Kilimanjaro: Binti adaiwa kumuua mama yake kisha kumng’oa macho

Acheni hizi hukumu za kimakundi na kikabila.
Unataka kusema hakuna watu wema uchagani au watu wabaya kwenye kabila lako?
NB: Mimi siyo mchagga.
Nikionaga mtu anakemea mambo ya ukabila napenda sana. Nachukia sana watu wanaoutukuza pia. Mimi katika kukua kwangu nilikua nasaidiwa na watu wa makabila mbalimbali na sometimes wanakupenda tu kuliko hata ndugu zangu.
 
Mnavyobaguana mkiwa huko Moshi Mara huyu ni mrombo mkibosho Mana dhambi ya ukabila itakula mpaka ukiwa mrombo utaanza kuangalia Koo kiubaguzi.mtabaguana mpaka family level.
Kwanza ivi Kuna wachaga kwani Kuna kabila la kichaga kweli Mana wilaya moja makabila Kama kumi tofautitofauti.
Mie hata mchaga bure sioi

halafu mnataka chadema itawale nchi wachaga watupu tutakwisha
 

Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Kindi Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro anadaiwa kumuua mama yake mzazi, Marietha Mushi (62) kwa kumnyonga na shuka, kisha kumpiga na kitu kizito kichwani na kumng’oa macho.

Habari zinaeleza kuwa mama huyo alikuwa na ulemavu wa mkono jambo linalodaiwa kuchangia ashindwe kujitetea wakati akishambuliwa na binti yake huyo.

Akizungumza na Mwananchi Digital Jumanne Julai 6, 2021 mkuu wa Wilaya ya Moshi, Said Mtanda amesema tukio hilo limetokea Julai 5, 2021 eneo la Kibosho Sambarai.

"Mtoto amemuua mama yake na mtoa taarifa ambaye ni kaka wa marehemu ameeleza kuwa alibaini kuuawa kwa dada yake kwa kunyongwa na shuka kisha kupigwa na kitu kizito kwenye paji la uso. Alisema aling’olewa macho na huyu mwanaye wa kike ambaye anasoma kidato cha nne,” amesema Mtanda.

Amesema mwanafunzi huyo amekamatwa na uchunguzi wa Polisi unaendelea

Source: Mwananchi Newspaper
Ili tukio natamani sana kuendelea kulijua ili nijue mwisho wake lakini sizani kama uyo mtoto atakuwa ndo muhusika mkuu wa tukio hilo kunakitu kimejificha apa..
 
Huko Kirimanjaro nako kuna mambo ya ajabuajabu sana.
Nakumbuka miaka ya nyumba Mwalimu mmoja wa shule ya msingi alimkata kichwa mama yake mzazi na kwenda kukitupa kichwa kwenye mashamba ya mpunga! What's going on there friends?
 
Acheni hizo kaka aangushe jumba kwa lipi?. Acheni kuwachochea polisi maana hawa jamaa huwa ni kipigo kikali katika kupata taarifa wasije mchapa kaka bure. Ukute kaka anaishi mbali na familia na hapo wanaishi wawili tu mama na binti kaka kapewa taarifa ya kifo akaja fasta ndio kutoa taarifa. Tuache ujuaji.
 
Binti mdogo halafu kamuua mama yake,kamnyonga,halafu baada ya kufa kampiga na kitu kizito,halafu kamtoa na macho,hapa uchunguzi wa kina unahitajika kwanini ampige na kitu kizito baada ya kumnyonga,na hayo macho kwanini kayatoa kama lengo lilikuwa ni kumuua tu...?
Alitoboa ili kupoteza ushahidi maana mtu akifa kwenye macho image ya vitu vya mwisho kuviona huwa inabaki machoni.

Hapo kuna mchezo unaendelea kwanza inaonekana muaji ni mtu mwenye uzoefu, pili huyo mtoa taarifa alijja kuea huyo bint ndio kahusika ?
 
Jamaa kwa hela tu hawajambo.yaani manka kukuua afu zile hela ziende kwao ni kawaida Sana na anasifiwa huko kwao na kufanyiwa party kuwa wewe ni jasiri mwanetu
Kina Manka bwana wana roho ngumu sana katika maamuzi ya pesa na uhai wa mtu....sasa basi, angalia wanavyopenda dini utafikiri ndiyo wao walioanzisha hapa duniani. Mchana na jioni kutwa kuswali, usiku wanaruka kushindana na popo na bundi kwenda kufinya watu waliolala majumbani mwao.
 
Ili tukio natamani sana kuendelea kulijua ili nijue mwisho wake lakini sizani kama uyo mtoto atakuwa ndo muhusika mkuu wa tukio hilo kunakitu kimejificha apa..
Ngoja tuone uchunguzi wa Polisi utatoa majibu gani
 
Back
Top Bottom