Kikwete: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

Mmmmh, haya makubwa jamani. Kweli Rais wa nchi anaona watu wanaopata Ukimwi au mimba ni vihelehele vyao . Kweli hii inasikitisha ....
ukimchunguza kwa makini utagundua kuwa hayupo kabisaaa,
anahitaji kukombolewa huyu, he is in mental illness, si bure
 
Personal responsibility gani kwa watoto walio chini ya miaka kumi na nane? Hivi kwa nini, nchi zilizoendelea zina sheria kali sana kwa watu wanaotaka kumess up na watoto walio katika hiyo age group?

Basi utaona ni tatizo la jamii nzima na si la mtu mmoja kutoa mwongozo. Viongozi wa kidini wako wapi? Wanaharakati wa kutetea haki za watoto wako wapi? Wabunge wako wapi? Wewe mwenyewe umefanya nini kuhakikisha statutory rape laws ni kali na zinatekelezeka na kutekelezwa?
 
Code:
Code:

Chaguo la Mungu hilo...........

Unajua wewe hilo jina ulilochagua, avatar yako na comment yako vimenifanya nicheke karibia nimwage maji kwenye hii keyboard!!! halafu na mwakitakotako na ile avatar, na kusema mungu ana bifu na taifa letu ndio kabisaaaaaa.... kweli JF ni mwisho wa mambo!!!
 
Mimi nisingependa mwanangu apewe mwongozo na raisi. Nitampa mwongozo mimi mwenyewe. Wazazi wengine pia ni wajibu wao kuwalea na kuwafundisha maadili mema watoto wao. Sio wajibu wa raisi huo unless uniambie imewekwa bayana hivyo kwenye job description yake.

kama ndio hivyo basi sio kazi yake pia kuwaita watoto wa watu viherehere.

mie ningependa mtu yoyote yule amkumbushe/amuelimishe/kumuongoza mtoto wangu pale anapofanya kosa hata kama mimi nishamwambia kabla.
 
hii kauli ya rais ni kihoja kwangu kwa mwaka 2010,sikutegemea kabisa hili tamko,
huyu mtoto wa pwani kweli mdundiko ni asili yake,afu watu wanampigia makofi!!
ivi anajua rate ya UKIMWI kanda ya ziwa na elimu ilivo duni???
ivi anawajua wale "wauza mboga" visiwani,ngoma za wasukuma nk?
huyu jamaa wa kumuombea sana Mola amuokoe na hili tatizo la "mdomo wake"
 
Basi utaona ni tatizo la jamii nzima na si la mtu mmoja kutoa mwongozo. Viongozi wa kidini wako wapi? Wanaharakati wa kutetea haki za watoto wako wapi? Wabunge wako wapi? Wewe mwenyewe umefanya nini kuhakikisha statutory rape laws ni kali?

Wewe si umesema Rais ana hoja. Na ukaendelea kusema ya ukauliza what happened to personal responsibility? ...Lakini hata hivyo Rais ameliangalia hili tatizo superficially sana na mbaya zaidi amegeneralize mambo. Na kauli kama hizi ni mbaya sana kwani sasa watoto wote watakaopata mimba wataonekana ya kuwa ni vihelehele vyo ndio vilivyopelekea wao kufika hapo walipo na zitapelekea hata kukosa msaada.
 
Kudanganywa ndio kiherehere anachokizungumzia raisi. Kubakwa ni jambo jingine kabisa. Lakini nikupe peremende halafu nikumege...hapana hicho ni kiherehere chako tu.
tofautisha kudanganywa kwa mtu mzima na underage mfano mtoto wa miaka 10 au 12 akidanganywa bado utasema ni kiherehere chake fikiria na uwezo wake wa kujua baya na zuri.
 
Wewe si umesema Rais ana hoja. Na ukaendelea kusema ya ukauliza what happened to personal responsibility? ...Lakini hata hivyo Rais ameliangalia hili tatizo superficially sana na mbaya zaidi amegeneralize mambo. Na kauli kama hizi ni mbaya sana kwani sasa watoto wote watakaopata mimba wataonekana ya kuwa ni vihelehele vyo ndio vilivyopelekea wao kufika hapo walipo na zitapelekea hata kukosa msaada.

Raisi told it like it is sema nyie tu mmesha condition akili zenu ktk kupinga kila kitu atakachosema hata kiwe kweli namna gani.
 
azaaye mpumbavu ni kwa huzuni yake mwenyewe; Wala baba wa mpumbavu hana furaha.
......sisi ndiyo tulomchagua huyu bwana japo si wote, furaha tutoe wapi na ufirauni wake?....
 
tofautisha kudanganywa kwa mtu mzima na underage mfano mtoto wa miaka 10 au 12 akidanganywa bado utasema ni kiherehere chake fikiria na uwezo wake wa kujua baya na zuri.

Ndio maana nikasema wazazi wana wajibu mkubwa sana ktk kuwafundisha mazuri na mabaya watoto wao. Mimi wa kwangu namfundisha kutokuchukua kitu chochote kutoka kwa mtu asiyemfahamu.
 
Hii ni moja kati statement mbaya iliyowahi kutolewa na kikwete. Mbaya zaidi, kauli hii inaweza kupelekea kikundi fulani cha watu kubaguliwa na kikundi kingine. Ni lazima State House wafanye damage control ........
 
sasa kupata mimba na ukimwi sio kihelehele ni nini sasa? unajua sie tunapenda maneno ya kupakana mafuta. Yeah kuna wachache sana wanaopata hizo vitu kwa ajali lakini 99.9999% ni vihelehele
 
"Suala la ubakaji katika wilaya ya Karagwe iliyopo mkoa wa Kagera bado lipo juu hivyo kutishia maendeleo ya elimu kwa mtoto wa kike. Takwimu zinaonyesha kuwa watoto zaidi ya 54 walibakwa katika kipindi cha mwaka 2009, takwimu hizo kwa mujibu wa wakazi wa karagwe wanadai ni ndogo sana ukilinganisha na idadi halisi ya kesi zinazotokea hasa vijijini. Mbali na ubakaji, wanafunzi kupewa mimba na wengine kuolewa kwa mwaka 2009 pekee walifikia 44 Karagwe ikiwa wilaya ya pili kwa ukubwa wa tatizo hilo ikitanguliwa na wilaya ya Chato yenye wanafunzi 74 waliopata mimba kwa kipindi hicho hicho...Mbaraka Ismaili mkazi wa kijiji cha Kagenyi wilayani Karagwe ambaye mtoto wake wa miaka 14 Fatuma Mbaraka alibakwa na mzee wa miaka 54 Ali Migeyo mwishoni mwa mwaka jana anasema kesi nyingi za kubakwa watoto zinafichwa na kuzimaliza kimila bila kufikishwa mbele ya sheria...Raisi Jakaya Mrisho kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wamekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za mtoto wa kike kielimu nchini kote huku raisi akiwataka wakuu wote wa wilaya na mikoa kuhakikisha wanakomesha tabia hizi za mimba kwa watoto wa kike..." - MAISHA NA MAFANIKIO: Ubakaji unavyodidimiza elimu Karagwe
 
Code:
Code:

Ina maana mwandishi wake wa hotuba Januari Yusuph Rajab Makamba huwa anachomekea viutani kwenye hotuba za bosi wake au Muungwana ana asili ya kutania tania hadi awe anatania hata kwa ishu ya kulia?

nini hiki???
mwandishi wake?
 
Ndio maana nikasema wazazi wana wajibu mkubwa sana ktk kuwafundisha mazuri na mabaya watoto wao. Mimi wa kwangu namfundisha kutokuchukua kitu chochote kutoka kwa mtu asiyemfahamu.

Tafiti zinaonesha kuwa watu anaowafahamu ndio hatari. Ubakaji mwingi unafanywa na mafataki ambao vibinti vinawafahamu - maankali, mabinamu na hata maboifurendi! Kikulacho...

Mkinge umpendaye na Fataki!
 
sasa kupata mimba na ukimwi sio kihelehele ni nini sasa? unajua sie tunapenda maneno ya kupakana mafuta. Yeah kuna wachache sana wanaopata hizo vitu kwa ajali lakini 99.9999% ni vihelehele

People here are pathetic! They like to be babied all the time. Shoot sometimes you gotta tell it like it is...
 
Back
Top Bottom