Kikwete: Nataka kurithiwa na rais kijana!

Kikwete: Nataka kurithiwa na rais kijana!

Eeeh! Yamekuwa haya...duh!

Kuhusu suala la Umri hebu tafadhali pitia posts zangu zote. Nimeshasema nikiwekewa wagombea wawili wenye uwezo na vigezo sawa(provided all other factors remain constant) ila tofauti ikaonekana kwenye Umri tu,basi I WILL VOTE FOR THE YOUNGEST CANDIDATE.This is my possition in a nutshell,Everyone has his position,so Do I ! Sasa kwa anyepinga hili aje na hoja nzito nzito ! ! !

Kuhusu kwamba mimi imeonekana nipo upande fulani,hilo nimeshaliongelea sana.Mbona mimi sijaonyesha upande mahala popote?Hebu tuache hisia mkuu ili tuwe objective katika debate.

Kuhusu kuwa na maslahi na hii hoja,yes nina maslahi nayo mkuu kwa ndiyo maana nikawahamasisha vijana wawe na uthubutu."Vijana ndiyo nguvu ya mabadiliko"(Hili lina maana pana) ,"vijana ndiyo taifa la Leo".Hizi ndizo slogan za chama changu ninachokipenda,hizi ndizo slogan powerful ambazo huwezi kuzipata mahala popote au kwenye chama chochote cha siasa Tanzania.Sasa unataka nisiwe na maslahi(Siyo binafsi) na hoja ambayo msingi wake ni slogan ya chama changu kwa vijana? Ukisoma post zangu kwa makini utajua what i feel for the youths.Hata wewe unajua nguvu ya vijana katika mapinduzi,mabadiliko yote muhimu duniani.Hivi tukipiga picha ya miaka 50 ijayo tunaona nini kama tunafanya tampering with our Interest kama vijana na kwa taifa kwa ujumla?Sasa Ndiyo maana JK kadandia,kadandia slogan ya CHADEMA


Kuhusu kuwa na post Nyingi kuliko mtu yeyote sholdn't bother you my comrade! Hii sio thread ya kwanza mimi kuchangia kwa wingi tangu nijiunge na JF karibia miaka 5.Sasa hii sijui ni kwanini inakuwa taabu kiasi hiki.Si kila mtu ana nafasi ya kuchangia?ukiangalia posts zangu nyingi nilikuwa nawajibu watu,natia watu moyo,tunajadiliana,tunafanya marekebisho sehemu isiyo sahihi na sehemu nyingine ambazo watu walikuwa wanapotosha kwa makusudi kwa nia yakukichafua chama changua au kuonyesha kwamba kuna migogoro(Hasa wale waliokuwa na ID zaidi ya Tatu ushahidi ninao ndiyo maana nimewa-ignore).Ninashauri tu watu wakubaliane na mawazo ya wengine hata kama hayawafurahishi

Kuhusu kuwa Dr.Slaa sio chaguo langu: Naomba nikueleweshe kitu kimoja mkuu,sina chaguo kwenye uchaguzi mkuu 2015 na nimeshasema.Kwanza mimi sitaki kujadili watu na katika post zangu huko nyuma umeona hoja niliyokuwa nasimamia.Hebu tuelewane mkuu.Mbona tunaandika kwa sababu ya msukumo wa hisia?

Kuhusu majibu ya hovyo hovyo:Ofcourse mara nyingi hata mimi nimejikuta katika mtego mbaya pale mtu anapoandika kitu ambacho sikipendi au nina maslahi nacho huwa naona kama vile ni majibu ya hovyo hovyo yasiyostahili but again huwa najishtukia najisahihisha kisha nafikiria sawasawa tena na kutoa uamuzi. Tuendelee na mjadala...weekend imeanza ,otherwise Asante sana comrade Vikwazo



Mkuu Peaceficky,

Asante sana kwa hiyo Observation yako.

Ila mkuu tukianza kulazimishana tena kuchangia kwenye thread mbona itakuwa tatizo? Sasa kuhusu mimi kutokuchangia kwenye thread ya inayomshushia tuhuma mwenyekiti wa chama,sikuona umuhimu wa kuchangia hiyo thread kwa sababu ni thread iliyokuwa inamjadili Freeman Mbowe.Sasa mimi sioni kama ni tija kujadili watu baadala ya issues au taasisi.Kuhusu akina Zitto,Nyakarungu kutokuchangia mimi siwezi kuwasemea

Kuhusu kutumia nguvu nyingi kuelezea hii hoja sjui unamanisha nini,sijakuelewa.Hivi mkuu unataka watu waendelee kupotosha na kuchafua watu pasipo sababu au kwa sababu wanazozijua nisichangie?Wengine hata wanachafua majina ya watu kwa makusudi na vitisho juu,hivi mkuu unataka kweli nikae kimya? But the least i can do is to handle the situation calmly! Rejea post zangu za nyuma,sijui kosa langu liko wapi?

Kuhusu thread za tuhuma za Mbowe kutupa adavantage: Hapa sielewi,Kivipi na kwanza mimi na nani?

Hebu tuendelee na mjadala , tuweke mikakati ya jinsi ambavyo tunaweza ku-transform taifa letu mkuu.Vijana ndiyo nguvu ya mabadiliko,sisi ndiyo taifa la leo.

Nikipewa options mbili za candidates mmoja akawa kijana na mwingine mzee,halafu wakawa wanalingana kila kitu kwa uwezo na vigezo then i will go for the youngest candidate! That is my position according to the prevailing sitiuation

Kuna mjadala hapo previous page nilikuwa nimemjibu Miss Parliament kuhusu dhana nzima ya 'Change' hebu fuatilia mkuu utoe maoni yako ili tuendelee na mjadala kwa sababu nakujua huwa unakuwa objective sana mara nyingi.Naamini una true spirit ya mabadiliko,najua wewe ni revolutionary(not reactionary).Hebu tulia mkuu usome post zangu utagundua hatutofautiani sana kimsimamo thogh it will difficult kwako kukubali hadharani tena ila kwa sababu wewe ni revolutionary nakupa benefit of doubt.Thanks alot!

Weekend imeanza

Ben
ni kweli mm ni revolutionary n' always nasimamia kile ninachoamini ni sahihi.

Umesema thread hii una changia kwa kuwa hutaki watu wapotoshe ukweli. Je kwenye thread juu ya tuhuma za mbowe, wale wanaosema pale chadema ni chama cha wachaga je hao hawapotoshi?
Wanaosema chadema ni kama kampuni tu ya mbowe je hao hawapotoshi?
Mbona sikuoni ukachangia pale sasa na kusaidia kueleza ukweli ili kuzuia upotoshaji?

Au na wewe unakubali cdm ni chama cha kikabila? Unakubali cdm kuwa ni kampuni ya Mbowe?

Kwanini tusitumie elimu zetu kuwaelimisha hawa wenye mawazo na fikra potofu kama hizi ili kuzuia wasiendelee kupotosha wengine hapa jamvini.

Ben narudia kukwambia tena kwamba wasomi tuna dhima kubwa sana kwa jamii yetu hasa hii ambayo % kubwa ya wananchi wake hawana elimu. Tutakaposhindwa kutimiza wajibu wetu sisi kama vijana wasomi itakua ni usaliti si tu kwa chama bali watanzania kwa ujumla.

Kuhusu kuniuliza wewe ni nani? Nimeshangazwa na swali hilo mana tunajua wewe ni Ben Saanane uliye enguliwa kugombea uenyikiti Bavicha.

Umesema pia huelewi nguvu gani niliyozungumzia kwamba unaitumia hapa kifupi ni kwamba unatumia kila aina ya ushawishi kukazania sana hii hoja ya rais ajaye awe kijana hoja ambayo haipaswi tubishane hapa mana tuna mengi ya kupambana nayo sisi kama chadema haijalishi ni viomgoz au wanachama
na tukumbuke umma huu wa watanzania umeweka matumaini yao kwetu sisi kama chadema katika kuwatetea,kuwasemea na kuwapigania tukitumia vijana wasomi ndani ya chama ambao ni pamoja na sisi hapa jamvini na wengineo wote ndani na nje ya Tz.
 
Ben
ni kweli mm ni revolutionary n' always nasimamia kile ninachoamini ni sahihi.

Umesema thread hii una changia kwa kuwa hutaki watu wapotoshe ukweli. Je kwenye thread juu ya tuhuma za mbowe, wale wanaosema pale chadema ni chama cha wachaga je hao hawapotoshi?
Wanaosema chadema ni kama kampuni tu ya mbowe je hao hawapotoshi?
Mbona sikuoni ukachangia pale sasa na kusaidia kueleza ukweli ili kuzuia upotoshaji?

Au na wewe unakubali cdm ni chama cha kikabila? Unakubali cdm kuwa ni kampuni ya Mbowe?

Kwanini tusitumie elimu zetu kuwaelimisha hawa wenye mawazo na fikra potofu kama hizi ili kuzuia wasiendelee kupotosha wengine hapa jamvini.

Ben narudia kukwambia tena kwamba wasomi tuna dhima kubwa sana kwa jamii yetu hasa hii ambayo % kubwa ya wananchi wake hawana elimu. Tutakaposhindwa kutimiza wajibu wetu sisi kama vijana wasomi itakua ni usaliti si tu kwa chama bali watanzania kwa ujumla.

Kuhusu kuniuliza wewe ni nani? Nimeshangazwa na swali hilo mana tunajua wewe ni Ben Saanane uliye enguliwa kugombea uenyikiti Bavicha.

Umesema pia huelewi nguvu gani niliyozungumzia kwamba unaitumia hapa kifupi ni kwamba unatumia kila aina ya ushawishi kukazania sana hii hoja ya rais ajaye awe kijana hoja ambayo haipaswi tubishane hapa mana tuna mengi ya kupambana nayo sisi kama chadema haijalishi ni viomgoz au wanachama
na tukumbuke umma huu wa watanzania umeweka matumaini yao kwetu sisi kama chadema katika kuwatetea,kuwasemea na kuwapigania tukitumia vijana wasomi ndani ya chama ambao ni pamoja na sisi hapa jamvini na wengineo wote ndani na nje ya Tz.

Aante sana mkuu.

Ila unaona sasa,hapo kwenye red.Hivi kuna mahala popote nimekuuliza swali kama hilo?mkuu mbona umetunga swali na kulijibu mwenyewe?anyway pengine umesoma haraka haraka hata mimi huwa nafanya hivyo sometimes.

Kuhusu maswala ya chadema kama chama cha kichaga na au hata cha kikristo nimeshawahi kulisemea tena mara nyingi.Sikuona umuhimu wa kuchangia ile thread na muda niliokuwa nao haukunitosha kurudia tena

Sikubali kwamba chadema ni chama cha kikabila.Siku zote nimekuwa nikipinga ukabila kutumika kwenye majukwaa ya siasa ingawa kuna wanasiasa dhaifu ambao wamekuwa wakitumia hoja hiyo.Is it not shameful that almost every issue gets the tribalism sickness, especially in a political forum which should be for vigorous, honest and progressive conversation? Siku zote nimekuwa msatari wa mbele kupinga ukabila na udini.ubaguzi wa aina yoyote hautakiwi kwenye siasa.

Hapo kwenye Blue,mkuu hebu soma post zangu tuone kama kuna mahali nilikokazania kwamba Rais ajaye awe kijana.Nadhani hapo hatujaelwana mkuu.nilikuwa najadili role ya vijana katika mabadiliko,pamoja na kuwania nyadhifa mbalimbali ikiwamo hata Urais.Pia nina uhakika umeona msimamo wangu kuhusu mgombea Urais ajaye.Sasa sijui hofu ya watu ni nini.

Kuhusu suala la kuongelea mambo mengine,sijaelewa unamaanisha nini.Mimi naona hili ndilo linalonihusu zaidi kwa sababu nahamasisha vijana.Kauli mbiu ya chama changu ninainadi kwa vitendo hapa kwamba vijana ni nguvu ya mabadiliko.Vijana ni taifa la leo.Labda kama kuna cha kujadili hapa na kama tungekuwa wanachadema tu hapa pengine tungepanua mjadala zaidi,tujadili kwamba ni lini vijana wanakuwa nguvu ya mabadiliko na au taifa la leo.

Unapowahamasisha vijana kwa kutumia kauli mbiu hizi ni lazima uwaonyeshe dhamira ya dhati ya kile unachomaanisha.Ndiyo maana kupitia hoja zangu uliona jinsi nilivyokuwa nawahamasisha.Pengine mimi sio muumini mzuri wa demokrasia"nadharia",mimi ni muumini mzuri wa demokrasia "dhahiri"(ya vitendo) na ikishindwa basi ile trait ya uanamapinduzi radical itaibuka.

Ni kweli jukumu la vijana wasomi ni kukisaidia chama ili tulikomboe taifa letu.Na hicho ndicho ninachofanya exactly kuunganisha vijana wote sio hapa tu hata mitaani.vyuoni,restaurants nk.platform zote ni jukwaa la mabadiliko.Tutashinda tu,tufanye kazi ya kuingia kwenye mioyo ya vijana ,nao wataona kweli itakayowaweka huru.Tuanze safari mpya ya uhuru wa pili tulijenge taifa letu.tuna potencials zote za kuwa taifa lenye nguvu Afrika. Youths for change,uchaguzi mkuu bado .tujenge chama kwanza.
 
Hehe, so Kikwete endorses Zitto for president? Kazi kweli kweli, tusubiri mabadiliko ya katiba ili umri wa mgombea Urais ushushwe kutoka miaka 40 ya sasa mpaka 35 kwa kuwa Zitto atakuwa na miaka 39 ifikapo 2015.

This age thing is ridiculous. Age aint nothing but a number. Baadae watasema Rais ajaye asitoke tena Bara, au awe mwanamke (kama gear waliyotumiwa kumng'oa Samuel Sitta kama Spika), au awe Mkristo, au asiwe Mkatoliki, au awe mcheza kiduku.

Kuna vigezo muhimu zaidi vya Rais ajaye --- Asiwe fisadi wala mwenye tuhuma zozote za ufisadi, awe anachukia rushwa kwa vitendo, awe mzalendo, awe anachukizwa na umasikini wa Tanzania, awe mchapa kazi, awe ana uzoefu wa kuwa Rais, awe anaheshimiwa na Watanzania, awe anaaminiwa na Watanzania, awe na vision ya kuleta maendeleo, awe na uchungu wa nchi yake, atoe ahadi kuwa ikifapo 2020 baada ya kipindi chake cha kwanza cha Urais -- mafisadi wote watakuwa jela, umasikini wa nchi utakuwa historia, maradhi na ujinga vitakuwa vimekwisha, na Tanzania itaacha kuwa taifa omba omba.

Huyu ndiyo Rais tunayemtaka na kumhitaji Tanzania, si Rais kijana, mwanamke, Mkristo, au Mzanzibari. Hivi si vigezo kwa kiongozi bora. Ebo?!


Naomba niongeze tena; AWE SIYO TU ANATAKA KUFIKIA JUST DREAM YA KUWA RAIS BALI AWE NA NIA YA DHATI YA KUIFIKISHA NCHI INAPOTAKIWA IFIKE NA AONGOZE KWA MASLAHI YA WATANZANIA
 
Naomba niongeze tena; AWE SIYO TU ANATAKA KUFIKIA JUST DREAM YA KUWA RAIS BALI AWE NA NIA YA DHATI YA KUIFIKISHA NCHI INAPOTAKIWA IFIKE NA AONGOZE KWA MASLAHI YA WATANZANIA
Jk hana uwezo wa kutuamulia rika la urais
 
JK amesema anataka kuridhiwa na rais kijana. Kauli hii inenishangaza na kunichanganya.

Najiuliza maswalii mengi:
Je, JK anatumia nafsi hii kuanza kupiga mawe rafiki yake EL?!, je, anatumia nafasi hii kumnadi Nape au Zito?!.

Hata hivyo ni aibu kuandaa kampeni kwa kisingizio cha rika, alipoingia kwenye kinyanganyiro cha uraisi ilijinadi kwa sifa ya "kijana" lakini ufanisi wake ni hafifu ni bora kama angewaachia nafasi hiyo wazee kama SAS huenda tungepiga hatua.
 
kikwete hana uwezo wa kutuchagulia rais ajaye,kwanza keshatuharibia nchi,angekuwa amefanya kazi ya kukumbukwa angekuwa na uwezo huo,sana sana hapo anataka kuendeleza udini aliouanzisha mwenyewe,ovyo!!!!!
 
Mkuu Gama ingawa tunaelewa ulichomaanisha ila naomba fanya marekebisho ya neno "kuridhiwa".

Majuzi alituambia wanataka Spika mwanamke matokeo yake tuna Spika sawa na mama wa nyumbani asiye na amri kwa wanae anabaki kulalama "Zitto kaa chiniiiiiiiiiii",

Tutamchagua Rais 2015 kutokana na historia yake na uwezo wake wa kiuongozi.
Rais dhaifu na mwoga kwa kisingizio cha "utawala wa sheria" mwisho wake ni 2015.

Hivyo vigezo vya ujana ama jinsia wabaki navyo huko huko kwenye chama chao, wameshatuharibia nchi vya kutosha sasa twasema YATOSHA!
 
atakuwa ni rais wa kwanza Tanzania kumaliza muda wa miaka 10 madarakani as a weak perfomer ever tangu uhuru wa nchi hii. Huyu huyu atuchagulie tena Rais??
 
  • Thanks
Reactions: Sal
Madudu ya Jk yamefanya tusahau madudu ya ben mkapa. Sasa na JK anapenda atayefuata exponent ya madudu iongezeke yaani huyo rais kijana afanye kipeuo cha pili cha madudu aliyofanya JK.

Ndio maana Mkapa hakupenda JK awe mrithi wake. Ni Kingunge alimomalia Mkapa sana kuwa Hayo ni Maagizo ya Mwalimu. Ikabidi mkapa awe mpole.


Mpango mzima ilikuwa JK aendee kuuza sura pale foreign. Basi tu mafisadi na mtandao walimzidi nguvu Mkapa. Ingekuwa TISS inafanya kazi ya taifa wangemsaidia Mkapa kufanikisha mpango wake.
 
JK amesema anataka kuridhiwa na rais kijana. Kauli hii inenishangaza na kunichanganya. Najiuliza maswalii mengi: je, JK anatumia nafsi hii kuanza kupiga mawe rafiki yake EL?!, je, anatumia nafasi hii kumnadi Nape au Zito?!. Hata hivyo ni aibu kuandaa kampeni kwa kisingizio cha rika, alipoingia kwenye kinyanganyiro cha uraisi ilijinadi kwa sifa ya "kijana" lakini ufanisi wake ni hafifu ni bora kama angewaachia nafasi hiyo wazee kama SAS huenda tungepiga hatua.
Mkuu samahahi hapo! Ni kurithi na si kuridhi. Hayo ni maneno yenye maana tofauti.
 
Kuridhiwa - Kukubaliwa

Nadhani ulimaanisha kurithiwa. Anyway, nahisi anajaribu kutupa jiwe gizani lakini anajua mwisho wa siku linawapata wale ambao washaanza harakati za kuutaka urais akiwemo Lowassa, Membe na Sitta. Sitashangaa nikisikia Nape au January Makamba wanasimamishwa kugombea urais.
 
Huyo JK hana uwezo wa kumuweka mtu madalakani ila ni Nguvu ya umma ndio inao huo uwezo wa kumuweka mtu katika hiyo nafasi ya Urais.After all hata yeye alipita tu kimagumashi:fish:
 
Zitto Kabwe, ambaye ameweka wazi kuwa anataka kuwa Rais wa Tanzania anasema kuwa Jakaya Kikwete amemwambia yeye na Mbunge wa NCCR Mageuzi, David Kafulila, kuwa anapendelea Rais wa 2015 awe kijana. Kikwete amewataka Zitto, Kafulila na vijana wengine wajiandae kumrithi.

Source: Post ya Zitto kwenye account ya JF ya kwenye facebook yenyewe hii hapa:

"Msikubali atakayenirithi awe wa rika langu. Kizazi chenu sasa kijiandae"-JK to David Kafulila and I when launching construction of Malagarasi Bridge.

... Hii message inawezekana pia ni ujumbe kwa wazee wote wenye NIA kwamba wao walie tu na waishie. Hususani jamaa yule EL. LOL
 
Anataka kumrizisha rich-one au malaria sugu. ngoja tuone.
 
Kwa kusema hivyo anatengeneza mazingira ya kummpendekeza Hussein Mwinyi kuwa mgombea. Hatutakubali kutawaliwa na mzenji
 
JK anajua kuwa 2015 kwa chama chake kupita ni ndoto, sasa anatafuta wapinzani watakaoweza kumlinda na ambao walio wengi tunawajua. Zitto na mwenzake.
 
Age ain't nothing ni mitizamo na mawazo ya mtu tu, sitaki watanzania kuwa biased na vitu vya kijinga kama vya age. Ndo yale waliyoboronga kuwa tunataka spika mwanamke mnaona yanayotokea bungeni sasa hivi? tutakayeona anatufaaa tu awe kijana well and good na awe mzee yote sawa. Bado namtaka Dr. Slaa sijapata wa kulinganisha naye so far.
 
Back
Top Bottom