WaTz na waafrika kwa ujumla tuna tatizo la kutoona au kukubali ukweli. Tatizo la Aids lilipoanza kwa kasi nchi za magharibi na Marekani wenzetu walianzisha kampeni kabambe ya kuwaelimisha jamii zao pamoja na namna za kujikinga. Hii ikiwa ni pamoja na kugawa condoms na kuelezea namna ukimwi unavyoambukiza kwa jinsi wanavyoelewa and it paid off!
Hapa kwetu hatukuwa wawazi promotion ya matumizi ya condoms ilikuwa chini na vilevile tunafumbia macho ukweli wa kuwa vijana wetu wake kwa waume wanashiriki ngono kuanzia umri mdogo. Hivyo basi tulitakiwa tuanzishe elimu ya ngono mashuleni wanafunzi waelewe miili yao na namna ya kujikinga, hiyo hatuna tunategemea nini?
Viongozi wazembe na kuropoka kwao kama hivi alivyofanya JK ni sawa na Mbeki alivyodai kuwa HIV haisababishi Aids na watu wanasikia viongozi wakiongea utumbo kama hivi na kuamini, matokeo watu wanaendelea kutongoza watoto wa shule na kuwapa mimba na aids!
Bila kuwa na elimu ya ngono mashuleni ni bure, vilevile bila kuwa na access kwa afya za jamii pamoja na uzazi wa mpango na kugawa pills za kuzuia mimba itakuwa kazi bure. Ukweli ni kuwa wasichana wakivunja ungo wanakuwa na nyege hiyo ni asili ya mwili wa binadamu sawa na wavulana wakipata balehe, bila kufundishwa namna ya kudhibiti matamanio yao itakuwa kazi bure kuwakemea wakishapata mimba au ukimwi ilhali ukuwapa elimu nasaha kabla!
Zamani kwenye jamii zetu asilia tulikuwa na jando kwa vijana wa kiume na unyago kwa wa kike, huko walifundishwa namna mbalimbali za kujiweka safi pamoja na jinsi miili yao invyofanya kazi siku hizi hiyo hamna, tunaacha mila zetu zenye manufaa bila kuangalia athari zake na kufuata mambo ya kimagharibi blindly bila kuchanganua athari zake. Wazazi wanaogopa kuwaweka chini watoto wao na kuwapa elimu ya ngono, shuleni hilo somo halipo kwa shinikizo la makanisa na mashekhe, sasa unategemea nini kama sio wimbi la mimba na ukimwi hapo?