Mwenye macho haambiwi tazama, wala mwenye masikio haambiwi sikiatunakoenda watabadili vyama sasa hivi!! samahani kwa kusema hivi ila dalili zote zinaonyesha.
Mwenye macho haambiwi tazama, wala mwenye masikio haambiwi sikiatunakoenda watabadili vyama sasa hivi!! samahani kwa kusema hivi ila dalili zote zinaonyesha.
Mwenye macho haambiwi tazama, wala mwenye masikio haambiwi sikia
---msingi mzima wa hii hoja ni kikwete kusema vijana ndio wanapashwa kurithi kiti cha uraisi, comment zako ziko wazi wewe ni wa upande gani? hayo ya ushahidi mzito ni wewe ndiye unapashwa kutuletea hapa ni nini tatizo la umri katika kugombea urais.
hisitoshe kama wewe ni mwana chadema mzuri kama unavyosema na kama una maslahi binafsi na hii hoja husingeishadadi kiasi hiki.
una post nyingi kiliko mtu yeyote katika hi hoja na unaongea yale yale na kutumia maneno ya kubeza wanaopinga unachosema.
kama husingekuwa mwana siasa wa hovyo hovyo kwa sasa ungetulia na kuacha muda ukifika chama kita hamu, sio kupiga kelele za nani kuwa raisi 2015,
una ajenda ya wazi wala ujajificha huko wazi kabisa kuna Dr slaa sio chaguo lako, unapiga kelele za umri hapa kutimiza malengo hayo.
kila la heri na siasa zako zisizo za hovyo hovyo lakini una majibu ya hovyo hovyo
Thanx mkuu kwa kuona hili, jamaa naandika post zake kijanja sana bt always maandishi hayadanganyi nimeshamwambia hilo japo amekataa but ukweli tunauoa kuwa ana suport hoja ya ujana hapa and the same time zitto amekomalia hili huko facebook hii ni dhahiri hawa wana advantages binafsi na kama sivyo why watumie nguvu kubwa kuelezea hii ishu tena kwa post ndeefu na kila aina ya maelezo?. Ina onyesha wazi wana adantages zao binafsi kuhusu huu mjadala
kuna group facebook tumemwalika zitto tangu mwaka jana na hajawahi kupost chochote kile alikua kama dormant member but juzi katuwekea hiyo ishu ya Jk karema rais ajaye awe kijana.
najiuliza kuna nini nyuma ya hii ishu? Inakuaje asipost kitu kwa mwaka mzima ila juz tu?na kwa nn iwe juu ya urais tu?
Mwenye macho haambiwi tazama
Ben na Nyakarungu Mbona kuna thread kibao tu hapa Jamvini abt cdm na hamchangii?
Mfano hai kuna thread moja inasema ''Mbowe ni tatizo chadema'' na mtoa thread ametoa lawama kuwa cdm chama cha kikabila, Mbowe dictator,fisadi,ana endesha chama kibabe, n.k sasa hapo simuoni Ben wala Nyakarungu wakitoa maoni yao.
Kama thread hii juu ya Urais kijana wanachangia na kuelezea juu ya ishu nzima ya ujana na umuhimu ktk uongozi na wanatoa maoni yao kujenga chama mbona kwenye thread hiyo ya tuhuma ''Mbowe ni tatizo cdm'' siwaoni wakachangia nakutoa maoni kujenga chama?
Kwa kuwa thread juu ya tuhuma za Mbowe chadema zinawapa advantages wao hawachangii wala kutetea chama na kwenye thread wameonekana wapo online wakiangalia mwenyekiti akishushiwa tuhuma huku wakishuhudia kabisa Ben,Zito,Nyakarungu.
Vijana sisi hasa wasomi tunawajibu mkubwa sana kwa maendeleo ya chama chetu but kwa hapa naona hawa wanatumia elimu yao vibaya.
Is just a matter of time watajipambanua tu na wasioona ndipo watakapo ona.
Special thanx to Miss Parliament kwa kuwaeleza ukweli bila kuficha.
Pamoja wanaharakati.
Jamii Forums is descending into anarchy; insults are thrown at people for discussing their ideologies. Hapo kwenye Red,too low.Just be diplomatic and civilized. Tafadhali behave!
Hayo mengine sijui umeyatoa wapi,Nimesharudia several time na unajifanya huelewi au inawezekana kweli hauelewi au hausomi post za wenzako,siungi mtu mkono,huwa naunga mkono hoja na ajenda.CHADEMA haijachagua mgombea Urais sasa sijui nguvu kubwa unayotumia ni ya nini.
Kuhusu mgogoro,kwani hujui migogoro ni muhimu?sasa kama hujui pamoja na maelezo yote tuliyotoa hapo juu basi kazi ni pevu tunahitaji kutenga siku nzima
Kuhusu mabadiliko unadhani ni kubadilisha watu tu.Haya mawazo ndiyo yanatufanya wananchi tuteseke kila siku na wakiona mawazo kama haya kutoka kwa mtu makini(pressumed) basi wanafurahi.we are doing exactly what they want us to do.Tujadili watu,makabila,dini nk.Na siku hizi kuna scramble ya Vijana kuingia mtego wa kusujudia ukabila na udini we even outdo our ancestors and our great grandparents
It's obvious our brutal rulers won't want things to work, 'cause they know if it does our perception will change and will in turn change our political ideaology.
Tanzania system is made to bread low/poverty driven thinkers, that's why someone can prefer to take 2000 Shillings or more to vote their conscience away to the devil; no deeper thought on how decisions made today affect their grand kids in future; and that's why you could apologise to a uniform man/woman that has gone beyond his/her constitutional limit towards you.
The world is moving on the fast lane, but as a nation, Tanzania still taking a nap. By the time we wake up, the rest of the world would have left us behind. We need a change! The nations with whom we began the race for greatness have all gone so far ahead of us that we are unlikely to ever meet up with them
The question still remains however, as to whether we have the political and moral will to respond to these calls and follow through with transformative actions that will lift our nation? Will our leaders do what is necessary to sustain the process?
Will our own prophet emerge to call Tanzania back to conscious life and effective actions, so that the labours of our heroes past will not be in vain?
Miss parliament,Tuache kufikiria ndani ya box na kushusha dhana nzima ya change katika level ya watu. Context ya mabadiliko tuyatakayo Tanzania ni lazima yaonyeshwe kwa dhamira ya dhati na vyama vya siasa ambayo itatoa reflection ya serikali itakayoundwa na zote vision,mission and Ideologies of political partie and that of the nation must be consistent.As a Nation We need changes in all the basic systems of society. The human society stands on a tripod of three systems, namely, the religious system, the political system, and the economic system.
For the society to run effectively each of this system must be made to function well. Where any of the systems is not functioning well, the society will malfunction. Where the three of them malfunction, the society is doomed to imminent collapse unless the right things are done. Our society, regrettably, happened to fall into the category of the societies where the three systems are tottering. If we do not change our direction, we are likely to end up where we are headed.
Sasa nijikite kwenye political system ambayo ndiyo tatizo letu hapa sasa(the engine of decision makers on the political landscape).In this System means the ways and means a given people agree to make decisions about their common life.
Politics, essentially, is the agreed-upon means by which a society orders its life through the making of public and private decisions. This is done through one of several ways a nation can choose to express its political identity such as monarchy, diarchy, democracy etc. We have chosen democracy in , which is that form of political self-expression of a nation that allows people to make decision through their elected representative. For democracy work, the electoral process must be ordered such that the will of the people is sovereign.
So Miss Parliament,Dada yangu we should reason bearing in mind concept ya change ni pana kuliko watu.so dont expect me to discuss/argue katika line hiyo
Froida,
Hujajua tu ? Ni muda mrefu sana.......! Tukaze mwendo watu wa aina hii watachoka tu walikuwepo na watakuwepo.
Nashukuru kwa watu kujadili mustakabali wa nchi yao mara baada ya sera nzuri kufeli kuleta suluhu kutokana na uongozi mbovu wa Rais wetu,.Lakini nakerwa na tabia ya watanzania kutaka kumshambulia zitto juu ya kauli na mtazamo wa kikwete juu ya rais ajaye,pili kuna watu wana imani za kijinga kutaka kumpinga zitto kwa hoja ya kwamba vijana hawaaminiki.,wakiimarisha kauli ya kikwete kutowagawa vijana eti kwasababu vijana ni mtaji wa wanasiasa!
Acheni kuwalimbikiza vijana kuwa mtaaji wa kupigia kura,zaidi waheshimuni mchango wao katika taifa kwa maana ya kwamba ni wazalishaji wakubwa katika Taifa lakini pia ni walinzi wakubwa wa raslimali za Taifa,kwanini muendelee kuwaheshimu kinafiki kama wapiga kura tuu!!kwanini siyo ktk medani za maamuzi makubwa ya kisiasa?? kivipi muwape ubunge,ulinzi kwa maana ya asasi nyeti za kitaifa,kijijini wakiwa nguvu kazi stahiki.Inapokuja nafasi kubwa za maamuzi eti hawaaminiki! kama hawa aminiki hawa ndiyo baado wazee wetu wa kesho,etii vijana hawaaminiki kwa hyo kizazi hiki tarajiwa cha wazee wa kesho hawaji kutoa uongozi mkubwa wa kitaifa kwasababu kama hatukuwaamini vijana kwasasa hatuwezi kuwaamini uzeeni!! kwa maana hiyo mara baada ya sisi kuwa wazee!! ,watoto wetu ktk ujana wao itabidi ndiyo waje kuwa marais wa Taifa hili na historia itawaonesha kwamba Baba na Mama zao hawakuwa waaminifu!!
kwa maana hyo kizazi chetu kitakufa kwa kukiuka baadhi ya nadharia mbalimbali za kwamba EVERY GENERATION HAS GOT ITS OWN MISSION!!!Kwa maana hiyo hiki ni kichekesho cha asubuhi! Itakuwaje kizazi kisichoaminika kikazaa kizazi cha kuaminika!!.Wito wangu kwa watanzania wote wajue kwamba,CHADEMA ni chama chenye katiba yake inayoelekeza nini wajibu wa mwanachama wake,pia hakuna kipengele kinachomkataza kijana ambaye ni mwanachama hai kutoka upande wowote wa Tz kuomba nafasi ya uteuzi ktk medani za uongozi.,wala hakuna mwiko wa mtu kutangaza ama kuto tangaza nia ya kuomba uteuzi..,Mfano mh Dr slaa hakutangaza na watanzania hawakujua ni nani atateuliwa kugombea! lakini CHADEMA kikamteua Dr slaa.,Kumbukeni 2005 tulipo mteua Mh Mbowe,mbona hatukumwekea sheria kwamba ni lazima agombee 2010?
CHADEMA ni ya wanachadema na watanzania wengine wanaolipa kodi kuendesha vyama vya siasa,CHADEMA itaamua nani apeperushe bendera kama ilivyoamua 2005 tukaiamini na chama kikajulikana,mwaka2010 tukaamini na chama kikatanuka.Hivo kila rika kwa kila mwanachama anaye kidhi vigezo vya kikatiba ya CHADEMA na ya Jamhuri anakaribishwa kuwania nafasi za mchakato wa kiuteuzi ndani ya chama.
Nijuavyo mpaka sasa CHADEMA haijamtangaza mgombea urais,kwasababu hakuna uteuzi uliofanyika.Viongozi wetu wote ndani ya chama chetu wameshiriki kikamilifu kujenga na kuimarisha chama,pia watanzania na wanachama kwa namna mbalimbali wamekipa uhalali chama kukubalika,kwa hiyo hapa siyo hoja ya Mbowe,pengine Dr Slaa au Zitto na wengine wengi,angekuwa Mbowe peke yake au Zitto peke yake, Hata Dr peke yake CHAMA hiki kingekuwa kama UDP au TLP.Tuache kupuuza michango ya viongozi ama wanachama ktk kuijenga CHADEMA.Naamini kama michezo hii itaendelea watakao iua CHADEMA siyo CCM ni wanachadema wenyewe kwa kupandikiza roho za kibaguzi kwa kuwagombanisha viongozi wa CHADEMA.
Viongozi wa CHADEMA wote wanajua na wanaheshimu katiba na taratibu za uteuzi wa nafasi za kiuongozi kwa kuheshimu misingi yote ya DEMMOKRASIA ikiwa ni pamoja na uhuru wa kutoa maoni.KARIBU
unasema unamfahamu Ben Nyakarungu,Zitto nina wasiwasi unaweza ukawa Usalama wa Taifa uko kazini kuharibu Vijana wa Chadema unasema unawafahamu wenyewe wanasema hakujui nimeangalia posts zako sidhani wewe ni mmoja wao wewe ni mvurugaji zaidi kwa maoni yangu unawachonganisha vijana na uongozi
Ben,
Nimefurahi sana kwa mawazo uliyotoa ni mazuri na ya kisomi sana.lakini ufike hatua ukubali kubadilisha msimao kutokana na hali ya mazingira.Zitto hawezi kuaminiwa hata ujenge hoja nzito kiasi gani jamani.kuna mtu alishawahi kusema huwa haukubali kushindwa ila kweli nimekubali.acheni upuuzi hizi nguvu zenu,akili na vipaji vyenu kwanini msizielekeze kwenye chama mkisaidie kwenye uenezi?nitatafuta kama kuna post ambayo ulishawahi kujenga hoja nzito kiasi hiki kukitetea chama,mwenyekiti au slaa hapa JF.unakuwa mzuri na kutumia taaluma yako vizuri zaidi kwenye hoja zenye maslahi yenu.hiyo ni tabia mbaya sana kwa wanasiasa mliojijengea uaminifu na chipukizi
kweli Zitto ameanza kubadilika kuwa positive na akiendelea hivi atafaa sana sana kuwa mgombea in future.
ujana sio hoja ya msingi_RIDHIWAN NI KIJANA ILA ANAHARUFU YA KIFISADI so jk anataka kutuambia nini hapa?
Siwalaumu wale ambao wanadhani kauli ya JK haina nia njema kwa upinzani kwa sababu mbili:
1) Kwa muda mrefu sasa, vyama vya upinzani vimehujumiwa sana na chama tawala na taasisi mbali mbali za serikali. Mfano dhahiri ni NCCR Mrema na CUF ya miaka ya 2000. Kila mara, kilipochipua chama imara cha upinzani, hujuma za kila aina zilijitokeza. Hivi leo najiuliza kama CUF iliwafuta wanachama wake wote na kuandikisha wapya maana sisikii tena ikisemwa ni chama cha kidini(kiislamu). Hizi hujuma ndizo zinazowafanya watu wawe defensive, hasa inapotolewa hoja isiyo na mashiko kama ya 'vijana'.
2)Vijana na Uongozi. Hoja kwamba rais ajaye shurti awe kijana si ya msingi. Kama tunataka viongozi wa kutuondoa hapa tulipo na kusonga mbele, hatuwezi kuwa na vigezo kama ujana, jinsi, kabila, dini au kanda. Kiongozi achaguliwe kwa uwezo wake kiutendaji, maono, uadilifu na uzalendo kwa taifa lake.
Zitto anatoa hoja kwamba kwakuwa 72% ya watz ni chini ya miaka 29, basi kiongozi ajaye lazima awe kijana. Hii ni hoja nzuri, lakini sio timilifu. Ztto anatakiwa pia atwambie kwamba zaid ya 80% ya watz wanategemea kilimo kuendesha maisha yao, je kwa mnasaba huo, uchaguzi ujao tuchague mkulima? Hata tukichukua facts za Zitto, huenda tukajikuta kwamba kati ya hao under 29, wanawake(wasichana) ndo wengi; je rais ajaye awe mwanamke? Hapa utaona hoja ya ujana inatumika kwa maslahi binafsi tu!
Ndugu Ben, umezungumzia suala la demokrasia na ushiriki wa vijana. Naomba niziongezee nyama hoja zako kama ifuatavyo. Demokrasia ni kitu kizuri, lakin lazima iende na mila na tamaduni za taasisi husika. Kwetu hapa, demokrasia isiyo na mila na tamaduni inaweza ikauangamiza upinzani ndani ya miezi michache(mfano mzuri ni NCCR ya Mrema). Fikiria kama upinzani wetu una mfumo mzuri wa ku-deal na mapandikizi, watu wanaojiunga kwa lengo moja la kuwasambaratisha. How have you dealt with Shibuda?. Fikiria kwanini chama kikongwe kama CCM, kina-discourage watu wengine wajitokeze kuchukua fomu ya urais na rais aliyepo madarakani? Pamoja na demokrasia kongwe ya reps na demo huko USA, bado kuna mambo ambayo sio debatable kwenye chama husika (e.g. tax, homosexuality etc.)
Kuhusu ushiriki wa vijana, umesema age group ya 35-40 imetengwa. Hapa naona umechanganya mambo ya chama na serikali. Kwenye chama na serikali, umri wa kupiga kura ni 18+yrs. Lakini kuchaguliwa urais ni 40+yrs na 18-35 umoja wa vijana kwenye chama. Ukweli ni kwamba kijana anaweza kushika uongozi wowote wa kiserikali(mwenyekiti wa mtaa,kijiji, katibu kata, diwani, mbunge) akiwa na umri kuanzia 18, isipokuwa kwa urais tu. Kwa mjibu wa katiba ya nchi(sio vyama), age group ya 35-40 haijatengwa, kama kutengwa urais wametengwa wote kuanzia 18-40 na sio 35-40 peke yao.
Mwisho, JK hawezi kutushawishi kwamba ujana tu ndio kiwe kigezo cha kwanza cha kuchagua rais. JK amenukuliwa akisema miaka 3 ya kwanza ya urais wake alikuwa anajifunza maana hakuna sehemu ya kusomea urais. Akaahidi kwamba baada ya miaka hiyo 3, mambo yataenda vizuri maana ameshajifunza. Kwa kauli ya hii, JK alikuwa anatuambia kwamba uzoefu ktk uongozi ni muhimu-tukiwa na rais ana miaka 18, anaweza akatumia miaka yote 5 (kama sio 10) kujifunza kuongoza. Vijana wetu lazima wapate muda wa kuiva kiuongozi, huu umri wa miaka 40 usichukuliwe kama kuwatenga vijana-bali kuwapa nafasi wajifunze kutoka kwa waliotangulia. Kila mwenye kuitakia mema nchi hii, lazima alinde vyama vya upinzani visisambaratike maana vinaiwajibishwa na kuipa ushauri mbadala serikali iliyopo madarakani.
first siamini kama Ben amejikita kumtetea mtu, second inaonyesha zitto si sehem ya chama na hapaswi kutetewa na "watetezi" isipo kua mbowe na slaa tu! kuna kazi kubwa chama chenu...sorry kama sikukuelewa vizuri,i stand to be corrected n i will concur to your inner meaning.
Fringe,
kwani maandishi ya ben unayaonaje?mbona anatumia nguvu na ushawishi kwenye hiyo hoja? huo ndiyo mtandao wao...kwanza naanza kupata mashaka sana.pengine Zitto alikuwa na mkono wake kwa Ben kugombea uenyekiti wa bavicha kabla ya kuenguliwa.Siamini kama Ben alikuwa peke yake kwani yeye alikuwa hajulikani ndani ya chama .alikuwa nje kwa muda mrefu,he was a newcomer lakini ule uwezo alionyesha si wa kawaida ni lazima zitto alikuwa nyuma yake tu.
Haiwezekani mtu atumie fedha nyingi kiasi kile na kujenga mitandao ghafla hadi kushika vyombo vya habari na baadae ifuate fununu kwamba anataka kujiengua.kuna ajenda hapa