Kikwete: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,617
NA MWANDISHI WETU
7th June 2010


Rais Jakaya Kikwete amesema matukio ya mimba kwa wanafunzi wa kike nchini yanasababishwa na viherehere vya wanafunzi wenyewe.

Aidha, Rais Kikwete amekiri kwamba matukio ya mauaji ya vikongwe pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), yanalidhalilisha taifa.

Rais Kikwete alitoa kauli hizo katika kijiji cha Kisesa wilayani Magu jana wakati akihutubia wananchi kwenye ufunguzi wa mashindano ya ngoma kwa kabila la Wasukuma; ngoma ambazo zinajulikana kama 'Bulabo'.

" Kila anayepata Ukimwi anaufuata mwenyewe na wengine ni viherehere vyao; kwa mfano watoto wa shule," alisema Rais Kikwete wakati akijibu risala ya Mkurugenzi wa Makumbusho ya Bujola, Fadha Frasince Sandhu, ambaye alisema ujumbe wa mashindano hayo mwaka huu ni vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, suala la zinaa kwa bianadamu, siyo la lazima hivyo binadamu anaweza kujizuia ama kujikinga kwa kutumia kondomu.

" Na kwa bahati mbaya shughuli ile (uzinzi) binadamu hana dharura nayo, hivyo unaweza kutumia kondomu kama unaona kwamba huwezi kutii amri ya sita ama huwezi kuwa mwaminifu katika ndoa yako," alisema kauli ambayo ilizua vicheko miongoni mwa watu waliohudhuria ufunguzi huo. Aliwashauri wananchi watakaoshiriki kwenye mashindano hayo wawe na tahadhari dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.

" ...katika mambo yanayolitia aibu taifa hasa kwa watani wangu Wasukuma, ni pamoja na mauaji ya albino na vikongwe eti tu kwa sababu wana macho mekundu. Ni mambo ya fedheha sana ingawa yanakwenda yanapungua lakini yanalidhalilisha taifa," alisema.

Aliwataka washiriki wa mashindano hayo walisaidie taifa katika kupiga vita mauaji ya aina hiyo.

Rais Kikwete alifuatana na wabunge kadhaa akiwemo Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (CCM) pamoja na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM).

Aidha, Rais Kikwete amepewa jina la Mungubabu, ikiwa na maana busara na uwezo wa kuongoza nchi kama Mungu.

Mashindano ya 'bulabo' yalianza mwaka 1954 kupitia Kanisa Katoliki Bujola, lengo likiwa ni kuweka burudani mara baada ya mavuno.


CHANZO: NIPASHE
 
Mmmmh, haya makubwa jamani. Kweli Rais wa nchi anaona watu wanaopata Ukimwi au mimba ni vihelehele vyao . Kweli hii inasikitisha ....
 
Kwa hiyo wote waliopata ukimwi ni via sexual intercourse, vipi wale waliozaliwa nao au waliopata through blood transfusion ? Na jee Rais anasend message gani kwa wale wanaowarubuni watoto wa shule ambao ni below 18? Jee hao watoto wa kike are they matured enough to make aninformed decisions...those are the questions that our president was supposed to ponder before blaming students and AIDS patients
 
NA MWANDISHI WETU
7th June 2010



" Kila anayepata Ukimwi anaufuata mwenyewe na wengine ni viherehere vyao; kwa mfano watoto wa shule,"


CHANZO:
NIPASHE

Inabidi aangalie kauli anazotoa, hii si kauli nzuri hata kidogo, vipo vitu vingi vinavyosabisha watu kupata ukimwi na wakati mwingine siyo kwa kujitakia au kuwa wazembe, huu ni unyanyapaa kwa mtu aliyekuja na kauli ya Tanzania bila ukimwi inawezekana....inasikitisha sana.
 
Lakini ana hoja hapo....
ukitazama haraka haraka yap lakini kwa undani yeye kama kiongozi ni kama mzazi pia.


sasa mkuu nyani ngabu majukumu ya mzazi au kiongozi ni kutoa muongozo sio kusema kumwambia mwanao kiherehere chake.swala la ngono lina ushawishi mkubwa sana na ni rahisi mno binadamu yoyote kuingia mkenge si mkubwa wala mtoto.

Kuna maneno mengi ya busara na ya kuelimisha ambayo Kikwete angetumia yangeweza kuwa msaada kwa hawa wanafunzi kuliko kuwaambia kiherehere na wazazi pia tunahitajika kuwaongoza watoto wetu vizuri na kuwaelimisha swala zima la ngono na sio kuwalaumu tu.


anyway ni simlaumu sana kwani kashatoa kauli nyingi za ajabu ajabu nadhani ni kwa vile uwezo wake wa kuongoza ni mdogo sana.
 
Kama hakuyatoa yeye si ungesikia Nipashe linafungiwa? - lakini alikuwa anatania tuuu
Very true mkuu... inasikitisha kwamba ameweka wote under one cluster wakati majority ni victims wa abuse, tena from people around them waliotakiwa wawalinde hawa wadogo zetu!!!

Siamini kabisa hii itapita kama kauli nyingine kwani tuna wanaharakati kwa gender wazuri sana, LAKINI SI UNAJUA TENA RAIS WETU KWA UTANI?? WE SUBIRI AJE TENDWA HAPA ATASEMA RAIS ALIKUA ANATANIA
 
Anaitwa Mungubabu tena? Acheni huo utani, hekima na busara hizo wanazijua wasukuma tu? Tuna kazi kwelikweli kuelimisha huu umma wa watanzania wanaopenda kusujudia watu na kuwapamba kwa sifa ambazo hawana..sijui tuna tatizo gani?
 
Waandishi waweke wazi kama ni kweli alisema "Kila anayepata ukimwi" ni kihere here....Unless alikuwa akizungumzia baadhi ya wanaopata ukimwi na si "Kila" anayepata ukimwi,kuna utofauti kwasababu si kweli "Kila" anayeupata ukimwi anaupata kwa njia ya zinaa.
 
Kwa hiyo wote waliopata ukimwi ni via sexual intercourse, vipi wale waliozaliwa nao au waliopata through blood transfusion ? Na jee Rais anasend message gani kwa wale wanaowarubuni watoto wa shule ambao ni below 18? Jee hao watoto wa kike are they matured enough to make aninformed decisions...those are the questions that our president was supposed to ponder before blaming students and AIDS patients

Mkuu, nadhani mkulu amekosa elimu ya ukimwi, jamii na makuzi hasa kwa ajili ya public speaking!!! kuna kauli ambazo ni za kuturudisha nyuma hasa kwenye fight against HIV/AIDS, TB na malaria... his statement ni confimration kwamba hajaiva kwenye vita dhidi ya stigma!!!

Pia tukumbuke kwamba kuna watoto wanzaliwa na virusi kutoka kwa mama, na wapo wengi sana under 18 siku hizi kwani hawakua wakibahatika kupimwa kwani huduma za PMTCT [prevention of mother to child transmission] hazikua active na wazungu walikua hawajaleta pesa
 
tuache utani wakuu haya maneno kayatoa raisi?
aaah mie sishangai kwani tz kuna raisi ama mropokaji tu, with no sence in how he is talking about.

mazungumzo ya mtu yanamtambulisha ana hekima ya kiasi gani, vipi kwa wanao bakwa na kupata ujauzito?
 
Wasichana wanaopata mimba ni viherehere vyao...

Hawa wanaopata mimba siyo wote wana viherehere, wengine ni ugumu wa maisha, utoto, na njaa kali...kunawengine huwa wanavamiwa kijinsia kwa nguvu na ndugu zao wa karibu baba/uncle etc.

Naukiangalia kwa macho mawili nani angesaidia kusaidia ugumu wa maisha na njaa kali kama siyo mtuhumu.
 
Back
Top Bottom