Kikwete: Nataka kurithiwa na rais kijana!

Kikwete: Nataka kurithiwa na rais kijana!

DOUBLE AGENT

Member
Joined
Jul 3, 2011
Posts
38
Reaction score
34
Zitto Kabwe, ambaye ameweka wazi kuwa anataka kuwa Rais wa Tanzania anasema kuwa Jakaya Kikwete amemwambia yeye na Mbunge wa NCCR Mageuzi, David Kafulila, kuwa anapendelea Rais wa 2015 awe kijana. Kikwete amewataka Zitto, Kafulila na vijana wengine wajiandae kumrithi.

Source: Post ya Zitto kwenye account ya JF ya kwenye facebook yenyewe hii hapa:

"Msikubali atakayenirithi awe wa rika langu. Kizazi chenu sasa kijiandae"-JK to David Kafulila and I when launching construction of Malagarasi Bridge.
 
Rais Kikwete hajakosea,na pia jukumu la kuchagua viongozi au jukumu la kujua ni kiongozi gani anahitajika linabaki kwa wapiga kura.Suala pia si la kijana tu,kijana mwenye uwezo ili tusijetukaburuzwa na ride ya ujana au jinsia tu kama ilivyokuwa 2005,people voted for "beauty" not for "Duty",ha ha ha! loh

Ila sasa anaposema msikubali anamaanisha nini?inaonekana sasa yeye atatumia udikteta ndani ya chama chake kukataza mtu asigombee? Kwenye hoja ya ujana hajakosea,ni wazo zuri

It will be unfair to deny /ask somebody not to contest and will be infringing on his constitutional right. It is a right given to him by the Constitution which he has a sole discretion to exercise.
Tanzanians at this stage should be talking of credible elections and free participation. Credible people should be allowed to participate in the election

Again,It would be unfair for anyone to ask anymember of a political party not to run for presidency on the basis of an unconstitutional arrangement by a political party.
 
Hehe, so Kikwete endorses Zitto for president? Kazi kweli kweli, tusubiri mabadiliko ya katiba ili umri wa mgombea Urais ushushwe kutoka miaka 40 ya sasa mpaka 35 kwa kuwa Zitto atakuwa na miaka 39 ifikapo 2015.

This age thing is ridiculous. Age aint nothing but a number. Baadae watasema Rais ajaye asitoke tena Bara, au awe mwanamke (kama gear waliyotumiwa kumng'oa Samuel Sitta kama Spika), au awe Mkristo, au asiwe Mkatoliki, au awe mcheza kiduku.

Kuna vigezo muhimu zaidi vya Rais ajaye --- Asiwe fisadi wala mwenye tuhuma zozote za ufisadi, awe anachukia rushwa kwa vitendo, awe mzalendo, awe anachukizwa na umasikini wa Tanzania, awe mchapa kazi, awe ana uzoefu wa kuwa Rais, awe anaheshimiwa na Watanzania, awe anaaminiwa na Watanzania, awe na vision ya kuleta maendeleo, awe na uchungu wa nchi yake, atoe ahadi kuwa ikifapo 2020 baada ya kipindi chake cha kwanza cha Urais -- mafisadi wote watakuwa jela, umasikini wa nchi utakuwa historia, maradhi na ujinga vitakuwa vimekwisha, na Tanzania itaacha kuwa taifa omba omba.

Huyu ndiyo Rais tunayemtaka na kumhitaji Tanzania, si Rais kijana, mwanamke, Mkristo, au Mzanzibari. Hivi si vigezo kwa kiongozi bora. Ebo?!
 
Zitto akiendelea kubadilika kifikra kama sasa atafaa kugombea!
 
Zitto akiendelea kubadilika kifikra kama sasa atafaa kugombea!
kweli Zitto ameanza kubadilika kuwa positive na akiendelea hivi atafaa sana sana kuwa mgombea in future.

ujana sio hoja ya msingi_RIDHIWAN NI KIJANA ILA ANAHARUFU YA KIFISADI so jk anataka kutuambia nini hapa?
 
Ili mradi hii thread isiwe na shari tu sasa.....
Tusiowasahaulifu na tunaojua kuunganisha dot tunajua what is going on! Majaliwa yakitokea yakutokea tutawaonesha nini tulimaanisha,sasa hv hatueleweki kwa wengi! Mambo yanaenda taratibu na kwa hatua! werevu kimyaaa kwanza!
 
Mhm, just wondering kwa hiyo wenye umri wa kina E.L ndo hawatakiwi kabisa? Huyu mtu ni bingwa wa kufunga milango aliyopitia!

Ha ha hahaha,kama ina tija kwa taifa na ikiwa busara za kiongozi huwa zinatiririka akiwa anaelekea ukingoni au baada ya kutoka madarakani.........

Anyway,Kauli mbiu ya maadhimisho ya uhuru ni ya kuwaandaa watu kubweteka...iwe hivi Tumejaribu,tujisahihishe na tusonge mbele kwa ujasiri baadala ya tume...,tumeweza ,tusonge mbele. anyway,nimechombeza tu.tueendelee na mjadala....

Pengine JK alitoa ushauri tu,ni ushauri mzuri ikiwa vigezo zaidi ya hicho vikizingatiwa na pia mchakato wa kidemokrasia ukaamua.kukiwa na wagombea wenye sifa zinazolingana lakini wakatofautiana kwa umri tu,hata mimi nitampa first priority kijana kwa hali ya taifa hili ilivyo sasa....
 
Kwa hivi hapo alipo kichwani mwake kwishiney sababu ya umri!!! Uzee dawa kumbe yeye uzee ugonjwa!!
 
Mhmm, Ngoja kwanza nitafute umri wa Mwinyi maana labda ana mlenga huyo?! CCM nani kijana anataka kugombe? Lakini nakumbuka moja ya agenda kubwa waliyotumia wanamtandao ni kurubuni watu kuwa Kikwete ni Kijana?!
 
wanavutiwa CCM hao, mtasikia wamehama. hapo mzee mwenyewe amewapa live, UNATAKA CHEO BASI HAMIA CCM.
 
Tanzani kuna vijana wengi wenye uwezo wa kuongoza nchi, lakini kigezo kisiwe ujana pekee na nadhani na uzalendo na utaifa ni mambo ya msingi
 
Baada ya madudu yote aliyoyafanya Kikwete, nikiwa kama mpiga kura nitakuwa na wasiwasi na choice yake ya rais ajaye.
 
kwa hio Dr slaa mzee wa kukurupuka akae pembeni kule chadema na kumuachia kijana Zitto
 
Zitto Kabwe, ambaye ameweka wazi kuwa anataka kuwa Rais wa Tanzania anasema kuwa Jakaya Kikwete amemwambia yeye na Mbunge wa NCCR Mageuzi, David Kafulila, kuwa anapendelea Rais wa 2015 awe kijana. Kikwete amewataka Zitto, Kafulila na vijana wengine wajiandae kumrithi.

Source: Post ya Zitto kwenye account ya JF ya kwenye facebook yenyewe hii hapa:

"Msikubali atakayenirithi awe wa rika langu. Kizazi chenu sasa kijiandae"-JK to David Kafulila and I when launching construction of Malagarasi Bridge.


No thank you,Kama issue zenyewe ndio hizo leo wewe chungwa kesho limao,no sasa hivi wabongo wako kivingine,haijalishi wewe kijana au mzee,cha msingi this time watu wanamind mchapa kazi,watu kipindi klichopita waliconsider factor hizo za ujana,and then what next.......

Kama vijana ndio hao leo anaongea hivi kesho akiwekwa sawa na wasure akikamata fuba lake anawageuka wabunge thubutu.Ilo this time halipo watu wako full data,Ili uwe Prezidar kweli wa TAIFA hili uko mbele ya safari you need to be CLEAN REAL CREAN,sio uchukulie umepiga deal UK or GMNY ufikilie watu hawataikamata nyeti.Watu wanadaka wanakusubilia kwenye KIU.Watu eeeeeh watu waaaa.

Usafi Usafi ndio jibu la kuwania upresidar wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom