Little Dreamer
Senior Member
- Sep 12, 2017
- 178
- 149
Habari wakuu!
Nadhani kwa kipindi hiki wengi mnaelewa katika tathnia ya usafirishaji abiria (mabasi) kumekuwa na ushindani mkunwa sana.
Yaani katika ushindani huo imefikia kipindi watu wanaingiza mabasi nchini kwa wingi kuliko kawaida, lengo ni kuweza kuhimili ushindani huo kwa kuboresha huduma ambalo ni jambo zuri sana.
Ni kawaida sana kwa sasa kampuni kama Abood kuagiza mabasi zaidi ya kumi kwa mkupuo, Shabiby mabasi kama 30 kwa mkupuo, Happy Nation kwa mkupuo analeta gari si chini ya tano, New Force nae analeta gari kwa wingi sana na kampuni nyingine nyingi.
Lakini jambo linalonishangaza ni kwamba kwa wingi huo wa mabasi na wingi wa kampuni za mabasi zinazozaliwa kila siku mbona hatusikii wakitangaza nafasi za kazi? Je kwenye hayo mabasi wanawaajiri watu gani? Kibaya zaidi ni kuwa ukienda kuomba nafasi za kazi utaambiwa nafasi zimejaa, na hapo umeenda kuomba siku hiyohiyo gari zimeingia bongo, je hizo nafasi zilijaa lini na zimejaaje?
Lakini nazipa pongezi kampuni ambazo zimejitahidi kutangaza nafasi za kazi kama Kilimanjaro express waliotangaza nafasi za mahostess na New Force ambao walitangaza nafasi za madereva, bila kusahau ABC Upper Class ambayo hivi karibuni imetangaza nafasi za mahostess, je hizo kampuni nyingine zaidi ya 50 zina tatizo gani?
Kinachonisikitisha zaidi ni kuwa baadhi ya hizo kampuni zinamilikiwa na wabunge wetu na wanasiasa ambao ndo wanaotutetea bungeni sisi wananchi kwenye masuala mbalimbali ikiwemo ajira, je mbona hatuoni kwenye mabasi yao wakiunga mkono wananchi kwa kutangaza na kuwapatia wananchi wenye vigezo kazi na kuwalipa mshahara mzuri?
Wito wangu kwa mamlaka, kama itawezekana basi kila kampuni ya mabasi isipewe usajili na kibali cha kufanya kazi endapo haitaonesha utaratibu wa kuajiri wafanyakazi na kuhakikisha malipo yao, kama hawajiwezi kwa hilo ni heri wakajipange upya maana watakuwa hawajafikia vigezo vya uwekezaji, kama hawawezi kuajiri na kulipa wafanyakazi.
Kama serikali na mamlaka zote kweli zinapambana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini basi waanze na hawa wamiliki wa mabasi maana kwa sasa mabasi ni mengi mno, hii itasaidia kuondoa wimbo la ukosefu wa ajira.
Lakini pia kwa kumalizia kuna vijana wengi wasio na kazi lakini ni wapenzi sana wa mabasi wanaojulikana kama wanazi, wengi wamekuwa wakiwashutumu kuwa kupitia staili yao ya kuyashangilia mabasi wanachochea ajali, je kama hao vijana wenye mapenzi ya dhati na baadhi ya kampuni kiasi hicho na baadhi yao wana vigezo mbona hawaajiriwi? Je, hamuoni ya kwamba mkiwaajiri watu wenye passion na mabasi mtaondoa wimbo la watu wanaoshinda barabarani kushangilia mwendokasi huku wakipigwa na maisha?
Naomba kuwasilisha🙌🏽🤝🏽