The Invincible
JF-Expert Member
- May 6, 2006
- 6,003
- 3,269
Description of Salva as Comical Ali is a fair comparison.
Ha ha ha! Comical Salva Rweyemamu. Jina hilo linakufaa mkubwa.
Description of Salva as Comical Ali is a fair comparison.
Salva ni kituko cha mwaka... ni heri arudi kwenye fani yake ambako anaweza kupata muda wa kuandika facts.... hizi hoax stories hazimsaidii yeye wala Rais wala mtanzania wa kawaida. Eti ametamka, nimesikia leo asubuhi kuwa wanaolalamika maisha magumu ni watanzania wachache walioko mijini tu... wale wa vijijini hawana maisha magumu kwani neema ya maisha bora, akataja... elimu bora, huduma bora za afya, barabara safi zipo vijijini.
!
Jamani Salva anakosa gani?. Kuna watu lazima waseme kuhusu watu?.
Simple mind discuss people.
Ordinary mind discuss events.
Great mind discuss ideas.
Whatever Salvz Says, that is his version. Everone is free to have his own version for his own ends. He is a Director of Communication-wa Ikulu. What do you expect his version to be!?.
What matters most was suppossed to be the media version of the story. That is what is suppossed to be nothing but the truth.
Kusema ukweli mimi nawahurumia hao watu zaidi ya 60 waliotiwa mbaroni kwa kadhia hiyo, kuna uwezekano mkubwa wasitendewe haki.
Mungu ibariki Tanzania.
Kikwete hakukatisha ziara Mbeya - Ikulu
(a) Rais akatisha ziara ya mkoa
Rais alipanga kukaa katika Mkoa wa Mbeya kwa siku 10. Amefanya hivyo. Hakukatisha ziara hiyo kama ilivyoandikwa katika baadhi ya magazeti. Aliingia Mbeya Oktoba 9, akaondoka Oktoba 13 jioni kwenda Tanga kuzima Mwenge, na alirejea jioni ya Oktoba 14 na kuondoka jana (juzi), Oktoba 18, jumla ya siku 10 kamili.
Ni vyema kujua kuwa kila Rais anapoweka mguu katika mkoa wowote, iwe ni asubuhi, mchana ama jioni ni siku kamili ya kuwapo kwake katika mkoa ama eneo hilo.
Kilichotokea ni kwamba kwa sababu ya ratiba kuwa na shughuli nyingi, ziko shughuli mbili ambazo hakuweza kuzifanya. Ameahidi atapata nafasi ya kwenda tena Mbeya kuzifanya.
(b) Mkutano wa majumuisho ya ziara kwenye Uwanja wa Sokoine
Na wala Rais hakuahirisha kuhutubia wananchi wa Mbeya kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine wakati wa majumuisho yake ya Mkoa huo kama inavyodaiwa.
Rais hakupangiwa kuhutubia mkutano kwenye uwanja huo kwa sababu alikuwa amekwisha hutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja huo, Februari 19, 2006, alipokwenda kuwashukuru wananchi wa mkoa huo kwa kukichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuongoza nchi yetu.
Na wala Rais hafanyi majumuisho ya ziara za mikoa kwenye mikutano ya hadhara. Huifanya kazi hiyo kwa kukutana na viongozi wa kisiasa, kijamii, kiuchumi, kidini, na kiusalama wa mikoa katika mkutano wa viongozi. Ndivyo alivyofanya jana (juzi) katika Ukumbi wa Mkapa mjini Mbeya.
(c) Kutotembelea Mbeya Vijijini
Kama nilivyoeleza, Rais alitembelea wilaya zote saba za mkoa huo zenye halmashauri nane kwa sababu Mbeya yenyewe ni wilaya moja lakini ina halmashauri mbili, moja ya mjini na nyingine ya vijijini.
Wakati mwingine uelewa wa waandishi wetu unapumbazisha kabisa. Jana, kabla ya kuingia kwenye mkutano wa majumuisho, Rais alitembelea kiwanda cha kutotoa vifaranga vya kuku katika eneo la Songwe, ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa Songwe, pamoja na kuzindua hospitali teule ya wilaya ya Ifisi, vyote vikiwa katika eneo la Wilaya ya Mbeya, lakini maeneo ya vijijini.
(d) JK akiri Mbeya ni pagumu
Huu pia ni upotoshaji mwingine. Kama kuna kitu Rais amekisema wakati wa majumuisho ya ziara yake jana ni kuumwagia sifa sana mkoa huo kwa jitihada za maendeleo ya wananchi - iwe katika elimu, iwe katika afya, iwe katika kilimo, iwe ni katika huduma za maji, iwe ni katika ufugaji, iwe katika umwagiliaji na maeneo mengine muhimu ya maendeleo.
Kile kinachoelezwa kuwa Mbeya ni pagumu, ni pale alipowasihi viongozi kujenga tabia na mwenendo wa uongozi wa pamoja akisisitiza kuwa viongozi hao wanajenga nyumba moja na hivyo hawana sababu ya kugombea fito kwa sababu ya tofauti zilizopo miongoni mwa baadhi ya viongozi wa mkoa huo.
Tofauti miongoni mwa viongozi wachache wa mkoa huo haziufanyi mkoa mzima wa Mbeya kuwa mgumu.
(e) Msafara wa Rais kupigwa mawe
Mwenendo mzima ambao uongozi wa Mkoa wa Mbeya unaweza kujivunia ni kujitokeza kwa wingi mno kwa mamia ya wananchi wa mkoa huo kila alipopita Rais ama kwenda kwa shughuli za maendeleo wakati wa ziara hiyo.
Kila sehemu, wananchi walimtaka asimame, wamwone, awasalimie. Na kama ilivyo ada, hakusita, hata sehemu moja, kufanya hivyo.
Hamu ya wananchi wa Mbeya kumwona na kumsikiliza Rais wao ndiyo ilimfanya Mhe. Rais kusema kuwa alikuwa ameondoka Mkoa wa Mbeya akiwa na kumbukumbu nzuri za wema, ukarimu na upendo wa wananchi wa Mbeya.
Ilikuwa ni hamu hiyo hiyo ambayo wananchi wa kijiji cha Kanga walikuwa nayo wakati Rais anafanya ziara ya Wilaya ya Chunya ambako alipitia na kuhutubia mikutano mikubwa ya wananchi katika maeneo ya Chunya Mjini, Makongorosi na Mkwajuni.
Kwa bahati mbaya wakati anawasili katika kijiji cha Kanga tayari ilikuwa usiku kati ya saa moja na saa mbili kwa sababu ratiba ya maeneo mengine ilikuwa imecheleshwa mno na hamu ya wananchi wa maeneo hayo kumsimamisha na kumwona Rais wao. Hivyo, msafara wake ukapita bila kusimama katika kijiji hicho.
Kile kitendo cha kiongozi wao kutosimama katika kijiji hicho ambako wananchi walikuwa wamejitokeza kwa mamia, wakasimama barabarani kwa saa nyingi wakiwa na hamu kumwona Rais wao, kikachochea na kusisimua tahayari (frustration) kwa vijana ambao wakaanza kurusha mawe kwenye baadhi ya magari yaliyokuwa kwenye msafara. (d) Magari ya Rais
Magari ya Rais, kwa maana ya magari yote yanayotengeneza sehemu kuu ya msafara wa Rais, hayakutupiwa hata jiwe moja. Na wala Rais mwenyewe hakupata habari za tukio hilo mpaka alipokuwa amewasili Ikulu ya Mbeya.
Na alipopata habari hizo alitoa maelekezo maalum kuwa zisije zikachukuliwa hatua za kipolisi kusumbua kijiji kizima na kutaka upelelezi wa suala hilo ufanyike kwa uangalifu mkubwa bila jabza.
Magari yaliyotupiwa mawe ni yale yaliyokuwa nyuma katika sehemu ya pili ya msafara, yaani nje ya sehemu kuu ya msafara. Na mpaka Rais anaondoka Mbeya jana (juzi), ni watu watano tu walikuwa wametiwa mbaroni, tofauti na habari za kubuni za magazeti kuwa wamekamatwa watu 60.
Rais anaamini kuwa tukio hilo la kijiji cha Kanga ni tukio la uhalifu. Kamwe haiwezi kutokea Rais Kikwete asisumbuliwe na tukio lolote la uhalifu katika nchi yetu. Hili ni tukio lililomkera, lakini kama alivyoeleza jana (juzi) kazi hiyo waachiwe polisi.
Muhimu kusisitiza hapa ni kwamba tukio hilo siyo linalowakilisha taswira ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya ambao wameonyesha mapenzi makubwa kwa kiongozi wao mkuu.
Ni makosa kwa kuuchukulia mkoa mzima wa Mbeya kama mkoa wa wahalifu kwa sababu ya tendo lililotendwa na watu wachache katika kijiji kimoja tu.
Na Gazeti La Uhuru!
Hii Habari Imenifurahisha Sana Nikaona Si Mbaya Kuwashirikisha!
Kikwete hakukatisha ziara Mbeya - Ikulu
*Ni chokochoko za magazeti, ilikuwa na mafanikio makubwa
Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete hakukatisha ziara katika mkoa wa Mbeya, kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Ni choko choko za magazeti? Sasa magazeti yamekua maadui wa Mtandao? Kweli ushirika wa wachawi haudumu.
Kikwete hakukatisha ziara Mbeya - Ikulu
*Ni chokochoko za magazeti, ilikuwa na mafanikio makubwa
(e) Msafara wa Rais kupigwa mawe
Mwenendo mzima ambao uongozi wa Mkoa wa Mbeya unaweza kujivunia ni kujitokeza kwa wingi mno kwa mamia ya wananchi wa mkoa huo kila alipopita Rais ama kwenda kwa shughuli za maendeleo wakati wa ziara hiyo.
Kila sehemu, wananchi walimtaka asimame, wamwone, awasalimie. Na kama ilivyo ada, hakusita, hata sehemu moja, kufanya hivyo.
Hamu ya wananchi wa Mbeya kumwona na kumsikiliza Rais wao ndiyo ilimfanya Mhe. Rais kusema kuwa alikuwa ameondoka Mkoa wa Mbeya akiwa na kumbukumbu nzuri za wema, ukarimu na upendo wa wananchi wa Mbeya.
Ilikuwa ni hamu hiyo hiyo ambayo wananchi wa kijiji cha Kanga walikuwa nayo wakati Rais anafanya ziara ya Wilaya ya Chunya ambako alipitia na kuhutubia mikutano mikubwa ya wananchi katika maeneo ya Chunya Mjini, Makongorosi na Mkwajuni.
Na Gazeti La Uhuru!
Hii Habari Imenifurahisha Sana Nikaona Si Mbaya Kuwashirikisha!
"Wananchi hawa si vichaa. Hata sababu zilizotolewa na serikali kwamba wananchi walishambulia msafara wa rais kwa kuwa walikuwa na kiu ya kumuona lakini hakusimama kijijini kwao kwa sababu ya giza, hazieleweki kwa watu wenye kupenda kufikiri na kutafakati kidogo.
Wananchi wanaompenda kiongozi wao hawamrushii mawe kumdhuru yeye au watu walioambatana naye. Najua serikali yenyewe haiamini kauli yake, ndiyo maana imemwaga mashushushu mahali hapo kuchunguza sababu za kitendo hicho.
Hata hivyo, tunapaswa kujiuliza. Kwanini sasa wananchi wanaonekana kushabikia urushaji mawe? Huu ndio ukomo wa uvumilivu wao wa siku nyingi? Ndiyo njia mpya ya kujieleza kwamba wamechoka kupuuzwa?
Ndiyo njia ya kuwafanya wakubwa wawasikilize? Je, baada ya mawe watatumia silaha gani? Je, wakubwa wapo tayari kujifunza kutokana na mawe wanayorushiwa na wananchi? Au wataendelea kuwatuma polisi warushe risasi kudhibiti mawe hayo? Je, watafanikiwa?"
[(e) Msafara wa Rais kupigwa mawe
Mwenendo mzima ambao uongozi wa Mkoa wa Mbeya unaweza kujivunia ni kujitokeza kwa wingi mno kwa mamia ya wananchi wa mkoa huo kila alipopita Rais ama kwenda kwa shughuli za maendeleo wakati wa ziara hiyo.
Kila sehemu, wananchi walimtaka asimame, wamwone, awasalimie. Na kama ilivyo ada, hakusita, hata sehemu moja, kufanya hivyo.
Hamu ya wananchi wa Mbeya kumwona na kumsikiliza Rais wao ndiyo ilimfanya Mhe. Rais kusema kuwa alikuwa ameondoka Mkoa wa Mbeya akiwa na kumbukumbu nzuri za wema, ukarimu na upendo wa wananchi wa Mbeya.
Ilikuwa ni hamu hiyo hiyo ambayo wananchi wa kijiji cha Kanga walikuwa nayo wakati Rais anafanya ziara ya Wilaya ya Chunya ambako alipitia na kuhutubia mikutano mikubwa ya wananchi katika maeneo ya Chunya Mjini, Makongorosi na Mkwajuni.
Kwa bahati mbaya wakati anawasili katika kijiji cha Kanga tayari ilikuwa usiku kati ya saa moja na saa mbili kwa sababu ratiba ya maeneo mengine ilikuwa imecheleshwa mno na hamu ya wananchi wa maeneo hayo kumsimamisha na kumwona Rais wao. Hivyo, msafara wake ukapita bila kusimama katika kijiji hicho.
Kile kitendo cha kiongozi wao kutosimama katika kijiji hicho ambako wananchi walikuwa wamejitokeza kwa mamia, wakasimama barabarani kwa saa nyingi wakiwa na hamu kumwona Rais wao, kikachochea na kusisimua tahayari (frustration) kwa vijana ambao wakaanza kurusha mawe kwenye baadhi ya magari yaliyokuwa kwenye msafara.
(d) Magari ya Rais
Magari ya Rais, kwa maana ya magari yote yanayotengeneza sehemu kuu ya msafara wa Rais, hayakutupiwa hata jiwe moja. Na wala Rais mwenyewe hakupata habari za tukio hilo mpaka alipokuwa amewasili Ikulu ya Mbeya.
Na alipopata habari hizo alitoa maelekezo maalum kuwa zisije zikachukuliwa hatua za kipolisi kusumbua kijiji kizima na kutaka upelelezi wa suala hilo ufanyike kwa uangalifu mkubwa bila jabza.
Magari yaliyotupiwa mawe ni yale yaliyokuwa nyuma katika sehemu ya pili ya msafara, yaani nje ya sehemu kuu ya msafara. Na mpaka Rais anaondoka Mbeya jana (juzi), ni watu watano tu walikuwa wametiwa mbaroni, tofauti na habari za kubuni za magazeti kuwa wamekamatwa watu 60.
Rais anaamini kuwa tukio hilo la kijiji cha Kanga ni tukio la uhalifu. Kamwe haiwezi kutokea Rais Kikwete asisumbuliwe na tukio lolote la uhalifu katika nchi yetu. Hili ni tukio lililomkera, lakini kama alivyoeleza jana (juzi) kazi hiyo waachiwe polisi.
Muhimu kusisitiza hapa ni kwamba tukio hilo siyo linalowakilisha taswira ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya ambao wameonyesha mapenzi makubwa kwa kiongozi wao mkuu.
Ni makosa kwa kuuchukulia mkoa mzima wa Mbeya kama mkoa wa wahalifu kwa sababu ya tendo lililotendwa na watu wachache katika kijiji kimoja tu.
Press Release ya Salva Rweyamamu ilitakiwa isomeke hivi:.
Kisa cha wananchi kushambulia msafara wa Raisi ni kuwa Raisi alikataa amri halali ya wapiga kura wake ambao walijitokeza kwa wingi mno barabarani wakimtaka asimame na msafara wake ili atoe maelezo kwa nini maisha ya wanakijiji wa Kanga ni magumu tofauti na ahadi ya Raisi ya maisha bora kwa kila mtanzania.
Raisi na msafara wake wakafanya jeuri wakakataa amri halali ya wananchi ambao ndio waliompa kura.
Wananchi wa Kijiji cha Kanga walipoona amekataa kusimama ndipo walipoamua kuuvurumishia mawe msafara wake kwa lengo la kumshinikiza asimame kitendo ambacho kilimfanya aongeze spidi ya kukimbia kwa mwendo wa kuua mtu kuwatoroka wapiga kura wenye hasira waliokuwa wakirusha mawe mfululizo.
Raisi akagoma kusimama hadi alipofika Mbeya ambako aliamuru wakamatwe wapiga kura walioamuru asimame na wakamrushia mawe waswekwe ndani.
Na hadi muda huu wapiga kura hao bado wako ndani na Raisi bado hajatoa maelezo kwa hata wapiga kura hao walioko ndani kwa nini maisha bora kwao na kwa kila mwanakijiji wa Kanga aliyerusha mawe na yule ambaye hajarusha mawe hayajawezekana.
Kitendo walichokifanya wananchi wa kijiji hicho ni cha kipekee hakilingani na sehemu zingine za Mbeya ambako wananchi hawakumpa amri ya kusimama ajieleze.