Kikwete awaachia huru Polisi waliomuua Jenerali Kombe

Hata hiyo hukumu yao ilikuwa kutuzuga tu wale walikuwa wamepata hifadhi tu kwani walikuwa wanatekeleza amri ya wakubwa. Yule Mmeto toka Msumbiji ana mkono katika mauji ya Gen. Kombe.

Kikwete elewa kuwa Mkapa alihusika na hao askari walikuwa wanatekeleza amri ya Mpaka na pia Mrema wa Tlp anajua kila kitu.ELEWENI ATAKAYE UA KWA UPANGA ATAUAWA KWA UPANGA.
 
Jamani hii inazidi ku-strength argument ya kuwa na katiba mpya. Haiwezekani muuaji anahukumia kunyongwa,
Rais badala ya kusaini hati ya kunyonga anampunguzia adhabu ya kifo kuwa kifungo cha miaka miwili? Uko wapi
hapa uhuru wa mahakama. Katiba mpya lazima ieleze makosa ambayo rais anaweza kusamehe na yale ambayo
hawezi kusamehe.

Huko Marekani Rais Obama hawezi kabisa kumsamehe mtu aliyehukumiwa kunyongwa. Tatizo letu katiba yetu imempa
madaraka makubwa rais na tunapopata rais kihiyo kama JK ndiyo tunaona ubovu wa katiba. From kifo to two years
imprisonment. Anything is possible in Tanzania. Sasa kwanini watanzania tusiamini kwamba kweli aliuwawa na serikali na CCM?!
 
Tafadhali JK Babu seya wala hakumuua mtu na yeye mfikirie umpunguzie adhabu.
 
hawa waliua kwa kukusudia..sasa wamewatumikia maboss wao waliowatuma kumtoa roho Kombe wa watu...nasikitikia tu familia ya marehemu Kombe sijui wanajisikiaje sasa hivi baada ya kupata habari hizi. mtu aliyelitumikia taifa anauliwa kizembe au kwa sababu za maslahi ya watu wengine na wauaji wake wanatoka jela ahhh! ningeua
 
Soma ibara ya 15 (1) (c) madaraka ya rais kwenye misamaha ya wafungwa...president amnesty.
Ni vizuri ukatuwekea kifungu hicho cha katiba ambacho kinampa Rais madaraka ya kutengua hukumu za mahakama. Hivi kama anaweza kutengua hukumu za mahakama, je uhuru wa mahakama upo wapi? Je, kweli huu ni muhimili wa tatu wa dola au ni mkono wa dola? Si ajabu JK analipiza kisasi kwa marehemu Kombe baada ya kugongana huko jeshini enzi zile!!!!!!!!
 
sasa kama hao waliua na ikathibitika na hukumu ikatolewa waachiwa huru. Kwanini na akina Babu Seya nao wasiachiwe huru tu mana hii nchi ishakuwa corrupt. nyambaf
 
Kama kuna zaidi ya watu 500 wanasubiri kunyongwa kwanini waachiwe hao wawili.
Hapa naanza kujiuliza WHAT NEXT?PLOTTING ANOTHER SCENE?............
Maswali ni mengi sana.
 
Nimekuwa nikipitia magazeti ya leo nikakutana na habari kuwa wale askari wawili waliohukumiwa kifo na mahakama kwa kosa la kumuua Kombe wameachiwa huru baada ya huruma ya rais Kikwete kubatilisha hukumu hiyo kuwa miaka miwili,nikajiuliuza kwa nn rais asiitumie huruma hii Babu Seya na wanae?.Kuna nn kwenye hukumu hii ya babu Seya?.Watu waliwahi kusema kuwa kuna mkono wa fulani hapa,msitake niamini hivyo.Na hii ya Kombe nayo!.

hukumu ya askari hao inasema waliua kwa uzembe sio makusudi pengine ndio kigezo cha huruma ya rais na nafasi yao ya kwamba walikuwa kazini kwa niaba ya jamhuri na wakazembea na kuua lakini babu sea na watoto wake hawakubaka kwa bahati mbaya bali kwa dhamira. Nafikiri huruma pia inazingatia namna kosa lilivyofanyika.
 
Kikwete elewa kuwa Mkapa alihusika na hao askari walikuwa wanatekeleza amri ya Mpaka na pia Mrema wa Tlp anajua kila kitu.ELEWENI ATAKAYE UA KWA UPANGA ATAUAWA KWA UPANGA.

Hapa nafikiri kuna makubaliano kati ya Mkapa na JK, Mkapa alikubali kwenda Igunga kuisaidia CCM kwa makubaliano kuwa wale vijana wake waliomfanyia kazi chafu ya Kumkolimba Kombe waachiwe, na JK kwa kuheshimu makubaliano hayo kawaachia huru.
 
Soma ibara ya 15 (1) (c) madaraka ya rais kwenye misamaha ya wafungwa...president amnesty.

Jamani, mbona mnalishana sumu? Kwanza hakiitwi KIFUNGU(SECT), bali inaitwa ibara(article). Nayo ni 45(1)(a-d) na wala siyo ibara ya 15 kama mnavyotaka kuwaaminisha watu.
 
Nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri. Si kila kitu ni siasa, mengine ni sheria zaidi. Ni bora usichangie kuliko kuchangia pumba. Hapa mzembe si Jk bali ni wewe nngu007. Katiba inampa uwezo rais kufuta au kupunguza adhabu yoyote. Rudi darasani!!!

Naunga mkono hoja. Alikuwa na uwezo kikatiba ya kusema wafungwe mwezi mmoja. Si yeye ni katiba ambayo ndiyo sheria mama.
 
You idiot allow free opinions here! One has the right to ask the situation and feelings of the relatives of the diseased. spare of your stupidity pro JK syndrome. The man was killed near my own home with eye witness when he raised his hands up as a sign of peace! damn it the sent bandits pumped some 4 bullets into his chest.

Ndugu! Hoja hapa si kwamba kifo cha kombe kiliumiza ama la. Hoja iliyopo hapa ni kuwa je, katiba inampa rais uwezo wa kusamehe? Kama ukisoma ibar ya 45 wala huwez kuwa na jazba za ajabu. Kifo chake kilituumiza ndiyo, lakini na katiba yetu ndo imempa uwezo rais.
 
Soma ibara ya 15 (1) (c) madaraka ya rais kwenye misamaha ya wafungwa...president amnesty.

Jamani, mbona mnalishana sumu? Kwanza hakiitwi KIFUNGU(SECT), bali inaitwa ibara(article). Nayo ni 45(1)(a-d) na wala siyo ibara ya 15 kama mnavyotaka kuwaaminisha watu.
 
Rais Jakaya Kikwete amewaachia huru askari polisi wawili Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo mwaka 1998 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi Mkurugenzi wa zamani wa Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe. Wamekuwa gerezani takriban kwa miaka 16, wamechiwa huru kwa huruma ya Rais ambaye alipunguza adhabu hiyo ya kifo, kuwa kifungo cha miaka miwili jela.

Kombe aliuawa kwa kupigwa risasi nne kifuani Juni 30, 1996 baada ya polisi waliokuwa wakisaka gari aina ya Nissan Patrol mali ya W. Ladwa, kumfananisha na mtuhumiwa sugu wa wizi wa magari.

::Mwananchi::

haya mambo ndio naamuaga kujiachia MK Sport na MMU..
 
Kama tz ingekua na viongozi makini hao jamaa ndio prime suspects na wana siri kubwa dhidi ya mauaji ya kombe walipewa order kutoka juu. Na pia walitafutiwa mawakili wa kuwatetea. Is the same story kama walivyofanya kwa sokoine. CCM walimuua kombe kwa sababu zao. Na kikwete anaujua ukweli.
 
Nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri. Si kila kitu ni siasa, mengine ni sheria zaidi. Ni bora usichangie kuliko kuchangia pumba. Hapa mzembe si Jk bali ni wewe nngu007. Katiba inampa uwezo rais kufuta au kupunguza adhabu yoyote. Rudi darasani!!!

Nawe huna maana. Mweleweshe mwenzako sio kutukana. Kwa namna hiyo hutamjenga mwenzio mtaishia kutukanana. Uwe mwalimu mwema!!!!
 
Back
Top Bottom