Rais Kikwete pamoja na Ujumbe wake wanategemea kukutana na Watanzania huko Los Angeles (CA),Kutakuwa na utambulisho na baadaye Rais ataongea na kujibu baadhi ya maswali ya Watanzania waishio huko,Ili kujua utaratibu na venue wasiliana na mratibu wa shughuli hiyo Ms.Assenga au Uongozi wa Watanzania Los Angeles.
Rais atakutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara weusi (African American) waishio huko Los Angeles na miji ya karibu na siku ya Jumatano Jioni atahudhuria hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na USDFA,Kutokana na Mchango wake Binafsi wa kupambana na maradhi na kuboresha Ustawi wa Afya ya Jamii Tanzania na Afrika kwa ujumla...Sifa na maneno hayo yapo kwenye kadi ya mualiko wa shughuli hiyo iliyoandaliwa na CEO wa USDFA, Bw.Ted Alemayehu.
Katika ratiba ya awali ilielezwa kuwa Rais alikuwa na safari ya kwenda Houston (TX) kuzindua DICOTA "Diaspora Council Of Tanzanians in US" uzinduzi uliopangwa kufanyika tarehe 20/may...Uzinduzi wa organization hiyo umeaahirishwa mpaka Septemba,Rais atakapokuja tena kwenye General Assembly.Kamati ya Uandaaji wa shughuli hiyo inayoongozwa na Dr.Lennard Tenende imethibitisha kutokuwepo kwa shughuli hiyo.
Siku ya Alhamis Rais atakwenda Washington DC,ambako pamoja na mambo mengine atakutana na Uongozi wa World Bank na Uongozi wa State Department.Pia imeleezwa kuwa Rais atakutana na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ambaye yupo Washington DC kwenye mkutano wa GLCA "Global Leadership For Climate" Rais Mstaafu Mkapa anatarajia kurudi nyumbani Ijumaa.
Rais Kikwete atamaliza Ziara yake Ijumaa baada ya Mkutano na Naibu katibu Mkuu wa UN ,Dr Asha Rose Migiro.Hii ni mra ya pili kwenye mwezi huu Rais kukutana na Naibu Katibu Mkuu,mara ya kwanza ilikuwa mwanzoni mwa mwezi walipokutana Copenhagen,Denmark.Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa Dr.Migiro amekuwa karibu na siasa za Tanzania katika siku za karibuni.Rais na Ujumbe wake wanamaliza Ziara yao Ijumaa jioni!