Kikwete: Lowassa ndiye mhusika wa Richmond

Kikwete: Lowassa ndiye mhusika wa Richmond

Status
Not open for further replies.
Kikwete aweka wazi kuwa waziri mkuu kipindi hicho ndio muhusika mkuu kwenye Richmond, baraza la mawaziri pamoja na yeye walihusika nawalikubaliana kuwa kuna upungufu wa umeme na mitambo ikanunuliwe lakini hakuhusika kampuni gani ya kwenda kuleta hiyo mitambo .

Alisisitiza sheria za manunuzi zifuatwe lakini waziri mkuu wa wakati huo hakufata na aliunda tume ya manunuzi ya kwake mwenyewe .

Heh na nyie mkamwamini kabisa, yani waziri mkuu alikuwa na mamlaka kumzidi yeye! Duh basi huyu jamaa ni hatari kweli, yani hadi rais akashindwa kumuwajibisha!? Dah
 
Udhaifu wa Kikwete huo ...ndio maana CCM wanapita ktk hali hii .....lakini udhaifu wa Kikwete haubadili ukweli juu ya Lowasa kuwa hafai kuwa mkuu wa nchi ....

Na ukweli wa Lowassa kutofaa kuwa mkuu wa nchi haubadili ukweli wa CCM kutofaa kuendelea kuwa chama tawala baada ya kushindwa kabisa kutawala kwa zaidi ya nusu karne.

Ukisema Lowassa hafai kuwa mkuu wa nchi na ukasema CCM nayo haifai kuendelea kutawala, basi hapo tutakuwa kwenye ukurasa mmoja.

Lakini usije na habari za eti Lowassa hafai halafu CCM wanafaa kuendelea kutawala kwa miaka mingine 5!

Nitakuona mwendawazimu!!
 
Mswahili katika ubora,hata aibu hana.rais mzima unakuwa mwongo namna hii.na kwa ujasiri kabisa anajivua nguo
 
Uswahili ni hatari sana. Kwanza kakubali alihusika. Halafu akasema taratibu za manunuzi hazikufuatwa. Alikuwa asilione hilo miaka yote? Porojo tu.Hatubabaishwi na porojo.
 
Mheshimiwa raisi wangu kikwete umeongea kweli ila kwanini umeacha mpaka nikaweka nadhiri kura kwa lowassa
 
Tuondoleen upumbavu wenu hapa. Aliyekuw amkuu wa nchi ni Lowasa au Kikwete? Nani alikuwa juu ya mwingine?

Baada ya kubaini kwamba Lowasa ndiye tatizo, bungeni aliwajibika, serikai ya kikwete ilifanya nini ili kumfikisha kwenye vyombo vya sheria?

Kikwete aache uanafiki. Tabia hizi hatutaki kuziona tena kwenye ikulu yetu.

Kikwete alipaswa kuhakikisha uchunguzi unafanyika na ingebainika Lowasa ana kesi ya kujibu, alitakiwa kufikishwa mahakamani na serikali ili haki kwa taifa itendeke. Alifanya hili?

Kikwete huyu huyu ndiye aliyekwenda kumnadi Lowasa Mondulikwamba ni jembe yaliyomkuta ni ajali ya kisiasa. Alipokuwa nasema haya alikuwa kwenye ulimwengu na mwili gani huyu?

Aliulizwa mhusika wa Richmond akaasema hamjui. Leo huu ujinga anataka kumwambia nani atakayemwondoa yeye kwenye huu ufisadi?

Miaka nana imepita lowaa akisifiwa kila mara na kikwete na chama chake. Hadi anapewa na form za kugombea uraisi. Hii biashara ninadhani inatosha kwa hao watoto wa shule mnaowasomba na malori kujaza viwanja. Watu wazima hapa.

Ninaomba kikwete aishie zake kwa namna anavyostahili. Narudia maneno ya Kingunge. Akitaka kuondoka kistaarabu, akabidhi nchi kwa atakayeshinda. Haya mngine anajifedhehesha na kujimalizia hata kaheshima kake alikosalia nako kama kapo.

Tumechoka. Tunahitaji Tanzania sahihi, siyo hii ya rasi wa ajabu ajabu.

Nakubaliana na wewe mkuu👏
 
Kikwete muda wake umeisha,sidhani kama anaamini hili,umeshauriwa na babu Kingunge ukabidhi madaraka kwa ustarabu
 
Anajua watanzania tulio wengi wapumbafu ndio maana anajaribu kutumia njia hii kuongea kabla watu hawajajua ukweli tayari uchaguzi umeisha. Msidanganyike. Kama unapenda ukawa piga kura ukawa kama unataka ccm then sikiliza

Kama unapende ccm piga kura ccm,kama unaipenda chauma piga kura chauma nk
 
Kikwete aweka wazi kuwa waziri mkuu kipindi hicho ndio muhusika mkuu kwenye Richmond, baraza la mawaziri pamoja na yeye walihusika nawalikubaliana kuwa kuna upungufu wa umeme na mitambo ikanunuliwe lakini hakuhusika kampuni gani ya kwenda kuleta hiyo mitambo .

Alisisitiza sheria za manunuzi zifuatwe lakini waziri mkuu wa wakati huo hakufata na aliunda tume ya manunuzi ya kwake mwenyewe .

Alikuwa wapi siku zote? Anafikiri atabadili mawazo ya wapiga kura kumbe ndiyo anaokoleza chuki dhidi ya mafi ccm
 
Ccm ni kiwanda cha kuunda mafisadi,lowasa ali graduate huko msituchanganye kura zetu ni kwa Lowasaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Kama yeye hakuweza kufikiri kabla ya kuzungumza, washauri wake pia walishindwa kumwambia ukweli kuwa kuzungumza maneno hayo ni kuonyesha udhaifu wake wa kufanya maamuzi sahihi ndani ya wakati sahihi? udhaifu ambao ndo umetufikisha hapa tulipo kwenye mikataba ya kilaghai na umasikini uliotukuka. Alichokifanya leo ni sawa na baba aliyeshindwa kumuadhibu mkewe au mtoto wake na kwenda kulia kwa majirani ili wamuone alikuwa sahihi.
 
Hatudanganyiki atajua yeye huyo Kikwete tushafanya maamuzi na kura ni kwa Lowasa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom