Kikwete: Lowassa ndiye mhusika wa Richmond

Kikwete: Lowassa ndiye mhusika wa Richmond

Status
Not open for further replies.
Ee Mungu muumba mbingu na nchi iepushe nchi hii na viongozi madodoki.wameifikisha nchi pabaya.sasa tunahitaji mabadiliko ya kweli.tumechoshwa na madodoki.
 
Duuuuh bac huyu jamaa anafaa kuwA Rais km aliweza kufanya mamuz makali kuliko kiongoz wk, so his powerful. Anafaa kuwa Rais na apewe kura tu.
 
na ukweli wa lowassa kutofaa kuwa mkuu wa nchi haubadili ukweli wa ccm kutofaa kuendelea kuwa chama tawala baada ya kushindwa kabisa kutawala kwa zaidi ya nusu karne.

Ukisema lowassa hafai kuwa mkuu wa nchi na ukasema ccm nayo haifai kuendelea kutawala, basi hapo tutakuwa kwenye ukurasa mmoja.

Lakini usije na habari za eti lowassa hafai halafu ccm wanafaa kuendelea kutawala kwa miaka mingine 5!

Nitakuona mwendawazimu!!
well articulated
 
Hivi ufisadi tulionao ni wa Richmond tu? Angalau huu kuna mtu aliwajibika, je mwingine
 
kwa nn hakuchukua hatua tena akamtetea. ina maana hata sasa kuna amaowalinda?
 
CCM haina pumzi ya kupambana na ufisadi.kwa kauli ya kikwete mwanza ni dhahiri ccm haina uwezo hata chembe wa kuondoa matatizo ya wananchi,na pia ni chama kinacholea ufisadi.kwa hali hiyo nazidi kukazia nia yangu ya kumpa Mh LOWASA kura yangu.Kura yangu ni kwa LOWASA.
 
Acha basi kumung'unya maneno.

Jibu hili swali, sawa?

Kwa hiyo kesho wewe unaipigia kura CCM na Magufuli, siyo?

Wote hawafai ....lakini nimeamua kumchagua Magufuli bila kujali matokeo yake kuliko kuwapa nchi wanamtandao waliogombana na Mkuu wa kaya na kuamua kwenda upinzani kutimiza haja zao .....kwasasa naona wagombea zaidi ya vyama ....
 
Lowassa katajwa na Kikwete kuhusika na Richmond, tujuze kama Rais kamtaja pia mhusika wa lumbesa ya Escrow ya Stanbank
 
Mpaka sasa mwana siasa wangu bora ni Lowassa....na kesho lazima nimpe vema.
 
Wote hawafai ....lakini nimeamua kumchagua Magufuli bila kujali matokeo yake kuliko kuwapa nchi wanamtandao waliogombana na Mkuu wa kaya na kuamua kwenda upinzani kutimiza haja zao .....

Wewe hujielewi kabisa!

Huwezi kusema Lowassa na Magufuli wote hawafai halafu ukaamua kumchagua Magufuli.

Kwa nini umpe kura yako mtu ambaye tayari ushakiri kuwa hafai?

Kama kura yako ni 'protest vote' kwa nini usimpe mama Mghwira wa ACT?

Hata ungesema kwamba kwenye urais hutampigia yeyote maana huoni anayefaa na ukasema walau utapiga kura kwenye ubunge na udiwani kwa wapinzani, ungeeleweka vizuri zaidi ya hapa.

Wewe siyo sehemu ya ufumbuzi wa tatizo bali ni sehemu ya mwendelezo wa tatizo.

Na usije hapa kulialia siku huyo utakayempa kura yako atakapoendeleza yale yale ya miaka 54 iliyopita.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Akiongea leo Mwanza kwenye kufunga kampeni za ccm Mh.Jk amesema ni kweli alishiriki kwenye makubaliano ya kutafuta kampuni ya kufua umeme baada ya Mabwawa kukauka nchi, lakini hakushiriki kutafuta kampuni gani ilete umeme, hivyo hahusiki kwa namna yoyote kwa ujio wa Richmond.

Hivyo waziri Mkuu ndio mhusika mkuu wa Richmond!

Mkubwa anadhani atamwinua Maguf kwa kumpaka ENL. Tool late. Kwenye sanduku LA kura Maguf Hana mvuto Kama ENL. Kutoa vitisho Pia hakusaidii.
 
Wewe hujielewi kabisa!

Huwezi kusema Lowassa na Magufuli wote hawafai halafu ukaamua kumchagua Magufuli.

Kwa nini umpe kura yako mtu ambaye tayari ushakiri kuwa hafai?

Kama kura yako ni 'protest vote' kwa nini usimpe mama Mghwira wa ACT?

Wewe siyo sehemu ya ufumbuzi wa tatizo bali ni sehemu ya mwendelezo wa tatizo.

Na usije hapa kulialia siku huyo utakayempa kura yako atakapoendeleza yale yale ya miaka 54 iliyopita.

Mkuu kulalamika kupo hata Lowasa akiwa mkuu wa nchi (God forbid)
 
Mkuu kulalamika kupo hata Lowasa akiwa mkuu wa nchi (God forbid)

Well, sawa, kulalamika kupo.

Lakini kwa nini uwe mwendelezo wa tatizo kuliko kuwa sehemu ya ufumbuzi wa tatizo?

Kwani ni lazima umpigie kura huyo Magufuli?

Kwa nini usipige kura ya 'protest vote' na kumpigia yule mama wa ACT?

Au kwa nini usipige kabisa kura ya urais lakini ukapiga kura za mbunge na diwani?

What the hell is wrong with you? Ni lazima kumpigia huyo Magufuli?

Shame on you and your ilk. Instead of being part of the solution you are part of the problem.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Magufuli baba,ukiingia ikulu piga lowasa ndani,maana huyu jk anamkingia kifua swaiba wake sana.
 
anatafuta huruma ya wapiga kura leo, mwambieni amechelewa sana hatotuweza kurudi misri
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom