Kile kipindi ambacho nilipotea

Kile kipindi ambacho nilipotea

Nikataka kumvagaa! Jogoo akanirukia akanikaba shingoni!.... Inaendelea!..............[/QUOTE]
Hahah mkuu kahawa yako kali sana jogoo akakukaba shingoni
 
Nikataka kumvagaa! Jogoo akanirukia akanikaba shingoni!.... Inaendelea!..............
Hahah mkuu kahawa yako kali sana jogoo akakukaba shingoni[/QUOTE]Dilute na kiroba kidogo
 
[/QUOTE]Dilute na kiroba kidogo
Hahaha viroba adimu sahiv mkuu
 
Dilute na kiroba kidogo
Hahaha viroba adimu sahiv mkuu[/QUOTE] 😳 😳 😳
 
Nimetamani kusimulia hiki kisa muda sasa lakini waungwana walikuwa hawajatoa ruhusa bado.

Nilipotea kwa vipindi viwili vyenye jumla ya siku 23, kati ya siku hizo ni siku chache sana nilikuwa nje ya Tanzania, nyingine zote nilikuwa hapa hapa ila kwenye dunia isiyoaminika na wengi, dunia ya ushirikina na uchawi katika uhalisia wake.

Nitangulie kuomba radhi sitaandika kila kitu bali yale ya muhimu tu nitakayoona ni muhimu kuandika.

Nilitoka Dar kwa dharura kuelekea sehemu ambako nitapata kile kinachonipeleka huko, safari yangu ikanipeleka mpaka Nyamisati, nikalala pale.

Siku ya pili asubuhi nikadamkia bandari bubu iitwayo gezani.... vituko vilianzia hapo.
Nikiwa pale bandari bubu upande wa pili wa bahari nikamwona mtu mrefu sana akiwa kavaa kanzu nyeupe na kitambaa kichwani Chenye rangi nyeusi na nyeupe hiki kitambaa kilimfunika uso wote kasoro macho
Huyu mtu mrefu sana alikuwa anatembea kwenye tope kuja tulipo (kumbuka ilikuwa maji kupwa )mshangao wangu ulikuwa ni yule jamaa kutembea juu ya tope bichi bila kuzama na kanzu yake nyeupe
Ilibidi niwaambie wenyeji wangu wale vijana wala majani wakanicheka sana wakasema hakuna kitu kama hicho hayo ni maruerue tu ya 'bichi'
Sikutaka kuendeleza ubishani kwakuwa najua ila yule mtu mrefu alikuja na kutupita karibu kabisa...mimi nilimuona wengine hawakumuona
Nilirejea Nyamisati kutoka pale gezani bandari bubu jioni ya siku hiyo, nikiwa na mipango ya kwenda Mafia lakini kufika pale nikakuta boat jahazi imeshajaa hivyo nikapewa matumaini ya kuondoka mchana wa kesho yake kulingana na mahitaji ya abiria kuwa wengi
Inaendelea......
Kwa bahati nzuri siku ile ya pili (sitataja tarehe)abiria wakawa wengi hivyo ikabidi kile chombo kilichoondoka alfajiri kigeuze
Bandari ya Nyamisati sio user friendly, ili uweze kupanda chombo inakubidi uchumpe kwenye mawe yaliyoko juu ya matope na ngazi ya chombo ni mbao ambazo tayari zina majimaji na tope
Ndani ya chombo hakuna siti kuna mabenchi machache tu hivyo watu hugombania kupanda ili kuwahi sehemu ya kukaa
Mimi niliwahi kupanda na kupata seat ya benchi katikati ya chombo bila kuteleza wala kupata dhahama za matope
Abiria walikuwa wengi na walipanda kwa kugombea ili kupata sehemu ya kukaa (safari ya kutoka Nyamisati mpaka Mafia ni masaa mane)kama bahari ikiwa imetulia
Ni wakati abiria wote wameshapanda na karibia nusu wakiwa wamekosa sehemu ya kuketi aliingia yule mtu mrefu na mavazi yake yaleyale na akaenda mbele kwenye benchi la mwisho kabla ya sehemu ile ya nanga akakaa
Hiki kitendo kiliwashangaza wengi kwakuwa hakuna aliyedhani kuwa pale kuna nafasi, tulisafiri salama mpaka mafia huku tukipiga story za kawaida za kufahamiana ndani ya chombo
Huyu ndugu huyu hakuongea na mtu wala kufunua uso wake kuanzia mwanzo wa safari mpaka mwisho
Kwa kawaida mnapokaribia kumaliza safari nahodha hukagua upya tiketi na kuzikusanya, kwenye hili zoezi yule ndugu hakuguswa kabisa, niliona kwa macho yangu hilo (nilidhani ni stuff, nilikuja kumuuliza nahodha tukiwa Mafia lakini akakataa kata kata kuwa na abiria wa namna hiyo chomboni
Tuendelee.....
Kile kitendo cha nahodha kumkana yule abiria ambaye hata shiva yake pale bandari ya mafia kiliniacha na maswali na tafakuri kuu! Yeye ndio alikuwa abiria wa kwanza kushuka na kwa taratibu za pale bandarini mafia gati lina urefu karibia kilometre moja (gati la vyuma)hivyo kuna magari maalum ya abiria huchukua watu kwa nauli ileile na kuwapeleka mpaka pwani! Wasiojua ama kutopenda kupanda gari hutembea kwa miguu lakini mtawapita njiani mkiwa garini
Yule ndugu hakupanda gari na sikumuona popote mpaka tunafika pwani
Tuendelee....
Ukishuka pale kilindoni Mafia bandarini, hotel nzuri ya kwanza ambayo ni standard na bei yake ni nzuri ni IBIZA, Ni pazuri panafaa panavutia, nilifikia hapo na kuwasiliana na wana JF ambao ikiwapendeza watakuja wenyewe hapa ila kwasasa siwezi kuwataja bila ruhusa yao
Nililala Ibiza na kesho yake nikaenda visiwa vingine vilivyo karibu na mafia (nakumbuka nilitupia picha hapa bila watu wengi kujua huko ni wapi) nilishinda huko na kurejea mafia jioni ya siku hiyohoyo
Kwa bahati mbaya sana kufika Ibiza ikawa vyumba vimejaa, wapambe wa pm walikuwa wamebanana hapo kwakuwa ilikuwa ni kipindi kile Majaliwa yuko kule
Sikuwa pekeyangu niliyekosa chumba pale tulikuwa wengi, kuna gest nyuma tu ya Ibiza ila nayo ilikuwa full ya karibu vingine ilikuwa ni kama mwendo wa dk 15 na bei ilikuwa mbaya...wengi tulishindwa
Kufikia saa tano usiku tukapata kigesti change shilling 12000, vyumba sio self..nilikuwa na raia wengine wa nje tukachukua vyumba 4 kila mtu na chake
Hii gesti ilinishangaza sana
Ilikuwa ina harufu ya udongo mbichi uliochanganyikana na harufu ya ukale
Ilikuwa ni kama inaelea ukiwa ndani ni hisia isiyoelezeka
Taa zake zote zilikuwa hafifu sana
Kubwa kuliko yote ilipofika saa sita usiku(nilikuwa macho bado nafanya tahajudi)nikahisi kichwa kuvimba na nywele kusisimka..! Haikuchukua muda umeme ukakatika
Lakini pia kukawa na harufu kali ya mchele, nilichoropoka chumbani, hamad nafika kwenye korido nikamuona yule ndugu anaishia mwisho wa gesti, nilimtambua Kwa mavazi yake
Inaendelea
Kiukweli ni kwamba nilisizi, Lakini Sikuwa pekeyangu karibia wapangaji kama wane hivi walitoka vyumbani mwao
Mimi sikurudi tena kulala mule ndani nilichukua kibegi changu na kwenda kukesha Ibiza mpaka alfajiri nilipotimkia bandarini
Tukiwa kwenye boat kurejea Nyamisati story zilikuwa za ile gesti na vituko walivyokumbana navyo usiku mzima, hasa ile harufu ya udongo mbichi na mchele, kuna baadhi walijiapiza kuwa hawatakaa warudi Mafia
Tulifika Nyamisati saa tatu hivi asubuhi bila kituko chochote....nilipumzika mpaka mchana tulipokodi fiber boat kwenda kwenye visiwa vilivyo karibu na hapo Nyamisati
Sorry kwa kupotea hewani si kweli kwamba jitu refu lilinitumbua...
Tuendeleee
Pale Nyamisati kuna fiber boats nyingi za kukodi ila sisi tulipata shida kweli kupata moja, mwishowe kijana mmoja akatuambua boat inayotufaa sisi ni ya jamaa anaitwa rasta nyoka
Basi akatafutwa na ndani ya dakika kumi akawa kafika
Huyu jamaa ni mrefu mweusi mwembamba mwenye rasta zilizofungwa kitambaa kote ndefu karibia na kiuno
Tulipatana na kuondoka Nyamisati saa saba mchana, nilikuwa nimeshamweleza kuwa tunataka kufanya ziara kwenye visiwa visivyopungua kumi, akasema hakuna shida kwakuwa kote anakufahamu vema
Ni baada ya kupanda ile boat na kuondoka pale ndio mwili wangu uliota vipele kwa taharuki, na hii ni baada ya kusikia ile harufu ya udongo na mchele, nilimwangalia nahodha wetu kwa kuibia na kugundua ni yule yule bwana
Hata wale raia niliokuwa nao niliweza kuona hofu ya wazi kwenye nyuso zao! Tuliangaliana wote bila kuongeleshana chochote
zile harufu za udongo na mchele zikawa zinakuja na kutoweka hapo tayari tukiwa kwenye mapori ya mikoko ndani ya bahari kuu
Ilibidi niweke hofu pembeni na kuanza kuongea na nahodha! Hakuwa mtu wa kawaida anafahamu mengi ya bahari mengi sana na ilikuwa akipiga story ya kutisha kuna wakati alikuwa anarusha mate kama nyoka...hii niliishuhudia si chini ya mara kumi
Visiwa hivi vilivyoko karibu na Nyamisati karibia vyote vimezungukwa na mikoko na kwa baadhi ya sehemu kuna vijiji na kwingine kuna kambi za uvuvi na kilimo, ni visiwa ambavyo viko naweza kusema nje ya utaratibu wa dunia, huko dili kubwa ni uchawi na kusafirisha mikoko
Rasta nyoka nahodha wetu ni mtu maarufu huko huko visiwani lakini unaweza kufika Nyamisati ukawaulizia kuhusu yeye na hakuna mtu anaweza kukiri kumfahamu! Yeye ndio mwamuzi wa kutaka akumbukwe au adahauliwe
Tulikuja kuweka kambi kisiwa kimoja kinaitwa Kilwani karibu na meli kubwa ya wajerumani iliyoachwa hapo wakati wa vita ya pili ya dunia, kwasasa haionekani tena imezama kabisa
Rasta nyoka Huyu nahodha wetu ndio yule jamaa mrefu , alitusimulia mengi kwa sharti la kutoyasema popote nami sitayasema hapa...nitaandika yale aliyokubali tu kusemwa, Huyu jamaa husafiri bure popote kama akiamua hula chochote popote bila kulipa, mambo anayofanya si kwa utashi wake bali kuna roho ndio zinamuongoza
Rasta zake si nywele kama nywele za kawaida, gesti tuliyolala anasema ni kituo na mapito, muda mwingi huishi huko visiwani kwenye mapori ya mikoko
Husaidia majahazi ya Zanzibar na Pemba kupeleka mbao za mikoko bila kukamatwa na maliasili, pesa anayolipwa hatumii yeye
Hana wazazi hana familia, amekulia visiwa vya nyamisati, mengine hayasemi mengine sitayasema
Tulifanya ziara ya woga kwenye visiwa vine tu hatukuwa tayari kulala kisiwa chochote na nahodha wetu
Tulimaliza na kisiwa cha Simbaulanga, kisiwa mdomo wa kuingia baharini au kuingia njia ya Nyamisati
Tulirejea nyamisati jioni tukalala pale, rasta nyoka hakuwepo tena hatukupeana namba sikumuona na somu hakupenda tupige picha hata moja
Kuna mengi sikuyasimulia hapa nimetii agizo , ila hapo Nyamisati Gezani , kilwani na visiwa vinginevyo Kuna siri kubwa kuhusiana na rasta nyoka...ukibahatika kwenda huko jaribu kumuulizia
Ipate full story hapo
CC: mrangi
 
Back
Top Bottom