Kikwete awaachia huru Polisi waliomuua Jenerali Kombe

Babu Seya na Mwanae hawajahukumiwa kifo. Hao waliua na walihukumiwa kifo. Wakina babu seya hawastahili huruma hiyo hiyo?

Mimi nadhani hapo ndio angepata support kuwa toka kwa wananchi, hao wauaji kawaachia, wale na kesi za kusingiziwa kawaacha, labda kwa kuwa tuhuma za bau seya zinamuhusu
 
Matakwa ya Katiba
Madaraka ya Rais ya kumsamehe mtu yeyote aliyepatikana na hatia, yamo katika Ibara ya 15 (1) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2005.

Nadhani watu wanataka kuona busara inatumika wakati mamlaka haya ya rais yanapotumika. Kwa maoni yangu naona Rais kupunguza adhabu ya kifo hadi miaka 2, ni kuwa kashauriwa kuwa wale ni kivuli cha " WAUAJI" na kuwanyonga ni kuwaonea anayetakiwa kunyongwa ni serikali! Hivi kama kweli wale watu waliua kwa makusudi, Rais anatumia busara gani kuwaonea huruma ya kupunguza adhabu ya kifo hadi miaka 2? Bwana KAUMZA, issue si kuwa mamlaka ya kikatiba, issue ni busara gani unaitumia ku exercise prerogative mercy
Nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri. Si kila kitu ni siasa, mengine ni sheria zaidi. Ni bora usichangie kuliko kuchangia pumba. Hapa mzembe si Jk bali ni wewe nngu007. Katiba inampa uwezo rais kufuta au kupunguza adhabu yoyote. Rudi darasani!!!
 
Adhabu ya kifo ikitolewa haifanyiki mpaka raisi aweke sahihi yake. Mimi binafsi sioni tatizo la raisi kuwasamehe. Watuhumiwa walikuwa kazini na inawezekana kuwa kweli kabisa walimfananisha. Halafu kitu kingine, kutoa uhai wa mtu hata kama ni muuaji inataka moyo!!! Mbona raisi aliyemtangulia pia hakuwahi kusaini adhabu ya kifo!!! Kwa hili mnamwonea.
Hivi Rais anaweza kubatilisha hukumu ya mahakama kuu jamani? Na rufaa kazi yake ni nini? Hapa nina wasiwasi na kusiginwa katiba. Huyu jamaa ni 'janga la kitaifa'!!!!!!!!
 
45. Uwezo wa kutoa msamaha Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 9
(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, Rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo–
(a) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, na aweza kutoa msamaha huo ama bila ya masharti au kwa masharti, kwa mujibu wa sheria;
(b) kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu yeyote aliyehukumiwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au asitimize adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum;
(c) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu;
(d) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu ya kutoza, au kuhozi (au kuchukua) kitu cha mtu mwenye hatia ambacho vinginevyo kingechukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka utaratibu utakaofuatwa na Rais katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa ibara hii.
(3) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa watu waliohukumiwa na kuadhibiwa Tanzania Zanzibar na kwa adhabu zilizotolewa Tanzania Zanzibar kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge inayotumika Tanzania Zanzibar, hali kadhalika, masharti hayo yatatumika kwa watu waliohukumiwa na kuadhibiwa Tanzania Bara kwa mujibu wa sheria.

Katiba inampa sana madaraka hayo na ana uwezo wa kusamehe adhabu yoyote au kuipunguza au kuzuia hata utozaji wa faini
Ila duh kwa adhabu ya kifo kupunguzwa mpaka miaka miwili then watu wanaachiliwa
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Jamani, mkulu kawaachia polisi walio muuwa Kombe. Polisi hao walikuwa wamefungwa kifungo cha maisha, lakini walipunguziwa adhabu hadi miaka miwili.
 
swala la kufananishwa Kombe halipo kabisa kwa sababu marehemu Kombe alikuwa mweusi ti kwa sura na mnene na huyo jambazi wanaedai alefananishwa nae alikuwa mweupe pe yani ule wa njano,halafu pia mwaka huo wa 1996 pale Moshi ni yeye tu alikuwa na nissan patrol na alikuwa anafahamika sana so hilo la kufananishwa haliingii vichwani kwa sisi tuliowfahamu watu hao
 
Matakwa ya Katiba
Madaraka ya Rais ya kumsamehe mtu yeyote aliyepatikana na hatia, yamo katika Ibara ya 15 (1) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2005.

Nadhani watu wanataka kuona busara inatumika wakati mamlaka haya ya rais yanapotumika. Kwa maoni yangu naona Rais kupunguza adhabu ya kifo hadi miaka 2, ni kuwa kashauriwa kuwa wale ni kivuli cha " WAUAJI" na kuwanyonga ni kuwaonea anayetakiwa kunyongwa ni serikali! Hivi kama kweli wale watu waliua kwa makusudi, Rais anatumia busara gani kuwaonea huruma ya kupunguza adhabu ya kifo hadi miaka 2? Bwana KAUMZA, issue si kuwa mamlaka ya kikatiba, issue ni busara gani unaitumia ku exercise prerogative mercy

Ndugu zangu, muwe mnasoma vingnevyo mtakuwa mna-argue kama watu wa vijiweni. Rais ana mamlaka hayo chini ya ibara ya 45(1)(a-d) na siyo ibara ya 15(1)(c) kama mnavyotaka kuwaaminisha watu. Kuhusu busara gani imetumika, hiyo hakuna mtu anayeweza kumsemea rais. Yeye mwenyewe ndo anaejua. Hata angemwachia Babu sewa, wapo watu wangehoji busara gani imetumika!! Kifupi ni kuwa, mamlaka anayo kikatiba na ameyatumia. Ombi langu. Someni. Ushabiki wa vijiweni acheni. Kwenye siasa tuongee siasa, na kwenye utaalamu tuongee kitaalamu. Otherwise, tutashusha hadhi ya Jf
 
Jamani, mkulu kawaachia polisi walio muuwa Kombe. Polisi hao walikuwa wamefungwa kifungo cha maisha, lakini walipunguziwa adhabu hadi miaka miwili.

Hiyo si kweli kabisaaaaaaaaaaa ni uwongo uliotukuka.

Hoa polisi walihukumiwa kunyongwa sio kifungo cha maisha na rais hakusaini hukmu hiyo hivyo wamekaa gerezani kwa zaidi ya miaka 16 na kama wameachiwa basi watakuwa wamemaliza kifungo chao.

Hiyo ni kama alivyoachiwa mama Liundi au Asha mkwizu baada ya rais kukataa kusaini adhabu zao za kifo.

usimsingizie JK bureeeeee. Mkapa ndio wa kulaumiwa kwa kukataa kusaini hukmu hiyo.
 
Sioni mahali kwenye katiba panaposema kuhusu hukumu ya kifo kuwa msamaha.. Nimeuliza mwanasheria mzuri tu hapa Tanzania anasema mara nyingi hukumu ya kifo kutolewa adhabu ya kifungo cha maisha ... Sasa ****** yeye katoa adhabu ya miaka miwili.

Ila nimejifunza jambo hapa.. Unapotekeleza amri ya mafisadi wao wao ndiyo watakaokulinda..
 
Matakwa ya Katiba
Madaraka ya Rais ya kumsamehe mtu yeyote aliyepatikana na hatia, yamo katika Ibara ya 15 (1) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2005.

Nadhani watu wanataka kuona busara inatumika wakati mamlaka haya ya rais yanapotumika. Kwa maoni yangu naona Rais kupunguza adhabu ya kifo hadi miaka 2, ni kuwa kashauriwa kuwa wale ni kivuli cha " WAUAJI" na kuwanyonga ni kuwaonea anayetakiwa kunyongwa ni serikali! Hivi kama kweli wale watu waliua kwa makusudi, Rais anatumia busara gani kuwaonea huruma ya kupunguza adhabu ya kifo hadi miaka 2? Bwana KAUMZA, issue si kuwa mamlaka ya kikatiba, issue ni busara gani unaitumia ku exercise prerogative mercy

Kabla kunena haya yote jaribu kukumbuka ni lini watu hawa walihukumiwa na Kikwete aliingia lini madarakani?

Kifupi hawa watu walihukumiwa kifo wakti wa Mkapa akiwa katika awamu yake ya kwanza tena mwanzoni kabisa. sasa kikwete huyo atapunguzaje adhabu hii na kuifanya miaka miwili wakati mkapa alitawala kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano na Kikwete asa amesha maliza muhula mmoja yaani miaka mitano.

Nafikiri ni vizuri kujua wame achiwa lini? na hukumu yao ya kifo ilitolewa lini, Kisha mtajuwa uwongo uliotukuka wa mtoa mada.
 
Nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri. Si kila kitu ni siasa, mengine ni sheria zaidi. Ni bora usichangie kuliko kuchangia pumba. Hapa mzembe si Jk bali ni wewe nngu007. Katiba inampa uwezo rais kufuta au kupunguza adhabu yoyote. Rudi darasani!!!
You idiot allow free opinions here! One has the right to ask the situation and feelings of the relatives of the diseased. spare of your stupidity pro JK syndrome. The man was killed near my own home with eye witness when he raised his hands up as a sign of peace! damn it the sent bandits pumped some 4 bullets into his chest.
 
Sioni mahali kwenye katiba panaposema kuhusu hukumu ya kifo kuwa msamaha.. Nimeuliza mwanasheria mzuri tu hapa Tanzania anasema mara nyingi hukumu ya kifo kutolewa adhabu ya kifungo cha maisha ... Sasa ****** yeye katoa adhabu ya miaka miwili.

Ila nimejifunza jambo hapa.. Unapotekeleza amri ya mafisadi wao wao ndiyo watakaokulinda..

Huyo mwanasheria unayedai mzuri basi amekutumbukiza kwenye shimoni kabisaaaaa. Hukumu ya kifo ni tofauti na hukumu ya maisha. Na hata siku moja hakumu ya kifo haiwezi kugeuka kuwa hukumu maisha pasi na mahakama kubadilisha kama kuna rufaa iliyokatwa.

Kwa mujibu wa sharia za huko Tanzania hukmu ya kifo inatekelezeka pale ambapo Rais wa JMTz atakapo saini hukmu hiyo na kuweza kutekelezeka. Na kama rais hatakuwa hajasaini basi utaendelea tu kukaa gerezani mpaka hapo wakubwa watakapopenda ima kukuweka katika majina ya msamaa wa rais au mara nyingi unakaa miaka 16 mpaka 18 kisha unaachiwa (sina uhakika sana wa miaka hii) lakini nita uliza huko Tz.

Wa Tz punguzeni siasa katika sheria.
 
Mpuuzi ni mpuuzi tu..sasa huyu jamaa ni mpuuzi ni jambazi,muuaji pia jizi..unategemea nini kwenye maamuzi yake kama sio UKUDA..!
 
Back
Top Bottom