Nimetamani kusimulia hiki kisa muda sasa lakini waungwana walikuwa hawajatoa ruhusa bado.
Nilipotea kwa vipindi viwili vyenye jumla ya siku 23, kati ya siku hizo ni siku chache sana nilikuwa nje ya Tanzania, nyingine zote nilikuwa hapa hapa ila kwenye dunia isiyoaminika na wengi, dunia ya ushirikina na uchawi katika uhalisia wake.
Nitangulie kuomba radhi sitaandika kila kitu bali yale ya muhimu tu nitakayoona ni muhimu kuandika.
Nilitoka Dar kwa dharura kuelekea sehemu ambako nitapata kile kinachonipeleka huko, safari yangu ikanipeleka mpaka Nyamisati, nikalala pale.
Siku ya pili asubuhi nikadamkia bandari bubu iitwayo gezani.... vituko vilianzia hapo.
Hizi njaa zako naona zinazidi kukupeleka pabaya sasa, unakaa unakiaminisha hiki kizazi kipya kinachotegemewa kuliendesha hili taifa siku za mbele mambo ya kufikirika na kishirikina bila kua na ithbati yeyote?
Hivi ni nchi gani iliyoendelea kiuchumi kwa kufuata imani za kishirikina na kusadikika? Nini lengo lako la kuwaaminisha hasa vijana mambo ya kutunga?
Nini lengo lako hasa?
Najua njaa ndio inayokusumbua na hakuna kingine,unawabrainwash vijana ili wakuone ni kama "mtaalam" fulani wa kichawi,ili wajenge tamaa kwamba wewe ndio kimbilio lao la kuwasaidia kufikia malengo yao!
Tena una kiteam chako humu ulichokitengeneza kwa lengo maalum la kukusapoti ili kuwahadaa na kuwavutia na wengine!
Wapo wanaojifanya wana promise ya kuonana na wewe au kujifanya eti wanakutumia msg private ili kuwahadaa wengine,
Mchezo unaoufanya ni sawa na wale wacheza karata 3 kekundu na keusi,kuna watu hua wanajifanya ni "wateja" wanakua wanakula pesa nyingi ili kuwahadaa na wengine watumbukiemo! Hiyo ndio kazi ya kigroup ulichokitengeneza ili kifuatane nawe kila thread kukusafishia njia ya kuwahadaa na wengine!
Acha hizo, unahadaa vijana ambao ni tegemeo kubwa kwa taifa na familia zao, tafuta shughuli ya kufanya kuliko kushinda JF mchana kutwa na usiku kucha ukiandika thread za kupotosha vijana kila baada ya dakika kadhaa!
Hizo hadithi unazoziandika zilikua zikisimuliwa zamani sana kupitia Radio tanzania RTD kipindi cha watoto cha MAMA NA MWANA.