Kikwete awaachia huru Polisi waliomuua Jenerali Kombe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete awaachia huru Polisi waliomuua Jenerali Kombe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Oct 12, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Rais Jakaya Kikwete amewaachia huru askari polisi wawili Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo mwaka 1998 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi Mkurugenzi wa zamani wa Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe. Wamekuwa gerezani takriban kwa miaka 16, wamechiwa huru kwa huruma ya Rais ambaye alipunguza adhabu hiyo ya kifo, kuwa kifungo cha miaka miwili jela.

  Kombe aliuawa kwa kupigwa risasi nne kifuani Juni 30, 1996 baada ya polisi waliokuwa wakisaka gari aina ya Nissan Patrol mali ya W. Ladwa, kumfananisha na mtuhumiwa sugu wa wizi wa magari.

  ::Mwananchi::
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Wanasheria tunaomba muongozo.....nimewahi sikia kuwa kutoka adhabu kifo haiwezi kupungua zaidi ya maisha gerezani na si vinginevyo!!yaani huwezi kupata msamaha na kupata labda miaka kadhaa jela kama inavyosomeka hapo juu
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Tuesday, 11 October 2011 20:45

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]WALIHUKUMIWA KUNYONGWA NA MAHAKAMA KUU, RUFAA

  Daniel Mjema, Moshi

  ASKARI Polisi wawili waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo mwaka 1998 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi Mkurugenzi wa zamani wa Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe wameachiwa huru.Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku, ambao wamekuwa gerezani takriban kwa miaka 16, wamechiwa huru kwa huruma ya Rais Jakaya Kikwete ambaye alipunguza adhabu hiyo ya kifo, kuwa kifungo cha miaka miwili jela.

  Kombe aliuawa kwa kupigwa risasi nne kifuani Juni 30, 1996 baada ya polisi waliokuwa wakisaka gari aina ya Nissan Patrol mali ya W. Ladwa, kumfananisha na mtuhumiwa sugu wa wizi wa magari.

  Akizungumza na Mwananchi jana, Matiku alisema walitoka gerezani Mei mwaka huu walikokuwa wakisubiri kutekelezwa kwa adhabu yao ya kunyongwa, kabla ya Rais Kikwete kuwaonea huruma na kuwapunguzia adhabu.

  “Unajua baada ya jaji kutuhukumu kunyongwa tulikata rufaa, Mahakama ya Rufani ambayo iliona ile hukumu ilikuwa ni sahihi ikasema tuendelee nayo hadi tulipoomba huruma ya Mheshimiwa Rais,” alisema Matiku na kuongeza:

  “Jopo lililomshauri Rais lilipendekeza tupunguziwe adhabu kutoka kunyongwa hadi kifungo cha miaka miwili na kwa kuwa tulikuwa mahabusu tangu 1998, kifungo hicho kilitosha.”

  Alipoulizwa wanachofanya sasa yeye na mwenzake Mswa, Matiku alisema anajishughulisha na shughuli za kilimo wakati mwenzake anajishughulisha na biashara.

  Maisha gerezani
  Konstebo Matiku aliliambia alisema katika miaka yote 16 aliyokuwa gerezani (1996 – 2011), aliishi katika magereza matatu tofauti, Karanga, Kilimanjaro; Maweni, Tanga na Ukonga, Dar es Salaam.

  “Kwanza tulikaa Karanga kwa miaka miwili hadi tulipohukumiwa na Mahakama Kuu mwaka 1998, tukahamishiwa Gereza la Maweni kwenda kusubiri kunyongwa, lakini mwaka 1999 mimi nilianza kuumwa hivyo nikahamishiwa Ukonga ili niweze kupata matibabu,” alisema Matiku.Alisema kuanzia wakati huo alitengana na mwenzake, Mswa hadi walipoachiwa kwa huruma ya Rais Mei mwaka huu.

  Alisema katika kesi hiyo walikuwa washtakiwa sita wakiwamo askari polisi watano na raia mmoja. Alidai kwamba raia huyo aliyekuwa akiitwa Ismail Katembo alifariki dunia akiwa gerezani mwaka 1997, huku askari wengine wakiachiwa huru na Mahakama Kuu baada ya kutopatikana na hatia.

  Matiku alisema katika kesi hiyo walikuwa wakitetewa na mawakili watatu tofauti na kwamba wakili wake anamkumbuka kwa jina moja tu la Sande... “Alikuwa akiitwa Sande, lakini kwa bahati mbaya mimi sina mawasiliano naye hadi sasa, wale wengine walioachiwa walikuwa wakitetewa na Profesa Msenga na huyu Mswa alikuwa akitetewa na wakili mmoja hivi ni profesa naye lakini jina lake limenitoka.”

  Matakwa ya Katiba
  Madaraka ya Rais ya kumsamehe mtu yeyote aliyepatikana na hatia, yamo katika Ibara ya 15 (1) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2005.

  Ibara hiyo inatamka “Bila kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Ibara hii, Rais anaweza kutenda lolote ikiwamo kuibadilisha adhabu yeyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote ili iwe adhabu tahafifu.”

  Kisheria, huruma hiyo ya Rais inatambulika kama 'Presidential Amnesty' wakati madaraka hayo ya Rais yakifahamika kama 'Prerogative Mercy' na hata Rais mstaafu Benjamin Mkapa aliwahi kuitumia wakati wa utawala wake.

  Madai ya familia
  Baada ya polisi hao kupatikana na kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kile Jaji Buxton Chipeta alichosema: “Uzembe wa hali ya juu”, mjane wa Kombe, Roselyne Kombe alifungua kesi ya madai dhidi ya Serikali.

  Mjane huyo na watoto wa marehemu, walifungua kesi Mahakama Kuu wakiidai Serikali fidia ya Sh690 milioni kwa msingi kuwa kifo cha Kombe kiliifanya miradi iliyoanzishwa na marehemu kupoteza mwelekeo na kufa.

  Oktoba 4, 2001, Jaji Lawrence Mchome ambaye sasa amestaafu, aliiona Serikali kuwa inawajibika kuilipa familia hiyo fidia kutokana na vitendo vya watumishi wake hao wawili lakini ikaiamuru ilipe fidia ya Sh300 milioni.

  Hata hivyo, Serikali haikuridhika na hukumu hiyo na ilikata rufaa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambayo kimsingi nayo iliafiki Serikali kulipa fidia isipokuwa ilipunguza kiwango cha fidia hadi kufikia Sh200 milioni.

  Adhabu ya kifo
  Hatua ya Rais kuwapunguzia adhabu polisi hao imekuja katika kipindi ambacho wanaharakati wa haki za binadamu wakipaza sauti kutaka adhabu ya kifo ifutwe na badala yake iwe kifungo cha maisha.

  Tangu Rais Kikwete aingie madarakani 2005, hajawahi kusaini hukumu yoyote ya kifo kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Benjamin Mkapa na hadi sasa zaidi ya watu 500 wanasubiri kunyongwa.

  Kwa mujibu wa hotuba ya aliyekuwa msemaji wa kambi ya upinzani bungeni, Fatma Maghimbi (CUF), mwaka 2008, Mkapa alibadilisha hukumu za watu 100 waliohukumiwa kunyongwa na kupewa adhabu mbadala.

  Maghimbi ambaye sasa ni mwanachama wa CCM, alisema Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ndiye pekee aliyesaini utekelezwaji wa hukumu ya kifo kwa watu 21 ambao walinyongwa mwaka 1994.

  Adhabu ya kifo ni kati ya zile sheria 40 ambazo Tume ya Marekebisho ya Sheria chini ya, hayati Jaji Francis Nyalali ilipendekeza zifutwe, kwa kuwa haimsaidii aliyeua, aliyeuliwa wala Serikali kuzuia kosa kama hilo kutokea.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Uzembe wa Rais wetu sasa hata wanaohukumiwa kifo wanaachiwa huru... Kweli wanajisikiaje.... is that their political statments???
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  dah! this is hillarious! adhabu ya kifo hadi miaka miwili? credibility ya mahakama iko wapi hapo sasa,hata kama ni clemency? na ilipendekezwa badala ya kifo iwe kufungwa maisha!!
   
 6. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hapo ndipo umuhimu wa kuwa na Judiciary unakosekana.

  Nani ametoa ushauri wa kijinga hivyo? Au ni hasira ya kulipishwa fidia?
   
 7. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri. Si kila kitu ni siasa, mengine ni sheria zaidi. Ni bora usichangie kuliko kuchangia pumba. Hapa mzembe si Jk bali ni wewe nngu007. Katiba inampa uwezo rais kufuta au kupunguza adhabu yoyote. Rudi darasani!!!
   
 8. HGYTXK

  HGYTXK Senior Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nimekuwa nikipitia magazeti ya leo nikakutana na habari kuwa wale askari wawili waliohukumiwa kifo na mahakama kwa kosa la kumuua Kombe wameachiwa huru baada ya huruma ya rais Kikwete kubatilisha hukumu hiyo kuwa miaka miwili,nikajiuliuza kwa nn rais asiitumie huruma hii Babu Seya na wanae?.Kuna nn kwenye hukumu hii ya babu Seya?.Watu waliwahi kusema kuwa kuna mkono wa fulani hapa,msitake niamini hivyo.Na hii ya Kombe nayo!.
   
 9. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ni suala la Muda tu mkuu..na lisemwalo lipo..
  Wajitahidi kuvumilia pengine Msamaha wa Dr Slaa hapo Nov,2015 Utawatoa gerezani...
  Miss you Babu Seya...
   
 10. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Kwani walikuwa hawajanyongwa tu miaka kumi na sita imepita oi! huu nao ni uzembe wa uwajibikaji au?
   
 11. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,577
  Likes Received: 846
  Trophy Points: 280
  ni ile issue ya msamaha wa raisi? Kwani kesi ya mauaji ina msamaha? Ni mara kwanza nasikia hii!
   
 12. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hivi Rais anaweza kubatilisha hukumu ya mahakama kuu jamani? Na rufaa kazi yake ni nini? Hapa nina wasiwasi na kusiginwa katiba. Huyu jamaa ni 'janga la kitaifa'!!!!!!!!
   
 13. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ndg zanguni huyu rais nec ni janga kwa Watanzania wengi.
   
 14. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri ukatuwekea kifungu hicho cha katiba ambacho kinampa Rais madaraka ya kutengua hukumu za mahakama. Hivi kama anaweza kutengua hukumu za mahakama, je uhuru wa mahakama upo wapi? Je, kweli huu ni muhimili wa tatu wa dola au ni mkono wa dola? Si ajabu JK analipiza kisasi kwa marehemu Kombe baada ya kugongana huko jeshini enzi zile!!!!!!!!
   
 15. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #15
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Babu Seya na Mwanae hawajahukumiwa kifo. Hao waliua na walihukumiwa kifo. Wakina babu seya hawastahili huruma hiyo hiyo?
   
 16. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145

  Wakati mwingine haya mambo yangekuwa yanawekwa wazi umma usingekuwa unawatwisha lawama mtu ingekuwa inajenga baada ya kubomoa.Ni vyema kuwa dunia tunayokwenda kutakuwa na siri za maana na siri zisizo na msingi zitakuwa hazina nafasi.Dunia tunnayokwenda ni dunia ambayo mwasisis wake Nelson Mandera ameianzisha ya ukweli [Trutha and reconciliation].Haya mabo ya babu Sya wakati mwingine yeye na familia yake kukaa ndani ni salama yake zaidi kuliko kuwepo huku nje.
   
 17. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,148
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  nazidi kusisitiza uozo wa jk tutaukumbuka milele..
   
 18. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hapa ndipo ule utata wa kifo chake utapoonekana kuwa ni kweli.
   
 19. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kwa hilo sasa iinatutibitishia bila shaka kwamba mauaji yale yalipangwaaa na serikali yenyeweeeee
   
 20. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,617
  Likes Received: 4,723
  Trophy Points: 280
  Hata hiyo hukumu yao ilikuwa kutuzuga tu wale walikuwa wamepata hifadhi tu kwani walikuwa wanatekeleza amri ya wakubwa. Yule Mmeto toka Msumbiji ana mkono katika mauji ya Gen. Kombe.
   
Loading...