Elections 2010 Kikwete apewa report ya kura za Slaa

Status
Not open for further replies.

.
Ni kweli mkuu, mfano mzuri wa vijiji ni chaguzi ndogo zilizopita. Ccm na serikali yake walishangazwa na ujasiri wa wanavijiji hasa huko Busanda, B/vijijini na tarime. Kama sii kutumia nguvu kubwa na mabavu wasingeambulia hata jimbo moja. Jijini DSM uswahili umezidi na watu wenye njaa wanaotafuta mlango wa kutokea hata kwa kuuza haki yao ya uzaliwa.
DR SLAA HANA BILIONI HAMSINI, HANA FUSO ZA KUWABEBA WASHABIKI KWENYE MIKUTANO YAKE ILA ALIMELIBEBA TUMAINI LA WATANZANIA LILILOPOTEA. HICHO NDICHO KITU WATU WANAKITAKA KUTOKA KWAKE!
 

Wait a minute. Usalama wa taifa wanamfanyia kampeni mgombea urais, JK. So campaigning for JK is among responsibilities of TISS. Tanzanians pay salaries of TISS for them to campaign for one political party and not for the interest of whole nation, Why?
 

My $100m bet.....Huyu jamaa hamwongelei mlinzi wa CJ?
 
Kinachonishangaza ni jinsi watu wanavyompa "thanks" aliyewalisha upupu wa data za hovyo. Wengine kama MMJJ huwa naamini kuwa ni mwana falsafa kumbe yumo kundini mwa vipofu
 

Huwezi kutumia matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kama benchmark ya uchaguzi mkuu. Huu ni utaahira wa hali ya juu. Mengine malizia mwenyewe.
 

Maji yapo shingoni ndiyo maana wamebadirisha ratiba. kwani wakati wanapanga ratba ya kwanza si walijua itaendelea hata baada ya Idd? Tatizo ccm wanakwenda kusi kwa ngalawa wakati pepo ni za kasi na zenye mawimbi makubwa na dhoruba.
 

Mkuu unategemea nini when TISS is not impatial and has completely lost its direction! Hebu tafuta mahojiano ya Arcado Ntagazwa na Raia mwemma utaona hili ninalolisema. TISS siyo yetu tena, ni yao. Tunatakiwa kuwapiga bao pamoja na TISS yao ili tuanze kazi ya kulisuka upya hili taifa. Miaka mingine mitano ya hasara ni jambo lisilokubalika hata kidogo.

If we don't screw them now, they do us!
 

Good observation; SASA mshauri bwana wako JK awe mstaarabu kama MBOWE alivyofanya 2005. Akubali matokeo kistaarabu atakapojulishwa kuwa Dr. Slaa ameshinda.
 
Mkuu Sikonge,

Una maoni yoyote hapo nilipo-bold?

Ndugu yangu Keil,

Hii habari imenishangaza saana. Sikutegemea Wanyamwezi wangu wawe na mwamko mkubwa namna hii kwa kipindi hiki kifupi. Naona kilimo cha Tumbaku kimewapiga Rumba hadi wenyewe wamepata hamu ya kubadili.

Nilikwama kumpata Sister hadi leo. Tatizo kubwa ni simu yangu ya kikazi ninayotumia, huwa haionyeshi namba na sasa hivi Tanzania wanaogopa simu zinazokuja bila namba. Wanasema huko Kenya watu 70 wamekufa na Arusha wamekufa wawili. Ila yeye nashindwa kabisa kumpata. Labda kaenda Kiloleli ingawa kuna kijana nilimpigia siku moja na nikampata akiwa Kiloleli. Hivyo hadi leo hii sifahamu ni Wabunge gani wa Upinzani huko Sikonge wanagombea. Kama Kakunda alihamia Chadema na Upepo huu, anaweza kuneemeka.

Wanyamwezi wangu wa TABORA Oyeeeeee!!!!!.

Nyie si Mabwege tena. Dr. Slaa tafadhali fika SIKONGE.
 

Mkuu kwani ni mara ya kwanza UwT kufanya kazi za kampeni? Mwaka 2005 ni hao hao UwT walifanya kazi ya kum-nominate JK, ndio maana unaona akina Tom Mwang'onda wakapewa u-Bunge wa kuteuliwa na Rais. DG-TISS [Apson] wakati wa mchakato wa nominations ndani ya CCM na uchaguzi ni baba wa Tom Mwang'onda. To me, Tom Mwang'onda kupewa ubunge wa kuteuliwa na Rais ilikuwa ni shukurani kwa Mzee Apson kwa kazi aliyofanya, ambayo hatuijui. Kama unataka more details, kamuulize Mzee Mangula [former CCM Secretary General].

Kuna mengi sana yanafanywa na watu wa UwT linapokuja swala la Uchaguzi Mkuu. Kwa hiyo usishangae na hizo ndio taasisi zetu ambazo zimeundwa kwa sheria za ajabu ajabu zikiongozwa na Katiba ambayo iko outdated. Ukiwaambia CCM tunataka mabadiliko, watakuja na viraka hata kama nguo yenyewe imeishachakaa, mwisho watakuwa wanabandika kiraka juu ya kiraka kingine ili mradi tu wahakikishe kwamba Katiba inaendelea kuwalinda na kulinda maslahi yao binafsi na ya chama chao.
 
Huwezi kutumia matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kama benchmark ya uchaguzi mkuu. Huu ni utaahira wa hali ya juu. Mengine malizia mwenyewe.

Mkuu, utashi wako uko wrong! Serikali za mitaa ndiyo kuna wapiga kura wote. Taswira ya nchi yoyote inaanzia mitaani. Statistics zote unazosikia hizi za REDET etc zinatoka huko na si kwingine. Kwa hiyo haikuwa vema kabisa kumwambia jamaa ulivyomwambia, unless amekukwaza na chadema yenu.
 
Pamoja na kiswahili chako kibovu nimekuelewa
ila hizo bold mbili ninakupasha kama ifuatavyo. Kama UwT wanahusika na mchezo mchafu wa kuua demokrasia nchini unatarajia kuna polisi wa kuwakamata? dawa yao pekee ni kura zetu na bunge period.

Hiyo bold ya pili unaonesha wazi kabisa kuwa unafahamu NDOA iliyopo kati ya Lipumba na CCM (nawatoa wanaCUF ktk hili maana hawajui) ndo maana umewaona wagombea wawili waliopo hatarini kupoteza reputation ni hao tu na siyo wagombea wengine wa vyama vingine. Sasa nenda kawaambie core kwamba hali imebadilika na wimbi la mabadiliko limeshachukua kasi halizuiliki.

MWISHO NI KWAMBA VITISHO NA KEBEHI HUWA NI BREAD CRUMBS MBELE YA MWANAMAPINDUZI MAKINI
 

Ha ha haaa! My dustbin is several meters away from me, lucky you!
 
Kama kweli habari hii isingekuwa na uzito tusingewaona wanaingia kwa fujo vibaraka wa CCM kuponda na kutubeza! Wengine tumesoma pschology na tumejifunza kusoma between the lines. ... utetezi wa akina Kasheshe kwangu ni ushahid tosha kuwa something fishy is going on and there is truth in this.
Pia niliata sikia ishu hii kama wiki 2 zilizopita... ndo maana tunasikia Pinda yuko UN sasa hivi badala ya JK ambaye alitarajia apumzike siku 16 na kufanyiwa ukarabati... :wink:
 
Propaganda ni kisu kinachokata pande zote, inategemea upande upi utaumia. Lakini "tuwaache watoto waende SHULENI, na wakubwa VITANI".
 
Nimesikia ni kweli; muda si mrefu itapatikana tuko tunaitafuta tarifa maalum; wamebana ni ya synovate ndio maana wametoa nusu nusu tu
 
Mwenye kuamini hizo statistics kwa kweli hana tofauti na aliyeamini kwamba CCJ ni chama tishio.....

Badala ya watu kujiuliza au kumuuliza HUTAKI UNAACHA hiyo ''statistics'' au survey iliendeshwaje na kwa sample ya watu wangapi kila mkoa, watu wapo excited kichizi na wanafurahia!

Inawezekana utafiti huo ulihusisha watu wachache mno (wasiozidi hata 100) kwa mikoa hiyo na watu wakaibuka na %!

Kazi bado mbichi sana jamani. Dr. Slaa na kamati yake ya kampeni wakaze buti tu mpaka tarehe 31.10 na tusilose focus kwa vijitakwimu tusivyojua vimepatikanaje.

Let us be a ''home of great thinkers'' for once...
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…