Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,329
- 33,139
Kwa maelezo yako Hao askari wawili hawakumuuwa huyo Jenerali kombe kwa Makusudi kama ni hivyo Rais J.K . Ana haki ya kuwaachia huru ingawa Mahakama kuu ilitoa Adhabu ya kifo. Je Tuangalie Sheria yetu inasemaje je mtu akiuwa kwa bahati mbaya anaweza kuhukumiwa Adhabu ya Kifo? Na hata kama atahukumiwa na Mahakama Kuu adhabu ya kifo mwamuzi wa mwisho ni Rais ,Rais akitia saini ndipo anaweza huyo mtu kuuwawa Natanguliza hivyo asanteni...Rais Jakaya Kikwete amewaachia huru askari polisi wawili Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo mwaka 1998 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi Mkurugenzi wa zamani wa Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe. Wamekuwa gerezani takriban kwa miaka 16, wamechiwa huru kwa huruma ya Rais ambaye alipunguza adhabu hiyo ya kifo, kuwa kifungo cha miaka miwili jela.
Kombe aliuawa kwa kupigwa risasi nne kifuani Juni 30, 1996 baada ya polisi waliokuwa wakisaka gari aina ya Nissan Patrol mali ya W. Ladwa, kumfananisha na mtuhumiwa sugu wa wizi wa magari.
::Mwananchi::
Ulijuaje walimwuua kwa bahati mbaya? Unawezaje kumpiga risasi "mhalifu au mtuhumiwa" ambaye kishaweka juu mikono yake? It was cold blooded murder ordered by someone. Otherwise kwa nini wapewe msamaha sasa na hela za kuanzishia biashara?Kwa maelezo yako Hao askari wawili hawakumuuwa huyo Jenerali kombe kwa Makusudi kama ni hivyo Rais J.K . Ana haki ya kuwaachia huru ingawa Mahakama kuu ilitoa Adhabu ya kifo. Je Tuangalie Sheria yetu inasemaje je mtu akiuwa kwa bahati mbaya anaweza kuhukumiwa Adhabu ya Kifo? Na hata kama atahukumiwa na Mahakama Kuu adhabu ya kifo mwamuzi wa mwisho ni Rais ,Rais akitia saini ndipo anaweza huyo mtu kuuwawa Natanguliza hivyo asanteni...
Awezi JK kwa sababu shida ni kwamba BABu Seya amekula na demu wake ndio nooma yote hiyo. Ukweli ndio hiyo na upo wazi ssa nauliza yeye JK atakua na wanawake wagapi ?? Mbona Rais mzima anatotia aibu ??? Malaya kama mbuzi Shame unto him. Afai kwa rais kabisa. Kwa nini tusiingie barabarani kupinga atolewe IKULU.... Tunasubiri lini jamani
R.I.P kombe, wauaji wako wapo mtaani.
Ndugu! Hoja hapa si kwamba kifo cha kombe kiliumiza ama la. Hoja iliyopo hapa ni kuwa je, katiba inampa rais uwezo wa kusamehe? Kama ukisoma ibar ya 45 wala huwez kuwa na jazba za ajabu. Kifo chake kilituumiza ndiyo, lakini na katiba yetu ndo imempa uwezo rais.
Wakati mwingine haya mambo yangekuwa yanawekwa wazi umma usingekuwa unawatwisha lawama mtu ingekuwa inajenga baada ya kubomoa.Ni vyema kuwa dunia tunayokwenda kutakuwa na siri za maana na siri zisizo na msingi zitakuwa hazina nafasi.Dunia tunnayokwenda ni dunia ambayo mwasisis wake Nelson Mandera ameianzisha ya ukweli [Trutha and reconciliation].Haya mabo ya babu Sya wakati mwingine yeye na familia yake kukaa ndani ni salama yake zaidi kuliko kuwepo huku nje.
Hiyo si kweli kabisaaaaaaaaaaa ni uwongo uliotukuka.
Hoa polisi walihukumiwa kunyongwa sio kifungo cha maisha na rais hakusaini hukmu hiyo hivyo wamekaa gerezani kwa zaidi ya miaka 16 na kama wameachiwa basi watakuwa wamemaliza kifungo chao.
Hiyo ni kama alivyoachiwa mama Liundi au Asha mkwizu baada ya rais kukataa kusaini adhabu zao za kifo.
usimsingizie JK bureeeeee. Mkapa ndio wa kulaumiwa kwa kukataa kusaini hukmu hiyo.
Nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri. Si kila kitu ni siasa, mengine ni sheria zaidi. Ni bora usichangie kuliko kuchangia pumba. Hapa mzembe si Jk bali ni wewe nngu007. Katiba inampa uwezo rais kufuta au kupunguza adhabu yoyote. Rudi darasani!!!
Kama wasema Mkapa hakusaini karatasi hiyo na hukumu ilisha pita JK alikuwa na mamlaka gani ya kuingilia hukumu iliyo pita na kuwa toa? kama wewe wakataa sisi tusimlaumu kwanini asiache nayeye kuingilia jambo hilo. Maana kama JK ame sign watoke basi wamekinzana na hukumu ya mahakama kumbuka mwenzio alipo kuwa kwenye urais haku sign wewe umekuja ukasign watoke mbona hapo mwatukanganya zaidi.
My Take;
Jk ni wakulaumiwa tuuu period
Jamani hii inazidi ku-strength argument ya kuwa na katiba mpya. Haiwezekani muuaji anahukumia kunyongwa,
Rais badala ya kusaini hati ya kunyonga anampunguzia adhabu ya kifo kuwa kifungo cha miaka miwili? Uko wapi
hapa uhuru wa mahakama. Katiba mpya lazima ieleze makosa ambayo rais anaweza kusamehe na yale ambayo
hawezi kusamehe.
Huko Marekani Rais Obama hawezi kabisa kumsamehe mtu aliyehukumiwa kunyongwa. Tatizo letu katiba yetu imempa
madaraka makubwa rais na tunapopata rais kihiyo kama JK ndiyo tunaona ubovu wa katiba. From kifo to two years
imprisonment. Anything is possible in Tanzania. Sasa kwanini watanzania tusiamini kwamba kweli aliuwawa na serikali na CCM?!
@barubaru
vipi kazi ya kumuondoa gadaffi mmekamilisha? ukimaliza utaenda syria? huku kwetu pia kazi zako za kijasusi zinahitajika
JK kaichoka ccm,
anaamua kufanya vituko makusudi ili watanzania muiondoshe ccm madarakani lakini hamtaki,
ni msaada gani mnaoutaka kutoka kwa JK zaidi ya haya madudu anayoyafanya?
au mnataka aseme wazi kuwa ccm haifai kuongoza nchi?
Kati ya JK na watanzania anaowaongoza nani mjinga hapa sasa?