Kikwete: Nimezungumza na Mkapa karibu saa nzima jana, hakuwa mgonjwa kusema anatia shaka

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,802
Rais mstaafu, Jakaya Kikwete leo amefika kwenye makazi ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Marehemu Benjamini Mkapa, pamoja na mambo mengine amezungumzia kumtembelea Mkapa jana hospitali wakati anaumwa.

Kikwete: Jana jioni nilikwenda kumuona hospitali, tulizungumza sana. Alikuwa na maumivu lakini siyo yale ambayo ukitoka kumuangalia mgonjwa unawaambia nimemuona mgonjwa lakini. Ni maumivu ya kawaida, tumezungumza sana karibu saa nzima nimekaa pale, tumezungumza mambo mengi kwa hiyo usiku nilipopata taarifa kwamba mzee amefariki, nikauliza kimetokea nini tena?

Kwa sababu hakua mgonjwa ambae unaweza kusema unatia shaka na nimeondoka nikimuaga nitakuja kukuona tena kesho lakini sikuombei uendelee kukaa tena hospitali, natamani nije nikusalimie nyumbani naye akasema nadhani niko vizuri. Kifo ni siri kubwa maana ungekuwa unajua basi unaweza kusema unaagana kabisa, tulizungumza tukipatana tutakutana tena tuendelee tena na mazungumzo.

Suala kubwa ni kwamba tumepoteza moja ya kiongozi mashuhuri, mtu ambae alilitumikia taifa letu vizuri kwa heshima kubwa kwa uadilifu mkubwa na kwa moyo wa upendo, la kuomba kwa watanzania katika kipindi hiki ni kuendelea kuomboleza kuwa na moyo wa ustamilivu, subra, kukubali kifo kimeumbwa na Mwenyezi Mungu, kila mmoja ndio njia yake, sisi Waislamu tunavyosema Inna Lilahi wa Inna Ilahi Rajiun maana yake sote ni waja wake, na kwake tutarejea. Tutarejea lini ni siri yake Bwana mkubwa alietuleta.

JK+mkapa.jpg
 
_Makonda anateseka akifika msibani anakaa upande wa pili tunapokaaga sisi wakati angekuwepo meza kuu na mkuu wa nchi na ndio angekuwa kati ya wanaokaribisha wageni mbalimbali kutoka nchi mbalimbali uku akiwa kwenye ulinzi mkubwa na msafara wa magari ya ikulu_

Maisha .... Haya 🤔
Tunywe bia🍻🍻🍻🤣🤣🔥
 
_Makonda anateseka akifika msibani anakaa upande wa pili tunapokaaga sisi wakati angekuwepo meza kuu na mkuu wa nchi na ndio angekuwa kati ya wanaokaribisha wageni mbalimbali kutoka nchi mbalimbali uku akiwa kwenye ulinzi mkubwa na msafara wa magari ya ikulu_

Maisha .... Haya 🤔
Tunywe bia🍻🍻🍻🤣🤣🔥
Msinihusishe kalikoroga mwenyewe
 
Back
Top Bottom