Serikali tunataka majibu juu ya uwepo wa mgodi wa siri katikati ya msitu huko Kitunda

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
Kuna taarifa za uwepo wa mgodi mkubwa wa madini katikati ya msitu huko Kitunda Tabora mpakani na Singida. Inadaiwa mgodi huo upo kwa siri na haujulikani katika mfumo wa serikali isipokuwa viongozi wachache ambao ndio waliohusika kuuza eneo hilo kwa maslahi binafsi.

Kutokana na usiri huo hakuna barabara yoyote inayoenda katika mgodi huo isipokuwa kuna uwanja wa ndege wa siri ambao hutumika kwa ndege kubeba madini pamoja na kuleta mahitaji katika eneo. Ukitembea kwa mguu kuelekea katika mgodi huo itakuchukua siku 3 mpaka tano kufika. Mgodi huo una ulinzi mkali ikiwemo kuzungushiwa face yenye ulinzi na CCTV camera.

Sasa nchi yetu ina jeshi la JWTZ ambalo moja ya majukumu yake ni kulinda mipaka ya nchi, sasa nauliza jeshi letu lilishindwa kubaini wageni waliovuka mpaka na kuanzisha mgodi mkubwa katikati ya nchi yetu na kuchimba madini na kuyatorosha? Vipi kuhusu vyombo vingine vya dola navyo havijui mchongo huu wa wakubwa? Sitaki kuzungumzia Usalama wa Taifa TISS kwa sababu TISS ya sasa haina tofauti na Green Guard ya UVCCM na imekosa sifa ya kuitwa chombo cha dola kama ilivyokuwa wakati wa mkapa mpaka wakati wa Nyerere.

Haya mambo ya migodi ya siri tulikuwa tunayasikia huko Congo ambako nchi yao ina tatizo la usalama sasa leo na sisi tuna tatizo hilo? Au Rushwa na tamaa za viongozi ndio vimepelekea jambo hili? Hapana , hapana lazima tuchukue hatua. Tumechoka kuendelea kuona rasilimali za taifa hili zinawanufaisha wageni kutoka nje ya nchi na wazawa wakibaki maskini huku maji, madawa, shule na chakula vikiwa adimu katika maeneo hayo.

Hivyo sisi kama Watanganyika na Watanzania tunahitaji serikali itoke hadharani ituambie kuhusu huo mgodi kabla hatujachukua hatua ambazo tunaamini tutalinda rasilimali za taifa letu kwa maslahi ya wananchi.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
Screenshot_20240303-212250_1~2.jpg
 
Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.View attachment 2923947
Wewe Mdude_Nyagali ni kenge kabisa. Sasa kama mpaka kenge wewe unajuwa itakuwaje ni mgodi wa siri?

Yaani iwe siri halafu na wewe ujuwe? Ridiculous
 
Back
Top Bottom