Bibi harusi mtarajiwa, mama yake wafa ajalini wakielekea Kilimanjaro kwenye maandilizi ya harusi yake

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
996
Bibi harusi.png

Bibi harusi mtarajiwa, Rehema Chao (37) na mama yake mzazi, Agness Chao (75) wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Raum kugonga lori.

Ajali hiyo iliyotokea baada ya Rehema aliyekuwa dereva wa gari hilo kukwepa shimo na kugongana na lori, pia imesababisha kifo cha mfanyakazi wa ndani wa mdogo wake, Irene Shija (15), huku wanafamilia wengine wawili wakijeruhiwa.

Ajali hiyo ilitokea jana Novemba 28,2023 katika eneo la Kichwa cha Ng'ombe, wilayani Mwanga, wakati Rehema akitokea mkoani Morogoro kwenye sherehe ya kuagwa (send-off) iliyofanyika Novemba 24,2023.

Rehema aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Sua, mkoani Morogoro alikuwa akirejea nyumbani kwao Marangu, Moshi akiambatana na familia yake kwa ajili ya maandalizi ya harusi iliyopangwa kufungwa Desemba 2,2023 mkoani Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alithibitisha ajali hiyo akisema wanamshikilia dereva wa lori, Joachim Meela (37) kwa mahojiano zaidi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Abdallah Mwaipaya, amewataja majeruhi kuwa, Veronika Chao (35), mdogo wa Rehema ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Nguzo Mbili, Geita na mwanaye, Jayden Erasto (2).

"Jana kulitokea ajali katika wilaya yetu ya Mwanga, iliyosababishwa na magari mawili, lori aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na mkazi wa Moshi likitokea Arusha kwenda Dar es Salaam lililogongana na Toyota Raum likitokea Morogoro kwenda Marangu,” amesema.

Mwaipaya amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Kituo cha Afya Kisangara, wilayani Mwanga, huku majeruhi wakiendelea na matibabu katika kituo hicho.

Ndugu, marafiki wanena
Ndugu wa marehemu, Elielisa Kombe ameiambia Mwananchi Digital kuwa, harusi ya Rehema ilikuwa ifanyike Oldonyosambo, mkoani Arusha.

Kombe amesema gari lililokuwa na watu watano wa familia moja, wakazi wa Msae Nganyeni, Marangu lilipata ajali wakati Rehema akikwepa shimo.

"Gari lilikuwa na watu watano, mama na watoto wake wawili, mjukuu na msichana wa kazi, ni majonzi makubwa kwa familia," amesema Kombe.

Amesema wamepanga maziko kufanyika Jumamosi, Desemba 2,2023. Amesema wanaendelea na vikao kwa kuzishirikisha pande zote mbili.

"Tunaendelea na vikao kwa sasa, kesho ni lazima tukae pande zote mbili, upande wa waoaji na sisi, lakini tunatarajia kuzika Jumamosi," amesema.

Happyness Msacky, mwalimu mwenzake na Rehema katika Shule ya Sekondari Sua, amesema wamepokea kwa masikitiko msiba huo.

Amesema walikuwa wote siku ya sherehe wakifurahi pamoja na mtumishi mwenzao.

"Msiba huu umetuuma sana, Rehema alikuwa na familia yake, yeye ndiye alikuwa dereva. Hili ni pigo kubwa kwa familia, hatuna cha kusema zaidi ni kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu," amesema.

Mwananchi
 
Poleni wafiwa na wote mlioguswa na msiba huu. Lakin nadhani haikuwa busara kwa kumwachà bibi harusi mtarajiwa kuendesha gari safari ndefu namna hiyo; kwanza alikuwa hyper excited kwa ajili ya arusi na mchecheto wa arusi. Haikuwa busara kabisa kumpa usukani. Apumzike kwa amani. Pole bwana arusi mtarajiwa😭
 
Back
Top Bottom