenda kuzika hili la elimu kwake sio muhimu.
Mkuu, bora ungekaa kimya kama huwezi msaidia huyo binti, wengine tutatoa kidogo tulichonacho
 
Hiyo si hekima hata kidogo, kama familia yako ina uhitaji huo ungekaa kimya ukaacha kuwasemea na wengine watakaochangia.
Utachanga wewe ama sifa za kijinga tu unatafuta, hakuna na hayupo Mtanzania mwenye hekima ya kuchangia elimu hayupo. Tembelea vijijini ujionee Mkurugenzi anatembelea V8 lakini kuna watoto wanakaa chini.
 
Asante mkuu, tufunge mjadala, kwani matusi na lugha za maudhi si hulka yangu. Mimi nitachanga kidogo nilichonacho
 
Upo right mkuu, jumuika Nami kuchangia kidogo
Asante mkuu, tufunge mjadala, kwani matusi na lugha za maudhi si hulka yangu. Mimi nitachanga kidogo nilichonacho
Upo right mkuu, changia kidogo ulichokua nacho,jumuika nami just to make a small difference kwa binti huyu, mama yake anaitwa Mariam Ramadhani na namba inasoma jina lake, kuna watu wana roho ngumu na mbaya mno humu, kutwa kulalama tu
 
Back
Top Bottom