Kikwete angekuwa na Ajenda ya Uislamu, ningemuelewa na kukubaliana naye, lakini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete angekuwa na Ajenda ya Uislamu, ningemuelewa na kukubaliana naye, lakini...

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, May 11, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nimekaa chini na kujiulizahivi Kikwete anafanya kazi kwa manufaa ya nani?

  Kabla ya uchaguzi na hata kesho hii kuna Wakisto wengi wanaoamini kwa nguvu kubwa kuwa Kikwete yupo pale Ikulu Kui-Silimisha Tanzania na kufanya kazi kwa maslahi ya Waislamu.

  Mnaodhania hivyo, Mchungaji anawapasha kuwa Kikwete hata hao nduguze katika imani kaka na dada zetu wa Kiislamu, kawasahau maana yeye anatumikia matumbo na kutimiliza matakwa ya Mafisadi, Wawekezaji na Mabeberu anaowaita Wakubwa!

  Kwa ufahamu wangu mdogo wa Uislamu, ni dini inayolenga kwenye kuleta haki, kuboresha maisha na zaidi kuondoa unyonge, umasikini, dhiki, magonjwa na ujinga.

  Waislamu wa Tanzania kwa muda mrefu wamekuwa wakitoa kilio cha kuachwa nyuma kimaendeleo, kuwa na maisha ya hali ya chini na hata kusahauliwa ukilinganisha na wenzao Wakristo.

  Kama jinsi Wakristo wanavyojisahau na kudhani kuwa na Rais Mkristo ni tija (Ben Mkapa) ndivyo ndugu zangu Waislamu na sisi Wakristo na Wapagani tulivyopotoka na kudhani kuwa Kikwete ataleta mambo ya Uislamu na kutumia mafundisho ya Uislamu kumuongoza katika uongozi wake kuliongoza Taifa letu. Ama tulidhania kuwa ataleta upendeleo wa kimaendeleo kwa Waislamu pekee!

  Ni heri angefanya mambo kwa manufaa ya Waislamu, ningemvulia kofia na kumpa sifa. Ningemuelewa na kukubaliana naye.

  Lakini Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete, ni Mwislamu jina na si wa matendo kama vile Ben Mkapa alivyokuwa Mkristo jina na si kwa matendo.

  Niliandika awali sana kuwa Waislamu wanaweza kufanya kosa kuamini kuwa kuwepo kwa Kikwete Ikulu, basi ni suluhisho la matatizo yao.

  Matatizo ya Waislamu ni matatizo ya Watanzania wote, sema tofauti ni kuna waliopiga hatua na kuna walioachwa nyuma.

  Kama leo hii Kikwete angewatumikia Waislamu na hivyo viwango vyao vya maisha kuboreka na kupiga hatua hata kukaribiana na Wakristo ( hisia kuwa Wakristo wana maisha bora) ningepiga vigelegele na kushangilia mageuzi na kuna mafanikio ya Maisha Bora kwa Mtanzania hata kama ukweli ungebakia kuwa ilikuwa ni Maisha Bora kwa Wasilamu.

  Leo hii ningeona kwa macho na kusikia kuwa Waislamu kwa kutumia upendeleo maalumu uliofanywa na Rais Kikwete, wameongezeka idadi mashuleni na wanafaulu kwa kiwango kikubwa nimgepiga makofi. Leo hii tungeambiwa idadi ya kina mama, watoto na wazee wa kiislamu ambao wanatibiwa bila shida na wanaanza kuwa na afya njema imeongezeka marudufu, ningeangua like keleuwii la kichagga la kushangilia.

  Leo ningesikia Waislamu kutokana na upendeleo maalumu, wana nyumba bora, ajira, mazao yao yananunulika kwa wingi na wanaweza kuzalisha kwa mfumo wa kisasa wa uzalishaji, ningekusanya bendi na tuanze mdumange kumsifia Kikwete.

  Lakini kama alivyoingia madarakani, hali ya Mtanzania iwe ni Muislamu, Mkristo au Mpagani haiajabadilika, wamebakia pale pale wakisuasua na kukodoleana macho na kushutumiana.

  Anayefaidika na sera na utawala wa Kikwete ni mtu fisadi, ni mwekezaji, ni yule aliye na madaraka, ni yule aliyeahidiwa nyongeza ya mapato kwa kuonyesha utii na mapenzi bila kumkosoa Kikwete au kuhoji anayotenda.

  Mbaya zaidi wanaoneemeka kwa shibe kubwa ni Mabepari ambao tuliwapiga vita wakiwa wakoloni wetu. Mabepari hawa na Makuwadi wao ambao ndio kuna wapambe, mafisadi na wanaoshangilia kutesa kwa zamu na kuneemeka, hawana dini ya imani ya Ukristo au Uislamu ambazo zinampa tukuzo na thawabu mtu masikini.

  Hawa dini yao ni ulafi na kuvimbiwa. Humo wako Wakristo, Wapagani, Waislamu na dini nyingine ambao ibada na imani yao iko kwenye fedha na vitu vya kidunia.

  Watu hawa hutumia mazingaombwe kwenda Makanisani na Misikitini na kupewa mapokezi ya zulia kama wao ndio Miungu, na hawaishi kufadhili Makanisa na Misikiti kwa kutoa Tujisenti vyao vilivyotokana na dhuluma waliofanya dhidi ya Watanzania; Waislamu na Wakristo na kutambakuwa wanasaidia umma.

  Ikiwa leo hii bado watu wa Chanika hawana maji ya Bomba na kule Manyara watoto wanakalia mawe kwenye darasa chini ya mti, huku Kikwete na wapambe wanagombania viwanja na mapato ya miradi ya kuwakumbatia Mafisadi na Wawekezaji, iweje ndugu Watanzania tudhanie kuwa tukiwa na Rais wa Dini yetu basi tumepona na tunahemea mavuno?

  Maisha bora kwa Mtanzania hayatapatikana kutokana na Kiongozi Mkuu kuwa wa dini fulani au kutoa upendeleo maalumu kwa dini fulani!

  Maisha bora yatapatikana kutokana na Kiongozi anayewajali wananchi wake, watu waliompa dhamana ya kuongoza kwa kuwaffanyia kazi na kuhakikisha kuwa Wananchi hawa hawateseki na hawaishi katika umasikini na udun wa kupindukia.

  Maisha bora yatakuja Tanzania pale Kiongozi wetu atakapoamua kufanyia kazi na kutafutia ufumbuzi wa kudumu matatizo ya Watanzania wote bila kujali dini, imani, rika, jinsia au kabila.

  Maisha bora yatakuja siku Kiongozi Mkuu atakapoamka na kuuchukia Umasikini, Ujinga na Maradhi yanayowazunguka Watanzania na kuanzisha mfumo mpya wa kijamii, kiuchumi na kisasa mabo utaijeng nchi upya na kutoa nafasi sawa za kuleta maendeleo kwa kila mtu.

  Hivyo mnaodhania kuwa Kikwete ataleta ajenda za Kiislamu, mmelogwa na mmepungukiwa. Kawapiga changa la macho pale alipoteua Waislamu wachache hapa na pale na mkafutuka kusifia na wengine kulaani, kumbe mwenzenu maslahi anayoyafanyia kazi kwa udi na vumba na hata kuyalinda ni ya Mafisadi, Wawekezaji na Mabeberu!
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  May 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mmh.. mchungaji hapa inabidi nifunge kwanza kabla sijaamua kuchangia lakini yawezekana umegusa ukweli mkubwa zaidi kuliko unavyodhania.
   
 3. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  No comment
   
 4. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Umesema yote baba mchungaji.

  Swali la kujiuliza, nani anafaa kwenda pale Ikulu uchaguzi mkuu 2010 atuondolee matatizo haya?
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Rev. right on the money.

  Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya wa-TZ ni makafiri kwa matendo, sio viongozi tu bali kila mtu, pamoja na kujinasibu na kujipigia chapuo ktk dini fulani 'ili tusiachwe nyuma au kuonekana primitive' au kupata certain social status ambazo zinaambatana na favors plus recognition ..Dini za ikifuatwa kwa staili hii it is fair to say we are 'nominal' followers. Tungekuwa wafuasi wa kweli wa dini hizi pamoja na mapungufu yake, basi hata walau kwa asilimia 50 tu, tungekuwa mbali sana ktk right spirits.
   
 6. F

  Firdous Member

  #6
  May 11, 2010
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kishoka:

  Hii ni makala ya kwanza kuona imeelezea ukweli wa Huyu Muheshimiwa. Tujifunze tujue
   
 7. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2010
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tumelogwa na aliyetuloga ameshakufa. Tufanyeje?
   
 8. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  huyu hatufai. inabidi aondoke mwaka huu apumzike kwa amani ili watu wengine ambao wako serious waingie kazini.
   
 9. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hahaha, umesema kweli, tena wametulogea kule kwenye zindiko la taifa la Lindi kwa wale wanaojua hili. we unafikiri kwanini kina kingunge na vizee vingine bado tu wanaitwa wazee wa chama? ni kwasababu kuna siri huwa wanaenda kuifanya kila wakati wakitaka kufanya uchaguzi, kuzindika nchi kwa term ya miaka mitano yote, and so is kila mwaka. ....utawala unaenda kuombwa kwa shetani mwenyewe, na shetani anataka sadaka kama za mv bukoba, reli ya kati na maajali yasiyokuwa na kichwa wala mkia. nchi hii inaongozwa na nguvu za shetani wajameni.....ila kuna siku Mungu ataingilia kati, na hayo yote yatakuwa historia, aibu itawapata hata watatamani miamba iwadondokee.
   
 10. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mchungaji, uliyoyasema yana mantiki sana. Lakini, kuna yaliyo nyuma ya pazia ambayo tusipoangalia nchi inaweza kwenda tusikokutaka kwa sababu ya udini. Rais wa nchi anaweza akawa mkristo ama muislamu jina, lakini kuwa hivyo ama kutokwenda kwake msikitini ama kanisani hakumfanyi awe neutral. Kiongozi asiyemcha Mungu ni rahisi sana kuyumbishwa ama kurubuniwa akaitumbukiza nchi kwenye matatizo ya udini. Halikadhalika, kiongozi asiyemcha Mungu mara nyingi si rahisi kwake kutilia maanani mustakabali wa wale anaowaongoza kwa sababu hajali mafundisho ama miongozo ya kidini. Ogopa sana kiongozi mbinafsi asiyejali mafundisho ya dini yake, ambaye sifa na kutukuzwa ndani na nje ya nchi yake ndio vitu muhimu zaidi kwake kuliko wale waliompa dhamana ya kuwaongoza.
   
 11. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Interesting!!!!????
  Mmmh hatari tulivyo na dini na madhehebu mengi tz, mikesha ya maombi na vikundi vya maombi ya jumuiya kila mitaa,kata,tarafa.... SASA HIVI MAOMBI MENGI KWENYE MIKESHA NI UCHAGUZI WA 2010 kama ilivyokuwa 2005 kumbe bado UTAWALA WA TZ UNALETWA NA SHETANI! mmmh bado shetani anatuongoza looh sasa tufanyeje jamani! kama sheikh mkuu,kakobe,mwingira,Dr Mch rwakatale mpo jamvinii hebu mtusaidie! tufanyeje?
  Maelezo yako yana ukweli kuhusu ajali...its good observation anyway maana taarifa nyingi za uchunguzi wa ajali hazitolewi na hata zikitolewa zina kosa mantiki.....'meli ilijaza kupita uwezo' its shame mbona mlijua kutoka kemondo bay na hamkuchukua tahadhari yoyote.....may be kafara!!1 at least iyo inapenya wenye ubongo wangu mie niliyelelewa kwenye imani za supernatural power  NANYI MTAIFAHAMU KWELI NA HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU
   
 12. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  mKUU KISHOKA HAPO UMESEMA UKWELI
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  May 11, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kishoka,
  Mkuu hapa sintakubaliana na mawazo yako na hasa hicho kichwa cha mada hii. Mkuu unapotosha na pengine kufikiria vitu ambavyo ni hatari zaidi ktkmaisha ya binadamu.
  Uislaam haudai kupendelewa isipokuwa unapinga kupendelea. waislaam wa kweli hawatakubali kupendelewa isipokuwa wale wasiojua nini maana ya Uislaam. Uislaam unapinga Kuonewa kwa mtu yeyote.

  Tofauti na Kupendelea, Uislaam unataka kuona HAKI ikitolewa kwa watu wake pasipo kujali imani zao na HAKI pekee ndio Uislaam mwenyewe. Hivyo kama Kikwete rais wa nchi atajaribu kupendelea waislaam huyu atakuwa ametoka ktk Uislaam kwa sababu huwezi kupendelea kitu kimoja pasipo kukinyima haki kitu kingine..Unless, umetumia neno kupendelea kwa sababu makusudio ya kuwaokoa kwanza wale waliokuwa wanyonge..

  Hata hivyo, waislaam Tanzania sii wanyonge hata kidogo iwe kikatiba au kiasili ukalinganisha na Wanawake ama walemavu. waislaam wana hakisawana wakristu isipokuwa waowenyewe ndio Tatizo. Unyonge wa waislaam Tanzania hauna tofauti na Unyonge wa Watanzania wote kwa ujumla wetu - UJINGA na ULIMBUKENI umetujaa!
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mkandara,

  Kila siku tunakumbushwa kuwa Waislamu maisha yao ni duni, kutokana na Wakristo kupendelewa na Wakoloni na kisha Nyerere na CCM. Alipokuja Kikwete, kulikuwa na shamrashamra za kusema "sasa tumepata Rais wetu" mithali ya Wamarekani weusi aambao wanatafuta Rais wao pekee.

  Hata humu ndani kumekuwa na mijadala mingi ya kidini kutoka kwa Wakristyo wenzangu wakimlaani Kikwete kwa Uislamu wake na si Uongozi wake na kudai yeye anafanya mambo kwa manufaa ya Waislamu.

  Kilio cha Waislamu kimejulikana kwa muda mrefu kuwa ni maisha duni, ukosefu wa maendeleo na hata kukosa uwakilishi, iwe ni Bungeni, Wizarani au kwenye Mashirika.

  Sasa nilichofanya ni kuwajibu wote ambao walidhania kuwa kwa kuwa Kikwete ni Mwislamu basi atafanya mambo kwa upendeleo kwa Waislamu, kuwa wamepotea.

  Kama angefanya upendeleo ambao ungeonyesha kukua kwa maendeleo hata kwa Waislamu pekee, wala nisingejali ningemuunga mkono kuwa ana azma wa kuondoa umasikini.
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Nilishasema kuwa hapa jamvini kuna watu wana busara dunia nzima, we kubwa ni miongoni mwao. Hii article inaonekana imeandikwa na mtu mzima mwenye akili timamu na mawazo ya kujenga alokaa chini na kutoka na kitu kizima.
  Mkubwa sina nyongeza katika hii article umesema yote ambayo nilipaswa kuyaongeza. Thanx!
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  May 11, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kishoka,
  Mkuunakuelewasana isipokuwa statement yako hii ya mwisho -
  Hapo uko peke yako mkuu wangu huo sii Uislaam ila ni Udini ambao ungeturudisha nyuma zaidi ktk Umaskini..kumbuka tu sasa hivi tunagawana Umaskini, Ukimpendelea mmoja ina maana unamdhalilisha mwingine..
   
 17. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #17
  May 11, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Well said...!
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Naona umepangilia hoja zako vizuri (kama ilivyo kawaida yajko) Mchungaji. lakini nikisona unavyo-arge naona kuwa unaweza kuwa unafanya kosa la kuwa short sighted kwa maana kuwa unaangalia sana karibu.
  Pamoja na kuwa Kikwete hajaonekana kuleta mabadiliko kwa waislamu katika muda mfupi huu, kuna uwezekano kuwa anachokifanya ni kuandaa mfumo. Mfumo huu ndio msingi wa kunufaisha kundi moja. Hali hii inaweza isionekane hivi sasa lakini ikaja kujitokeza dhahiri miaka mingi baada ya yeye kuondoka. Kuna uwezekano kuwa footwork ya kuandaa mfumo huo inafanywa na yeye hivi sasa, na inaweza kuwa ndio chanzo cha malalamiko tunayoyasikia.
   
 19. Ngomo

  Ngomo Senior Member

  #19
  May 12, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 199
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  hii article imeenda shule
   
 20. M

  Myaye Member

  #20
  May 12, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Re: Kikwete angekuwa na Ajenda ya Uislamu, ningemuelewa na kukubaliana naye, lakini

  Hakika we Umenena, mada hii imejitosheleza. Hakuna Ndoto ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania. Kila kukicha twaja na Slogan mpya! Leo Elimu kwanza wakati idadi na kiwango wanachofaulu kinashuka. Kilimo kwanza, Mfuko wa Mbole Laki, Malaria haikubaliki tugawa Vyandarua tu, hatuangalii Mazalia ya Mbu, Bei ya Dawa za Mbu wala Dawa za Malaria!
   
Loading...