Kampuni za mabasi zatakiwa kuheshimu utaratibu-LATRA

Apr 9, 2022
66
32
Ikumbukwe kuwa tarehe 28, juni, mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa maagizo kwenye Wizara mbili, Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi pamoja na Wizara Ujenzi na Uchukuzi ya kuweka utaratibu wa Magari kuanza kutoa huduma ya usafirishaji abiria masaa ishirini na nne(24), tayari utaratibu wa kuangalia maeneo yakuanzia kufanya kazi yaisha anza kufanyika katika taasisi ngazi ya chini.

IMG-20230818-WA0806.jpg

Johansen Kahatano Mkurugenzi Mdhibiti Usafiri wa Barabara kutoka (LATRA), amesema tayari wameanza kuchukua hatua licha ya kubaini changamoto mbalimbali zilizojitokeza barabarani wakati wa usiku ikiwa ni pamoja na mabasi kwenda mwendo wa kasi na kuharibika njiani pasipo kupata msaada.

Amesema kuwa hivi karibuni yamejitokeza baadhi ya Kampuni ambao wameanza kutoa huduma nje ya ratiba ambazo wamepangiwa, kuna mabasi ambayo yanaanza safari saa mbili na saa moja yanatembea usiku kucha kwenda sehemu mbalimbali ya Nchi.

IMG-20230818-WA0804.jpg

"Sasa hii inakuwa ni kinyume na kanuni na kila gari linapaswa kufuata ratiba yake ambayo wamepewa, lakini pia tumebaini kunachangamoto ambazo zimejitokeza hivi karibuni mabasi kuharibika usiku wa manane, kwendwa mwendo wa kasi kwa kujua kwamba huko njiani Askari hawapo, na sisi tunawafuatilia tukipata taarifa kama hizo tunawapigia Polisi sasa wanapokuwa hawapo, maana yake wanaona kuna njia inakuwa wazi kwao kufanya wanachotaka, tumeona tupeleke ujumbe huu waache kufanya hivyo kwa sababu wanavunja kanuni" alisema Johansen.

IMG-20230818-WA0805.jpg

Anafafanua kwamba Wananchi ambao labda wangeona huduma hii sasa waanze kutumia ni kwamba bado haijakuwa tayari hivyo wawape nafasi wakati wanafanya maandalizi ya msingi yenye nia njema, wanapoanza sasa na zile changamoto walizozisema kama Magari kwenda kasi, kuharibika njiani pasipo kupata msaada zisiwepo.

"Kila mtu ajue naanza safari na atafika salama, kwaiyo ambacho sasa hivi tungependa kifanyike wale ambao wanania ya kutoa huduma hiyo waanze kuleta maombi ili hata Serikali itakapo fanya maamuzi baadaye kwamba sasa tunaanza, tujue hata uhitaji ni mkubwa kwa kiasi gani, na ni kwa maeneo yapi huduma hii zinahitaji kuanza kutolewa, kwa hiyo ndio rai yetu na maombi kwa mamlaka hasa Wananchi wasitumie hizo huduma za usiku" alisema Kahatano.

Hata hivyo Kahatano amesema Kuna kampuni tatu ambazo zinekiuka taratibu za mamlaka hiyo ambapo tayari wameshawapiga faini kutokana na changamoto hizo, mbali na onyo hilo amezitaka Kampuni za Mabasi yaendayo masafa marefu amabayo yanayotaka kuanza safari zake saa 24 wafanye maombi ili waweze kutumia huduma hiyo.
 
Safi sana, maendeleo ni pamoja na watu kuwa na uhuru wa kusafiri 24 hrs...
 
Back
Top Bottom