Kikwete Mbeya: Mgongano na wananchi na mwitikio wa serikali

Nimehamasika sana na haya matukio, wamemfungia Kubenea kwa nini sasa ilihali taarifa alizozitoa zina fanana na haya matukio????

WITO: matukio haya yawe kama Propeller kwetu kwa ajili ya kuhamasisha na kuelimisha wananchi kwa ajili ya uchaguzi 2010 tuko kwenye pos nzuri na wakati mzuri kabisa.....
 
Huu useme wa wahenga ndiyo unatimia ..." You can not fool ALL the people ALL the time"

Hii habari imeandikwa kwenye gazeti la Nipashe toleo la leo, lakini very unfortunately gazeti hili sajaliona kwenye mauzo mpaka saa nne ya asubuhi leo...

mwenye nakala atuhabarishe kilichojiri... naamini mwandishi alikuwapo eneo la tukio...
 
Huu useme wa wahenga ndiyo unatimia ..." You can not fool ALL the people ALL the time"

Hii habari imeandikwa kwenye gazeti la Nipashe toleo la leo, lakini very unfortunately gazeti hili sajaliona kwenye mauzo mpaka saa nne ya asubuhi leo...

mwenye nakala atuhabarishe kilichojiri... naamini mwandishi alikuwapo eneo la tukio...

Inawezekana limenunuliwa lote na Mafisadi, Mod kama litapatikana naomba mscan hiyo habari nimwonyeshe mke wangu maana yeye na CCM ya Kikwete mhhh hawezi kuamini kama kuna Mtanzania anayeweza nyanyua jiwe kwa changuo la 'Mungu'
 
..hii habari imeandikwa kwenye nipashe ya leo..na ni bahati imetoka kwani magazeti mengine yameogopaa kuitoa au yameombwa....hata hilo nipashe lenyewe kuna uwezekano mkubwa lisifike mikoani maana mtandao wananunua kopi zote ambazo zilikuwa hazijafika distribution....

Ukitazama kwenye mtandao wa ipp bado haijawa uploaded na si kawaida ...ila ukifanya refine serch utaona hivi......
habari za ipp zimeanza kuwa uploaded ila page hazipatikani na ninahisi kama ile habari ya jk kupigwa mawe imehujumiwa, sijui! Ngoja tusubiri
 
...hakiyamungu .na UT ..mafisadi wamenunua nipashe yote leo...mimi mwenyewe nimepata moja lakini kwa mbinde......hapa naona mwandishi aliyechapisha hiyo habari anaitwa.......THOBIUS MWANAKATWE...chunya.
 
naona darleo wameshaiwekaa.....DarLeo-Gazeti lako la kila siku jioni......IPPMEDIA labda wana mgomo baridii naoo..........

Aibu nzito! Msafara wa JK kupopolewa mawe

*RC ashtuka, FFU wamwagwa

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

BAADA ya msafara wa Rais Jakaya Kikwete kushambuliwa kwa mawe jana mjini Mbeya, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wamemwagwa kijijini Kanga wilayani Chunya na wanaendesha msako mkali kuwanasa waliohusika, lakini hadi tunakwenda mitamboni hakuna aliyeripotiwa kukamatwa kuhusika na tukio hilo.

Msafara wa Rais Kikwete jana ulishambuliwa kwa mawe na watu wasiojulikana katika kijiji cha Kanga saa 1:30 jioni

Rais Kikwete yuko katika ziara ya siku 10 mkoani humo. Tukio hilo liliripotiwa kutokea wakati kiongozi huyo mkuu wa nchi akiwa njiani kuelekea Mbeya mjini kutoka Mwakajuni Chunya ambako alifanya ziara jana.

Ilidaiwa kwamba watu hao walichukua uamuzi kushambulia msafara huo kwa kile kilichodaiwa, hasira ya kushindwa kumwona Rais Kikwete baada ya kumsubiri kwa muda mrefu, apite kijiji hapo na wamweleze kero zao.

Kutokana na giza kutanda, Rais Kikwete hakuweza kusimama kijijini hapo, ndipo hasira za watu hao ziliibuka wakaamua kukusanya mawe na kuanza kupopoa mawe magari yaliyokuwa kwenye msafara huo.

Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, kimesema asubuhi hii kuwa jumla ya magari 12 yalishambuliwa kwenye tukio hilo, mawili yakivunjwa vioo huku dereva Simon Peter aliyekuwa akiendesha gari lenye namba STK 3107 akijeruhiwa vibaya kichwani na kulazwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Majeruhi mwingine aliyetajwa kujeruhiwa vibaya ni Skauti Barnabas Moses alijevunjika vidole viwili vya mkono wa kulia na anaendelea kupatiwa matibabu.

Wakati Polisi wakiendelea kusaka wahalifu hao waliofanya tukio hilo la aibu kuna taarifa kwamba serikali imefungua jalada namba MB/IR/ 8279, MB/RB 10512/2008 na MB/RB 10511/2008 kwa nia ya kuwashitaki watu hao kwa kosa la kujeruhi na kuharibu mali.

Baadhi ya wakazi mjini hapa, wameliambia Dar Leo kuwa pamoja na Mkuu wa Mkoa, John Mwakipesile kuwaambia waandishi wa habari jana kwamba waliofanya kitendo hicho ni walevi, watu hao hawapaswi kupuuzwa na wasichukuliwe kama walevi bali wasakwe na wakipatikana wapewe adhabu kali.

Mkuu huyo wa mkoa pia ameshtuka na kutangaza kuwa ratiba ya ziara ya Rais mkoani humo itafanyiwa marekebisho ili asisafiri tena muda wa usiku kuepuka balaa kama hilo.

"Hawa ni wahuni wamefanya kitendo cha aibu ambacho hakijawahi kutokea tangu nchi yetu ipate uhuru, wasiachwe hivi hivi wachukuliwe hatua kali," alisema Pearson Mwanjala mkazi wa kitongoji cha Mwanjelwa mjini Mbeya.

Tukio la kushambuliwa msafara kiongozi huyo mkuu wa nchi ambalo linazidi kuacha maswali mengi kuliko majibu, limekuja siku tano tu baada ya msafara wake kusimamishwa mara tatu na wakazi wa Mbeya Oktoba 10 alipoanza ziara yake mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Zelothe Steven amethibitisha kupelekwa kwa vijana wake kijijini Kanga kusaka wahalifu hao hata hivyo amesema kuwa taarifa kamili za tukio hilo zitatolewa baadaye leo.
 
...hakiyamungu .na UT ..mafisadi wamenunua nipashe yote leo...mimi mwenyewe nimepata moja lakini kwa mbinde......hapa naona mwandishi aliyechapisha hiyo habari anaitwa.......THOBIUS MWANAKATWE...chunya.

huyo muandishi na editor wajiandae mbona wataipata....
 
...hakiyamungu .na UT ..mafisadi wamenunua nipashe yote leo...mimi mwenyewe nimepata moja lakini kwa mbinde......hapa naona mwandishi aliyechapisha hiyo habari anaitwa.......THOBIUS MWANAKATWE...chunya.

Mkuu naomba uscan hiyo habari tutundikie hapa pse....
 
Watu wamechoka, malalamiko chungu nzima jamaa hasemi chochote kuhusu malalamiko hayo, kazi yake ni kukenua tu na kupretend kama hali ni shwari. Walimu wanagoma, Wafanyakazi walitaka kugoma mahakama ikawazuia, mafisadi bado wanapeta na yeye yote haya hayaingii akilini ili kuyatafakari kwa makini na kuyafanyia kazi kwa haraka.
 
Ninaposoma hili tukio najisikia kutetemeka.

Hapa ndio nguvu ya umma au ndio nini? Je, kama yamefanyika hivi kwa Rais mwenye ulinzi na makerubi wanaomzunguka, je hao wengine wasio nao...(tutajaza). Hapa tunapata picha gani, Kuwa leo Tanzania sio salama tena, KIMYA KINGI KINA MSHINDO MKUU au ndio kusema wananchi wakikosa wakuwasemea wanaweza kusjisemea kwa vitendo, au ni kukata tamaa kiasi cha kuona heri kufa kuliko kuishi?.

Kumbe kelele za kuzomea, sasa hazitakuwa tena kelele ila MAPAMBANO ya mapanga na sime na mawe! Jamani, Watu waliuwawa kwa mawe zamani kwa kuonekana najisi, je wakati huu?

Sipati picha halisi kama hili limetokea, ila kama ni kweli, ni wakati wa kufikiri nini cha kufanya kulinusuru taifa?

Hapana hapa nadhani wananchi walivuka mpaka, na sio stahili kuwafunga gerezani au kuwaua, tunahitaji kama taifa kukabiliana na hili kwa kutizama nyuma wapi tulipopotoka kiasi hiki na tubadili mwelekeo.

Tunahitaji kuliombea taifa letu liepukane na hukumu hii iliyo mbele. INASIKITISHA
 
Hivi kati ya Mbunge na Mkuu wa Mkoa nani ana madaraka zaidi mkoani? Nani anasimamia polisi na magereza?

Jasusi,

Dr. Mwakyembe ni lawayer, watu wakikamatwa unaenda polisi na mahakamani ili kuhakikisha wanatolewa/ wanawekewa dhamani. Suala hapa sio nani ana madaraka kuliko mwenzake, bali kutumia sheria zilizopo kuwatoa hao vijana kama kweli wamewekwa ndani.
 
Sasa naelewa kwa nini JKN alikuwa hachagui mtu wa Mara kuwa kiongozi wa mkoa wa Mara. Haya matatizo yangeepushwa Mbeya.

Jasusi,

Tatizo la Watanzania ni kupenda siasa na maneno mengi badala ya kuchapa kazi. Binafsi ningependa kupewa nafasi ya kufanya kazi nyumbani na siogopi kufanya kazi na mtu yeyote. Binadamu huwa hachagui jirani.

Tatizo la wanasiasa wetu hawana habari kabisa na matatizo ya wananchi wanaowaongoza na badala yake wanajali maslahi yao. Wabunge wanaona mkuu wa mkoa yuko pale kujijengea jina ili baadaye apate ubunge, hivyo kumwandama. Na mkuu wa mkoa na yeye anafanya kila jambo kuwakwamiza wenzake ili waonekane hawafai.

Kwanini wanasiasa wetu hawawezi kufanya kazi pamoja? Uchaguzi ukiisha watu waache maneno na washindane kwa kupeleka maendeleo na kuchapa kazi.

Siasa za nyumbani ni ujinga mtupu.

Watu wana matatizo na hakuna wa kuwasaidia, wabunge na viongozi wengine wanashinda Dar na Dodoma. Matokeo yake mpaka rais akifika ndio muda pekee wa kumfikishia matatizo yao na hii tayari inamletea balaa kubwa JK.
 
hawa watu bwana badala watumie kichwa ana kujiuliza sbb gani zimepelekea hayo... kama kawaida wanatumia mabavu.... hawajajifunza tuu kule tarime na mabavu yao???
 
Watanzania walewale: Kyela anasimikwa kuwa CHIFU; huku kungine anapigwa mawe!

Well, mafisadi na swahibas lazima wafanye kila jitihada kuhakikisha kinara wao anaonekana hero, na ndo maana hata habari za kuzomewa ziara yake zimekuwa zikifichwa, hata hii ya kupigwa mawe unaona ilivo sua sua kama si ushujaa wa Datoo, ndo basi tena japo ndo hivo asante JF wachache tungezipata humu!

Ila ukweli unabaki pale pale kwamba kwa mawe haya ni meseji senti, na namshauri avue hiyo miwani ya wapambe nuksi aangalie hali halisi ya watanzania atufanyie kazi kwa yale tulo mkabidhi si kulinda maslahi ya kakundi ka mafisadi huku mamilioni ya watanzania tukiteseka!

NA ASIPO ZIBA UFA AKAE TAYARI KUUJENGA UKUTA
 
Mzee Mwanakijiji,

Hii habari kama ni kweli si Dr. Mwakyembe aende kuwatetea na kuwatoa hao vijana? Kama mbunge ana wajibu wa kulinda maslahi ya wapiga kura wake.

Ungewashauri waliokutumia ujumbe waufikishe pia kwa mbunge wao ili kama hana habari basi achukue hatua.

Itakuwa ni ukichaa kuwakamata vijana kwasababu tu wanalalamikia uongozi uliopo.


Uhuru wa maoni kupitia mabango bado tuna safari ndefu sana. watu kusema hawamtaki kiongozi ni jambo la kawaida kabisa na wala si uchochezi,cha kufanya ni kunyamaza kimya tu yule mtu ambaye hatakiwa na kutafakari ni kwanini wamesema hivyo,naamini majibu kiongozi huyo atakuyanayo tu.
 
Baadhi ya wakazi mjini hapa, wameliambia Dar Leo kuwa pamoja na Mkuu wa Mkoa, John Mwakipesile kuwaambia waandishi wa habari jana kwamba waliofanya kitendo hicho ni walevi, watu hao hawapaswi kupuuzwa na wasichukuliwe kama walevi bali wasakwe na wakipatikana wapewe adhabu kali.

Hard to believe if this happens in a country where wananchi wanaishi kwa kuaminishwa Tanzania ni nchi ya amani na utulivu.

Definitely there is strong wind of change in this land.

Ndugu Mwakipesile: Ya kweli hayo kuhusu walevi?
 
Msafara wa JK wapigwa mawe

2008-10-16 13:47:02
Na Thobias Mwanakatwe, Chunya


Ziara ya Rais Jakaya Kikwete mkoani Mbeya imeingia dosari baada ya wananchi wa kijiji cha Kanga wilayani Chunya kupiga mawe magari sita yaliyokuwa katika msafara wake yakiwa yamewabeba mawaziri, waandishi wa habari na viongozi waandamizi wa serikali na kusababisha baadhi yao kujeruhiwa.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea katika kijiji hicho majira ya saa 7:30 usiku wakati msafara wa Rais ukiwa njiani kuelekea Mbeya mjini ukitokea mji wa Mwakwajuni wilayani Chunya ambako Rais Kikwete alikuwa ziarani.

Miongoni mwa magari yaliyopigwa mawe ni la Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawabwa, ambalo jiwe lilipiga upande wake na kugonga `wepa`. Hata hivyo, halikuvunja kioo wala kumjeruhi Waziri huyo.

Magari mengine yaliyopigwa mawe ni la Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwatumu Mahiza, gari la Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Thomas Mwang`onda lenye namba za usajili T 894 AAY na gari namba STK 2429 lililokuwa limewabeba waandishi wa habari, ambalo limevunjwa vioo vya mlango na waandishi wawili kujeruhiwa.

Magari mengine yaliyopigwa mawe na wananchi hao ni STK 3240 na STJ 3958 linalotumiwa na Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya, katika msafara huo lilikuwa limewachukua maafisa wa serikali kutoka Ikulu.

Kutokana na tukio hilo, waandishi wawili wa magazeti ya serikali pamoja na kijana mmoja, Chipukizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wote walijeruhiwa na walipewa huduma ya kwanza na madaktari ambao wapo katika msafara wa Rais mara baada ya magari kuwasili katika Ikulu Ndogo ya mjini Mbeya majira ya saa 3.00 usiku.

Baadhi ya viongozi waliozungumza na gazeti hili katika Ikulu Ndogo, walisema kuwa wananchi waliofanya tukio hilo walikuwa wamejipanga pembeni mwa barabara na baada ya magari manne ya mwanzo kupita, ndipo mawe yalianza kuvurumishwa.

Baada ya magari hayo manne kupita, magari yaliyokuwa nyuma yalianza kuvurumishiwa mvua ya mawe na wananchi hao.

Habari zaidi ambazo gazeti ilizipata zinaeleza kuwa hatua ya wananchi hao kufanya uhalifu huo ilitokana na hasira ya kushindwa kumwona Rais Kikwete baada ya kumsubiri kwa muda mrefu ili apite katika kijiji hicho na ili wamweleze kero zao.

Kutokana na muda kuwa umekwenda na giza kutanda, Rais Kikwete hakuweza kusimama katika kijiji hicho, hali iliamsha hasira za watu hao ambao waliamua kukusanya mawe na kuanza kushambulia magari yaliyokuwa kwenye msafara.

Hata hivyo, gari la Rais Kikwete, mke wake pamoja na walinzi wake hayakuhusika katika kadhia hiyo ya aina yake inayoashiria kuporomoka kwa maadili kwa kiwango cha juu kwa wananchi kiasi cha kutokuheshimu hata msafara wa kiongozi mkuu wa nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, akizungumza na waandishi wa habari saa 3:30 usiku Ikulu Ndogo mjini hapa, alisema waliofanya kitendo hicho ni walevi na kwamba serikali itahakikisha inachukua hatua kali dhidi yao.

Alisema kutokana na tukio hilo, ratiba ya Rais Kikwete katika ziara yake mkoani humo itabadilika na msafara wake hautatembea tena usiku.

Kuanzia sasa hivi ratiba ya msafara wa Rais kutembelea sehemu mbalimbali za mkoa itabadilishwa kwa kuanza mapema asubuhi na kurejea mapema ili kuepuka tukio kama la leo (jana) lisijirudie, alisema.

Mwakipesile alisema tayari kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kimepelekwa katika kijiji cha Kanga kusaka wahusika wa tukio hilo la aibu kuwahi kutoka katika Jamhuri ya Tanzania.

Tukio hili linatokea siku tano tu baada ya msafara wa Rais Kikwete kusimamishwa mara tatu na wakazi wa mkoa huo, Oktoba 10, mwaka huu siku alipoanza ziara ya siku 10.

Katika matukio hayo yaliyoanzia Mbeya Mjini eneo la soko la Mwanjelwa, wananchi walisimama barabarani kuzuia msafara wake ili kumweleza kilio chao juu ya mafisadi kutokuadhibiwa na hali ya maisha kuzidi kuwa duni miongoni mwao.

Pia walitaka kupewa sababu za kutokuwekwa matuta barabarani hali ambayo imesababisha watoto wao wengi kugongwa na magari; wananchi hao kadhalika walitaka kujua kwa nini hawana huduma ya maji safi.

SOURCE: Nipashe
 
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea katika kijiji hicho majira ya saa 7:30 usiku wakati msafara wa Rais ukiwa njiani kuelekea Mbeya mjini ukitokea mji wa Mwakwajuni wilayani Chunya ambako Rais Kikwete alikuwa ziarani.

Cha shangaza jamani hivi inakuwaje Kiongozi wa nchi anatembea usiku na gari vijijini ili hali ni giza tororo. unona sasa hata walizi wake na maaskari wengine hawakuwaona waliokuwa wanatupa mawe. kwa jinsi polisi wa tz walivyo maskini wanaishi wakijiji wakamatwa wasio husika
 
Back
Top Bottom