Kwa ninayoyaona target ya nyoka pale bustanini haikuwa mwanamke

Kwa ninayoyaona target ya nyoka pale bustanini haikuwa mwanamke

Afisa_Nkai

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2025
Posts
418
Reaction score
839
Wakuu mimi niko salama!.
Nirudi kwenye mada nimekuja kugundua target ya nyoka pale bustanini haikuwa mwanamke kabisa, ingekuwa ni mwanamke basi eva alipokula tu lile tunda biashara ingeishia pale pale lakini kwanini sasa ilimfikia mwanaume?, kumaanisha kwamba target ya nyoka ilikuwa ni mwanaume, nyoka alimtumia mwanamke kumfikia mwanaume.

Ukiacha kula tunda ni kitu gani kingine nyoka alizingumza na mwanamke na ukitaka kujua kilichozungumzwa unapaswa uangalie kile ambacho mwanamke anakifanya nyuma ya haya yote, na kwa kuwa target ni mwanaume angalia namna ambavyo mwanamke anaenenda kinyume na mwanaume, hapo ndo unakuja kugundua kumbe wanawake hawahitaji mume, hawahitaji mpenzi kama ambavyo wanajinasibu kwenye mitandao they just need SLAVE (mtumwa).

Target ya mazungumzo ya pale bustanini ukiachana na kula tunda ilikuwa ni kuhakikisha mwanaume anakuwa mtumwa wa mwanamke, kwa namna gani ushawahi kuona mwanamke kabisa anajinasibu anataka mwanaume ambae ni provider, provider kwa namna gani sasa yaani provider ni mtu ambae anatafta kwaajili yake, na ukijaribu kwenda kinyume na hapo wanakwambia kuwa Mungu alisema utatafta kwa jasho, sasa kutafta kwa jasho na mimi mwanaume kuwa provide wako inaingilianaje an how come.

Nachoka mimi na haya mambo and what is the real essence of this life.
 
Kumhudumia mwanamke sio lazima. Ni hiyari(upendo) wako.
Hakuna amri ya lazima ya Mume kumhudumia mke. Kaangalie torati ya Musa kama ni suala la Sheria alizozishusha Mungu wa biblia.

Sheria inasema, Fanya kazi kwa Siku sita. Sheria hiyo haijataja mwanamke au mwanaume. Ni wote sharti wafanye KAZI.

Ni kiherehere na ujinga wa wanaume kujifanya wanaowajibu wa kuhudumia Wake zao Jambo ambalo sio lazima bali ni hiyari kama vile wanawake nao wanahiyari ya kuhudumia waume zao.
 
Sahihi kwamba hakuna amri ya lazima ya mume kumhudumia mwanamke, shida ni mwanamke mwenyew anataka mwanaume provider n.k
 
Kosa kwenye hiyo simulizi lilikuwa ni uchaguzi mbaya.

Kwani Eva alimshikia bunduki Adamu kumlazimisha ale tunda?
kwahiyo kitendo cha adam kukubali kula tunda ilikuwa ni bad move kama kwenye game of chess ♟️ 😂
 
Sahihi kwamba hakuna amri ya lazima ya mume kumhudumia mwanamke, shida ni mwanamke mwenyew anataka mwanaume provider n.k

Wanaume ndio tuliiweka hiyo amri makusudi ili tuwatawale wanawake.

Unafikiri wanawake wakijilisha wenyewe wanaume wataweza kuwatawala?
 
Nyoka alikuwa ni mwalimu wa mwanga, katika Gnosticism, sisi tunamuheshimu sana nyoka. Ndiye mfunua siri wetu! Ni ishara ya ukombozi wa kimtazamo na kifikra, mwanzilishi wa udadisi! Kupitia nyoka tulikombolewa kutoka katika utumwa wa kifikra.
 
Sahihi
 
Back
Top Bottom