Kikwete Mbeya: Mgongano na wananchi na mwitikio wa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Mbeya: Mgongano na wananchi na mwitikio wa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 6, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,596
  Trophy Points: 280
  Christopher Nyenyembe, Mbeya
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  WAFANYAKAZI waliopunguzwa kazi katika mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira (KCM), mkoani hapa mwaka 2005, wanaoidai serikali zaidi ya sh bilioni 47, wamemgeuzia kibao Rais Jakaya Kikwete, wakimtaka aongozane na maofisa wa hazina watakaowalipa fedha hizo.

  Hatua hiyo inayoonekana kumtega Rais Kikwete, imetokana na taarifa kuwa Rais Kikwete, anatarajia kufanya ziara yake ya kwanza katika mkoa huu hivi karibuni.

  Baadhi ya wafanyakazi waliozungumza na Tanzania Daima, jana walisema wanataka kuonana na Rais Kikwete ili wamfikishie kilio chao ambacho hakijapatiwa ufumbuzi tangu walipopunguzwa kazi.

  Wafanyakazi hao walidai kusikitishwa na hali hiyo, kwani hata kamati ya rais aliyoiunda kuchunguza sekta ya madini na mikataba, ilipita katika mgodi huo na kupokea kilio cha wafanyakazi hao, lakini bado hawajalipwa fedha zao.

  Wafanyakazi hao wanaililia serikali kwamba hawajalipwa mafao na mishahara yao ya miezi kadhaa waliyokuwa wakidai tangu mgodi huo ulipokuwa chini ya serikali na kuwafanya washindwe kuondoka kwenye nyumba za mmiliki mpya aliyekabidhiwa mgodi huo.

  "Baada ya suala letu kushindikana kwa muda mrefu, sasa tunataka kutumia ujio wa rais kuwasilisha kilio chetu kwake kwani ndiye pekee aliyebaki kutusaidia," alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

  Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Migodini (TAMICO), Thomas Cheyo, alisema jana kuwa hali za wafanyakazi hao waliopunguzwa kazi tangu mwaka 2005 ni mbaya na wengi hawana chakula, hivyo ujio wa Rais Kikwete ni faraja kwao.

  "Tumepata taarifa kuwa Rais Kikwete anakuja Mbeya, tunaomba atembelee hapa mgodini ili tuweze kumfikishia kilio chetu, tangu tulipopunguzwa kazi mwaka 2005, tunaidai serikali mafao yetu ya zaidi ya sh milioni 47 lakini hatujalipwa, wengine wamekufa, wengine wana hali mbaya, hata Mbunge wetu, Dk. Harrison Mwakyembe tumemueleza," alisema Cheyo.

  Alisema kitendo cha serikali kushindwa kuwalipa haki zao, kimewazidishia ugumu wa maisha na hawaelewi yupi mwenye jibu sahihi kuhusu hatima ya malipo hayo.

  Mkuu wa mkoa huo, John Mwakipesile alipohojiwa kuhusu nafasi ya rais kuutembelea mgodi huo katika ziara yake ya kikazi, alisema hajapangiwa kuutembelea mgodi huo.

  "Rais kweli anakuja Mbeya, lakini hana ratiba ya kutembelea mgodi wa Kiwira katika ziara yake, kesho nina kikao na waandishi wa habari saa nane ofisini kwangu ili kuzungumzia ziara hiyo," alisema Mwakipesile alipokuwa akizungumza jana kwa simu.

  Uamuzi wa serikali ya mkoa kutompangia ziara rais kuutembelea mgodi huo, kunaweza kuzidisha kilio cha muda mrefu kwa wafanyakazi hao ambao mkuu wa mkoa huo, Mwakipesile aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Kyela na kwenye bodi ya Kiwira, ni miongoni mwa viongozi wanaojua undani wa matatizo ya wafanyakazi hao, ambayo hayajapatiwa ufumbuzi.
   
 2. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Ahakikishe anamkamata mkapa alipe hawa watu, kwa kuwa mkapa na yona walinunua mgodi huu pamoja na mali na madeni(asset and liabilities)
   
 3. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  nilishawahi kutembelea kule siku moja. uyo jamaa wanamtaka sana, ati watu wa kule wanamchukia kwasababu ati hawajali na kwamba alichukua nafasi ya mwandyosa wao na kwamba hajamlinda kabisa mwakyembe. inaonekana hata kura za uchaguzi ujao jamaa atapata chache sana toka mkoa wa mbeya. wao ndivyo wanavyosema.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,596
  Trophy Points: 280
  Mwandishi Wetu Oktoba 8, 2008
  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

  WAKATI Rais Jakaya Kikwete anaanza ziara mkoani Mbeya leo Jumatano, wasiwasi umetanda miongoni mwa wananchi juu ya kuwapo harakati za kufanya fujo.

  Taarifa kutoka kwenye wilaya za mkoa huo zinabainisha kuwapo kwa vitisho dhidi ya baadhi ya wananchi kwa madai kwamba wamepanga kufanya fujo wakati wa ziara hiyo ya Rais jambo walilodai ni uongo.

  Baadhi ya wananchi waliozungumza na Raia Mwema wamesema kwamba madai ya fujo hizo ni juhudi za Mkuu wa Mkoa huo, John Mwakipesile, kuhakikisha kwamba wananchi hawamzomei yeye wakati Rais Kikwete atakapokuwa akitembelea sehemu mbali mbali za mkoa huo.

  Wananchi hao (majina yanahifadhiwa), wanahoji, "Kwa nini azunguke mkoa mzima na kusema uongo kuwa tunataka kumfanyia fujo Rais, na kama ni msafi, kwa nini aandae makundi ya wazee mamluki Ileje, Kyela, Mbarali, Mbozi na Mbeya Mjini ya kula chakula na Rais ili wampambe kwa Rais na yeye kuendelea kuutesa mkoa wa Mbeya?"

  Mbali ya kuwasiliana na vyombo vya habari, kumekuwapo na ujumbe mfupi wa simu uliosambazwa kwa watu mbali mbali vikiwamo vyombo vya habari ambao pamoja na mambo mengine unamwelezea Mkuu huyo wa Mkoa kama mtu mgomvi, mfitini, mkabila na mchochezi.

  "Sisi tunampenda Rais wetu, ila hatumtaki RC Mbeya, RC ni mgomvi, mfitini, mkabila na mchochezi," inasema sehemu ya ujumbe huo.

  Baadhi ya wabunge waliohojiwa wamelezea kusikitishwa kwao ni jinsi baadhi ya viongozi wa Serikali mkoani humo, wanaodaiwa kuwa wanamtandao, wanavyompotosha Rais kuhusu hali ya kisiasa mkoani humo, na kuielezea hatua hiyo kuwa inalenga kudidimiza maendeleo ya mkoa kwani mambo yote ambayo yamekuwa yakizungumzwa hayana ukweli wowote.

  "Walianza kuvumisha kwamba Mwandosya (Profesa Mark) anajitangaza kuwa yeye ndiye Rais. Hivi katika akili ya kawaida tu wewe unaweza kuamini kwamba Profesa anaweza kufanya upuuzi kama huo? Yote ni kumgombanisha na Rais. Mara wanasema Rais Kikwete hampendi Profesa Mwandosya, lengo wajenge chuki kati ya Rais na wananchi. Baadhi ya wabunge wameandaa vikundi vya kumzomea Rais, lazima Mbeya tuzikatae siasa hizi za kipuuzi," alisema mmoja wa wabunge wa mkoa huo.

  Wafuatiliaji wa siasa za Mkoa wa Mbeya wanabainisha kwamba tatizo la msingi katika ziara za Rais Kikwete mkoani humo ni hofu waliyonayo baadhi ya viongozi, hususani Mkuu wa Mkoa huo, ya kukataliwa mbele ya Rais kutokana na wananchi walio wengi kutomkubali.
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kutoka kwa Michuzi Blog

  Na Mwandishi wetu, Mbeya


  Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuanza ziara ya siku 10 ya mkoa wa mbeya ambapo anatarajiwa kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya zote saba za mkoa huo wa kusini nyanda za juu.

  Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. John Mwakipesile amewaomba wakazi wa mkoa huu kujitokeza kwa wingi kumpokea JK ambaye anazuru Mbeya kwa mara ya kwanza toka achaguliwe kuwa rais Desemba 2005.

  Mr. Mwakipesile ameviambia vyombo vya habari leo kwamba JK atalala katika kila makao makuu ya wilaya katika ziara hiyo, mbali na kukaguia miradi na kuhutubia wananchi.

  Kwa mujibu wa Mh. Mwakipesile, akishawasili kesho na kuapata ripoti ya mkoa Ikulu ndogo ya Mbeya, ataelekea Mwakaleli katika wilaya ya Rungwe ambako atazi ndua kiwanda kipya cha chai na baadaye atahutubia wananchi.

  Amesema siku itayofuata ataelekea Kyela kabla mya kuvuka kuelekea Ileje na Chunya. Okotoba 13 atakagua kituo cha ukulima cha Uyole na baadaye mchana ataweka jiwe la msingi katika Mbeya City Hostels inayojengwa. Kisha ataruka kwenda Tanga kwenye sherehe za kuzima mwenge.

  Shughuli zingine za maendeleo atakazozindua ni kuzindua tawi la benki la CRDB la Mbozi, Saccos ya kijiji cha Ilembo pamoja na kukagua hospitali teule ya wilata ya Mbeya huko Ifilisi, sehemu za Mbalizi. Pia atakagua ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Oct 8, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hatimaye imekuwa na bila ya shaka hili litazima mzizi mzima wa fitina. Lisije kuanzisha fitina nyingine tu maana wenye fitina huwa hawachoki.
   
 7. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mzee Mwanakijiji,

  Watazua mengine, kinachoitwa ugomvi kati ya prof. na JK ni kamradi ka baadhi ya watu. Ukiisha wao watakula nini?

  JK anaenda kukagua uwanja wa Songwe ambao mara nyingi tumeambiwa hapa umesimama ili kutokumpa sifa prof. Huwa najiuliza hizi habari watu wanatoa wapi?

  Prof. mwenyewe alikuwa Kyela juzi kuhakikisha hiyo ziara inaenda salama.
   
 8. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  tunasubiri tuone hilo, wengine tupo hapa mbeya hatujui kinachoendelea, ila muungwana atawasili hapa leo saa tisa, jana nimesikia matangazo kibao kuwa mkuu wa wilaya leonidas gama anawatangazia watu wajitokeze kwa wingi na wala siyo mkuu wa mkoa, labda ndo itifaki yenyewe
   
 9. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #9
  Oct 9, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Maneno mengi ya nini.watu bwana utadhani Simba na Yanga vile
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Oct 15, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wananchi kadhaa wa Kyela inadaiwa wametiwa mikononi mwa Polisi baada ya kusimamisha bango lenye maneno ambayo yanaweza kuchukuliwa kuwa ni kichochezi wakati wakati wa mkutano wa Rais Kikwete katika ziara yake wilayani humo siku chache zilizopita..

  Taarifa hiyo ambaye imetumwa kwa ka “nzi” kalikokuwa kanaruka ruka kakimind its own business unasema hivi:

  “Haki za binadamu ziko wapi? … Eric Sata, na wenzake watatu Lwitiko, Roger na Thomas wote wa kituo cha mabasi Kyela wako rumande kwa siku tano na wamehamishiwa Mbeya leo bila dhamana wala kufunguliwa mashtaka kosa lao ni kukutwa na bango likisema “Kikwete tunakupenda, ila hatumtaki Mwakipesile; ondoka naye”

  Ujumbe huo uliotumwa kwa simu unasema kuwa "kuna taarifa kwamba (kina Sata) wanateswa ili waseme kuwa wametumwa na Dr. Mwakyembe na Prof. Mwandosya. Upuuzi wenu wa kumlinda Mwakipesile, usituulie ndugu zetu hatutakubali."

  Nimepata nafasi ya kuzungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Bw. Stephen Zelothe ambaye alikataa kuthibitisha au kukanusha taarifa hizo akidai kuwa anafanya jambo muhiimu sana na nimtafute wakati mwingine.


  KLHN itaendelea kufuatilia taarifa hii ili hatimaye ukweli wake au uongo wake uonekane....for now I'm erring on the side of caution...
   
 11. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyu Mwakipesile anajifanya mungu mtu?. Wananchi wa mkoa wa mbeya hawakutaki kwanini wasiseme?. Mwakipesile na kundi lake waachilieni vijana hao mara moja ama na wewe watoto wako hawatakwenda shule ama popote pale.
   
 12. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji,

  Naona haya mambo ya mitandao yenu yatawakimbiza watu miaka hii kwa jinsi mnavyofunua visa vyao wanavyovifanya gizani na ghafla vinawekwa peupe kwa kila mtu kujua......watatafutana sana miaka hii.

  Nadhani wangekuwa na uwezo ule mradi wa kufunga "fibre optic" nchi nzima ifikapo 2010 utakaotumia dola 170 millioni wangeupiga STOP kwanza....ili waendelee na mambo yao ya kiimla.
   
 13. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ina maana hili si muhimu? Hawa watu wengine sijui hata hizi kazi wanafanya vipi! Whatever he was doing, "jambo muhimu" is neither the right language nor excuse.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Oct 15, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ungeongeza "sana" maana siwezi kumlaumu maana Rais nadhani bado yuko mkoani Mbeya kwa hiyo naweza kuelewa "jambo muhimu sana" ina maana gani. Lakini alizungumza kama hajui kinachoendelea na kuahidi kufuatilia... hadi aende "kutafuta jibu"..
   
 15. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kichwa cha Habari: Wako Lock Up kwa kumnyanyulia JK bango Kyela!..

  Mstari wa kwanza: Wananchi kadhaa wa Kyela inadaiwa wametiwa mikononi mwa Polisi

  Details za ndani:
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Bw. Stephen Zelothe ambaye alikataa kuthibitisha au kukanusha taarifa hizo

  Ha haa ahaaaaa!

  Kwa hiyo, huyu mleta habari angekuwa anauza gazeti, au tungekuwa tunachajiwa senti kwa kila thread unayofungua tungekuwa tumeliwa hapa tukifungua tukiwa na fikra kwamba ndani kuna cheche za kweli!
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Oct 15, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  umesoma kianzio kimesemaje..
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ha haa ahaaaaa!

  Kwa hiyo, huyu mleta habari angekuwa anauza gazeti, au tungekuwa tunachajiwa senti kwa kila thread unayofungua tungekuwa tumeliwa hapa tukifungua tukiwa na fikra kwamba ndani kuna cheche za kweli!


  Mkuu Kuhani,

  Tunakuomba ule uchunguzi wako wa Dr Masao na THI, ni kilio cha wengi hapa kupata ukweli unaoujua wewe....pse!!!
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Oct 16, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hakuna ulazima wa hilo, tumelishasamehe tugange yajayo. Alikosea tu kidogo kama wanadamu wengine na hatuwezi kuendelea kumshikilia nalo. Hii ni tetesi kuwa kuna watu wapo Lock up kwa sababu ya kumuinulia bango Kikwete... ni uvumi ambao kuna watu (mimi mmoja wao) wanaoamini kuwa ni kweli until proven otherwise.
   
 19. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #19
  Oct 16, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mzee Mwanakijiji,

  Hii habari kama ni kweli si Dr. Mwakyembe aende kuwatetea na kuwatoa hao vijana? Kama mbunge ana wajibu wa kulinda maslahi ya wapiga kura wake.

  Ungewashauri waliokutumia ujumbe waufikishe pia kwa mbunge wao ili kama hana habari basi achukue hatua.

  Itakuwa ni ukichaa kuwakamata vijana kwasababu tu wanalalamikia uongozi uliopo.
   
 20. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #20
  Oct 16, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtanzania,

  Tanzania hii ya leo, vichaa/wendawazimu wako wengi!
   
Loading...