Kikwete: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

Kikwete: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

nini hiki???
mwandishi wake?
ole wao waandishi na mafarisayo, wanaocheka wakati wa kulia,
nasema tena Ole wao, wanaoleta furaha sehemu yenye huzuni, waletao mzaha sehemu ya
kusikitika, ole tena ole
 
Tafiti zinaonesha kuwa watu anaowafahamu ndio hatari. Ubakaji mwingi unafanywa na mafataki ambao vibinti vinawafahamu - maankali, mabinamu na hata maboifurendi! Kikulacho...

Mkinge umpendaye na Fataki!

Ubakaji ni hoja nyingine kabisa. Ubakaji ni kosa na wabakaji inatakiwa wapewe adhabu kali sana. Ingekuwa juu yangu mimi wabakaji wote wangekuwa castrated. Hakuna msamaha.
 
Raisi told it like it is sema nyie tu mmesha condition akili zenu ktk kupinga kila kitu atakachosema hata kiwe kweli namna gani.

Na wewe umeikondisheni akili yako kumtetea by any means necessary.
 
Ubakaji ni hoja nyingine kabisa. Ubakaji ni kosa na wabakaji inatakiwa wapewe adhabu kali sana. Ingekuwa juu yangu mimi wabakaji wote wangekuwa castrated. Hakuna msamaha.

Na urubuni/kurubuni je?
 
Na wewe umeikondisheni akili yako kumtetea by any means necessary.

You got that wrong...how many times have I bashed him before? I only defend him when I feel he's being unfairly attacked and bash where I feel he's wrong. I just don't bash, bash, and more bash just because....
 
Hapo sasa ndipo wazazi wanapoingia. Kabula hapa huwezi kumdanganya kitu wewe. I double dare you to try....atakushushua mzee mzima

Saizi yake ni Ankali Zakumi!

God forbid, but, frankly, you feel it when it hit home!
 
Halafu umeona ile special dedication to you? Hayo mayoutube unayotumia kumfundishia Kabula nayo ni hatari. Don't wait until the chicke come home to roost!
 
Halafu umeona ile special dedication to you? Hayo mayoutube unayotumia kumfundishia Kabula nayo ni hatari. Don't wait until the chicke come home to roost!

Where is this special dedication to me at? And from whom?
 
Ndio maana nikasema wazazi wana wajibu mkubwa sana ktk kuwafundisha mazuri na mabaya watoto wao. Mimi wa kwangu namfundisha kutokuchukua kitu chochote kutoka kwa mtu asiyemfahamu.

ndio maana tukasema kwamba yeye pia mzazi na sidhani kama mzazi anatakiwa kuzungumza vile kama ana akili zake timamu.


jinsi alivyoitoa kama wauni tu mtaani wanavyochukulia watoto wakike wana viherehere.kama anataka kujifananisha na hawa wauni wa mtaani basi sawa.
 
One day Mungu atatujalia raisi ambaye hatanii mambo sensitive kama haya...
 
Mimi nisingependa mwanangu apewe mwongozo na raisi. Nitampa mwongozo mimi mwenyewe. Wazazi wengine pia ni wajibu wao kuwalea na kuwafundisha maadili mema watoto wao. Sio wajibu wa raisi huo unless uniambie imewekwa bayana hivyo kwenye job description yake.

hivi mkuu hujui kwamba kuna watoto ambao yatima hawana wazazi na wanategemea muongozo kutoka kwa wakubwa wengine? sasa maneno haya ya raisi yamewasaidia nini mtoto ambaye yatima kama kweli unasema jukumu ni la mzazi peke yake?
 
in short ni kwamba the statement was uncalled for!!! hata kama wapo waliozaliwa na hyper-sexual behavior
 
Duh mkulu kachemsha ile mbaya.. hiyo kauli ni ya hatari haswa kwa waathirika. Huwezi kusema kila wenye ukimwi wamefwata wenyewe.. hata waliozaliwa nao?? hilo si sawa!!! Na wasichana wapatao mimba si wote ni kiherehere... Amegeneralize mno na hii itamcost mahali flani na wakati flani!!!
 
Rais Jakaya Kikwete amesema matukio ya mimba kwa wanafunzi wa kike nchini yanasababishwa na viherehere vya wanafunzi wenyewe.
Aidha, Rais Kikwete amekiri kwamba matukio ya mauaji ya vikongwe pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), yanalidhalilisha taifa.
Rais Kikwete alitoa kauli hizo katika kijiji cha Kisesa wilayani Magu jana wakati akihutubia wananchi kwenye ufunguzi wa mashindano ya ngoma kwa kabila la Wasukuma; ngoma ambazo zinajulikana kama 'Bulabo'.
" Kila anayepata Ukimwi anaufuata mwenyewe na wengine ni viherehere vyao; kwa mfano watoto wa shule," alisema Rais Kikwete wakati akijibu risala ya Mkurugenzi wa Makumbusho ya Bujola, Fadha Frasince Sandhu, ambaye alisema ujumbe wa mashindano hayo mwaka huu ni vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, suala la zinaa kwa bianadamu, siyo la lazima hivyo binadamu anaweza kujizuia ama kujikinga kwa kutumia kondomu.
" Na kwa bahati mbaya shughuli ile (uzinzi) binadamu hana dharura nayo, hivyo unaweza kutumia kondomu kama unaona kwamba huwezi kutii amri ya sita ama huwezi kuwa mwaminifu katika ndoa yako," alisema kauli ambayo ilizua vicheko miongoni mwa watu waliohudhuria ufunguzi huo. Aliwashauri wananchi watakaoshiriki kwenye mashindano hayo wawe na tahadhari dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
" ...katika mambo yanayolitia aibu taifa hasa kwa watani wangu Wasukuma, ni pamoja na mauaji ya albino na vikongwe eti tu kwa sababu wana macho mekundu. Ni mambo ya fedheha sana ingawa yanakwenda yanapungua lakini yanalidhalilisha taifa," alisema.
Aliwataka washiriki wa mashindano hayo walisaidie taifa katika kupiga vita mauaji ya aina hiyo.
Rais Kikwete alifuatana na wabunge kadhaa akiwemo Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (CCM) pamoja na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM).
Aidha, Rais Kikwete amepewa jina la Mungubabu, ikiwa na maana busara na uwezo wa kuongoza nchi kama Mungu.
Mashindano ya 'bulabo' yalianza mwaka 1954 kupitia Kanisa Katoliki Bujola, lengo likiwa ni kuweka burudani mara baada ya mavuno.
CHANZO: NIPASHE
 
One day Mungu atatujalia raisi ambaye hatanii mambo sensitive kama haya...

Hili la ngono naamini hata Mungu hawezi litolea maneno ya kubembeleza, nafikiri yeye Mungu atasema yeyote anaye fanya ngono atapambana na adhabu kali ya moto.

Sasa mie sipati picha watoto kati ya miaka 13 na 18 sijui Mungu atawasamehe kwa sababu wa me danganywa ? sipati picha.

Lakini mimi nafikiri huo umri ni wa kibinadamu kuita watoto. nafikiri Mungu anasema hivi Mtu yeyote aliye BALEHE na mwenye uwezo wa kuzaa sio mtoto ni mtu mzima. Huu umri tuliojiwekea ni sisi wanadamu tu.
 
NA MWANDISHI WETU
7th June 2010


" Kila anayepata Ukimwi anaufuata mwenyewe na wengine ni viherehere vyao; kwa mfano watoto wa shule," alisema Rais Kikwete wakati.

CHANZO: NIPASHE


Duh! Another Kikwete's gaffe!!! Mwambie maneno hayo aliyekamatwa kwa nguvu na kubakwa kisha kuambukizwa ukimwi kwamba kilikuwa ni kiherehere chake tu, mwambie mtu aliyepata ukimwi kupitia blood transfusion kwamba kilikuwa ni kiherehere chake tu! mwambie mtoto aliyezaliwa na mama aliyeathirika kwamba kilikuwa ni kiherehere chake tu, mwambie mke/gf ambaye mumewe/bf alitembea nje na kumletea ukimwi kwamba kilikuwa ni kiherehere chake tu! Naona huyu bwana ni mmoja ambao bado wanaamini kwamba ukimwi unatokana na tendo la ndoa tu na kila muathirika yeye ndiye wa kulaumiwa kwa kiherehere chake!!! Halafu tunataka kumpa miaka mingine mitano ya kuongoza nchi!
 
na mwandishi wetu
7th june 2010

rais jakaya kikwete amesema matukio ya mimba kwa wanafunzi wa kike nchini yanasababishwa na viherehere vya wanafunzi wenyewe.

aidha, rais kikwete amekiri kwamba matukio ya mauaji ya vikongwe pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), yanalidhalilisha taifa.

rais kikwete alitoa kauli hizo katika kijiji cha kisesa wilayani magu jana wakati akihutubia wananchi kwenye ufunguzi wa mashindano ya ngoma kwa kabila la wasukuma; ngoma ambazo zinajulikana kama 'bulabo'.

" kila anayepata ukimwi anaufuata mwenyewe na wengine ni viherehere vyao; kwa mfano watoto wa shule," alisema rais kikwete wakati akijibu risala ya mkurugenzi wa makumbusho ya bujola, fadha frasince sandhu, ambaye alisema ujumbe wa mashindano hayo mwaka huu ni vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

kwa mujibu wa rais kikwete, suala la zinaa kwa bianadamu, siyo la lazima hivyo binadamu anaweza kujizuia ama kujikinga kwa kutumia kondomu.

" na kwa bahati mbaya shughuli ile (uzinzi) binadamu hana dharura nayo, hivyo unaweza kutumia kondomu kama unaona kwamba huwezi kutii amri ya sita ama huwezi kuwa mwaminifu katika ndoa yako," alisema kauli ambayo ilizua vicheko miongoni mwa watu waliohudhuria ufunguzi huo. Aliwashauri wananchi watakaoshiriki kwenye mashindano hayo wawe na tahadhari dhidi ya maambukizi ya ukimwi.

" ...katika mambo yanayolitia aibu taifa hasa kwa watani wangu wasukuma, ni pamoja na mauaji ya albino na vikongwe eti tu kwa sababu wana macho mekundu. Ni mambo ya fedheha sana ingawa yanakwenda yanapungua lakini yanalidhalilisha taifa," alisema.

aliwataka washiriki wa mashindano hayo walisaidie taifa katika kupiga vita mauaji ya aina hiyo.

rais kikwete alifuatana na wabunge kadhaa akiwemo waziri wa nishati na madini, william ngeleja (ccm) pamoja na mbunge wa bariadi magharibi, andrew chenge (ccm).

aidha, rais kikwete amepewa jina la mungubabu, ikiwa na maana busara na uwezo wa kuongoza nchi kama mungu.

mashindano ya 'bulabo' yalianza mwaka 1954 kupitia kanisa katoliki bujola, lengo likiwa ni kuweka burudani mara baada ya mavuno.

chanzo: nipashe
kula tano mkuu jk. Hujakosea kabisa
 
Kikwete hakutakiwa kuwa rais wa nchi kama Tanzania ambayo inahangaika sana kupata direction. Sidhani kama kweli huwa anajua vizuri mambo anayoonegea au anayoidhinisha. Wiki chache zilizopita tuliambiwa kuwa alisaini mswada wa sheria bila kuusoma, Wasiwasi wa aina hiyo hunitisha sana kuhusiana na maamuzi mengine aliyofanya kwa niaba ya nchi. One of them ni ule wa EAC. Mimi nindhanai kuwa position nzuriya Kikwete kisiasa ilikuwa ni "Waziri wa Nchi Asiyekuwa na Wizara Maalum"
 
Back
Top Bottom