hp4510
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 8,907
- 9,695
Katika pitapita yangu nimekutana na video ya kampeni katika uchaguzi wa mwaka juzi (2015) ambapo aliyekuwa akimaliza muda wake ndugu JK alisema pasipo kumung'unya maneno kwamba mwenye richmond si mwengine ila ni Bwana Lowassa.
Yawezekana kwa wakati ule tulikuwa na mihemuko ya vyama na joto la uchaguzi na kupelekea kwa namna moja ama nyingine watu kutopata wasaa wa kusikia hilo (Binafsi sikupata kusikia hotuba hii hapo kabla). Lakini leo tunaweza jadiliana kwa kina juu ya hili jambo.
Inakuwaje kitengo cha kampeni cha wakati huo cha CHADEMA hawakupata kujibu tuhuma hizo jukwaani kama ambavyo bwana JK alizitoa Jukwaani.? Kwa maana wengi walikuwa wanasuburi ama walidhani Lowassa angejibu ama kutoa maelezo iwapo tuu angeanza kushambuliwa.
CHADEMA wasitake kutuambia kwamba hawakusikia hizo tuhuma, kwani katika ushindani wa wakati ule naamini kabisa ni lazima kulikuwa na mtu/watu mahususi kwa ajili ya kufuatilia yanayofanywa na wapinzani wao (CCM) na isitoshe tuhuma zilitolewa public katika utambulisho wa kumnadi JPM,
Kwa hiyo naamini kabisa viongozi wa juu wa CHADEMA pamoja na Lowassa mwenyewe walisikia kupitia vyombo vya habari. Na pia wasije na hoja kwamba Bw. Lowassa alikuwa akilinda kiapo cha kutotoa siri alichokula wakati akiwa katika baraza la mawaziri, kwani kama ni kulinda kiapo hicho JK angekuwa wa kwanza na wala asingeanza kuyatamka hayo mambo ya Richmond katika jukwaa la kisiasa.
Tena JK hakuishia kutamka tuu, bali alitamka kwa lengo la kuvunja nguvu ya upinzani uliokuwa mbele yao na kujivunia wafuasi toka upande wa pili pamoja na kujipa nguvu upande wao.
Pia CHADEMA msije na majibu ya kuwa kama EL ni mtuhumiwa wa Richmond, basi apelekwe mahakamani ama ashitakiwe. Hii itakuwa si utetezi yakinifu, kwani yawezekana upande wa pili hawaoni sababu ya kumpeleka mahakamani either wanaona kwa kumpeleka mahakamani wataibua madudu yao yaliyojificha ama wameona kwa kumpeleka mahakamani watampa nguvu ya kisisa ama vyovyote vile.
Najua wengi mtakuja kwa kusema nimetumwa na CCM, Kwanza tuu niweke wazi kuwa mimi si mwanachama wa CCM wala CHADEMA (kwa maana sina kadi ya chama chochote kati ya hivyo). Ila tuu nimepata kuwa mkereketwa wa upinzani. So juu ya hili sijatumwa na mtu yeyote yule.
Nimeambatanisha video hiyo, Tuhuma hizo zimeanza kutolewa kuanzia dakika ya 5:10 na kuendelea.
yote hayo ni sawa, swali ni je mbona hakamatwi? Mbona ajafunguliwa kesi? Mbona yupo tu pale masaki?