Kikwete angekuwa na Ajenda ya Uislamu, ningemuelewa na kukubaliana naye, lakini...

Reverend, a big thank you! umenikumbusha stori ya wakenya kusherehekea kwa nguvu Obama kuwa Rais wa marekani! Ni mapinduzi tuu, ambayo yanapaswa kukupa nguvu kwamba despite the color of my skin, i can go beyond the sky! Dini ina-impacts (kwa mtazamo wangu mie) kwenye ndoa tuu, kwani ukaribu wake ni too much! Lakini, KABILA, RANGI YA NGOZI, WALA DINI havina tija katika maendeleo ya nchi hii! Naona na wengine wameshaanza kurudisha u-zanzibara na uzanibari!
 
Ni kweli huwezi pata maendeleo kwasababu tu rais wa jamhuri ana dini inayofanana na yakwako. Kwa Tanzania hii ya leo, ukitaka kuendelea itabidi uwe fisadi, au mwekezaji, au beberu au kwa uhakika zaidi vyote vitatu!!
 
Rev. Kishoka,
Mkuunakuelewasana isipokuwa statement yako hii ya mwisho - Hapo uko peke yako mkuu wangu huo sii Uislaam ila ni Udini ambao ungeturudisha nyuma zaidi ktk Umaskini..kumbuka tu sasa hivi tunagawana Umaskini, Ukimpendelea mmoja ina maana unamdhalilisha mwingine..

Maendeleo ya Mkandara, ni maendele yetu wote. Sikatai si sahihi kuwa na upendeleo maalumu au hata udini. Lakini kama upendeleo huu ungelenga kuboresha maisha ya wengi ambao wana hali duni na tukaona mafanikio ya kweli, ningekubaliana hata kwa shingo upande.

Lakini anachofanya yeye ni lile la kusema Tajri aneemeke zaidi na masikini adhoofike maradufu!
 
Hii inapaswa atumiwe Dr. Slaa na itakuwa fungakazi kwa wanaoendekeza udini. Hawa wameshindwa kutawala sasa ni kugawa watanzania. Waogoppeni hao kama ukoma.
 
Mi nakushangaa ndugu mtumishi nenda chuo kikuu cha dodoma kimejaa waislamu wakiite tu chuo kikuu cha kiislam,management yote imejaa waisllam tena wapemba .walimu asilimia 90 ni waislam,amini usiamini nendeni pale mshuudie
 
Maoni yako ni kweli, ila tatizo linaletwa na kikundi kidogo sana cha waislamu wanaoangalia dini ya mtu bila kujali anafanya nini. Kwa wao wanachotaka ni kiongozi mwislamu, atawasaidia au atawasahau hilo siyo swala kwao, kinachomata ni ile dini yake tu. Sidhani kama wakristu wana sensitivity kali kuhusu dini ya kiongozi wa kisiasa kwani najua kuwa baadhi yao waliwahi kusema kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu wao. Katika kundi lile la waislamu wasioamnini dinadamu mwingine yeyote asipokuwa mwislamu, isingewezekana kutamka hivyo kwa mgombea mkristo.
 
Mnaodhania hivyo, Mchungaji anawapasha kuwa Kikwete hata hao nduguze katika imani kaka na dada zetu wa Kiislamu, kawasahau maana yeye anatumikia matumbo na kutimiliza matakwa ya Mafisadi, Wawekezaji na Mabeberu anaowaita Wakubwa!

Napendelea sana kuona kuwa huo ni ukweli, ambao sasa ni wakati muhimu kwa waislam kuukubali na kuunganisha nguvu yao na wakristu na matabaka mengine yote ...ili kuushinda ufisadi! Ufisadi si lele mama, unahitaji umoja na muugano wa Kitaifa na sio tabaka moja pekeyake... Fisadi hashindwi kwa namna hiyo!

Rais anapaswa kuutuunganisha ili kuutokomeza Ufisadi!

Lakini kama hatafanya hivyo mafisadi watamtumia kututenga kwa ajili ya faida ya mafisadi hao!
 
Nilitaka kuanzisha mada yenye kichwa cha habari STUPID MEMBE want Tz to join OIC for begging. nilikuwa nasema stupid kwa kuwa namuona kama mtu mwenye mawazo ya kuwa ombaomba ilhali nchi ikiwa na kila mali-asili na watu kwa ajili ya kutafuta maendeleo yake yenyewe. nilishtushwa na habari ya Membe kuwaita viongozi wa kikristo Mwanza na kuwaomba kuridhia Tanzania kujiunga OIC kwa kuwa wanachama wa OIC wana mapesa mengi kwa hiyo viongozi wa CCM wataenda kuomba na kuchotewa.
Dhana ya kujikomboa ni ya kutumia kile tulichonancho ili kufanikisha malengo yetu na si kujikita Umatonyani
 
Jamani samahani,

Hivi huo Kikwete anasali sala tano wapi? Mimi nasikia sala ya Eid tu... hata slaa za ijumaa sijui kama anasali...
 
Kikwete angekuwa na Ajenda ya Uislamu, ningemuelewa na kukubaliana naye, lakini..

Hiyo title mmhh..Sizani kama kweli unaweza kukubaliana na mtu mwenye ajenda za udini (ubaguzi).. huo ni kama mtego. UFISADI, UKABILA NA UDINI kwangu vyote ni sumu ya maendeleo...we can not justify one or the other
 
Maoni yako ni kweli, ila tatizo linaletwa na kikundi kidogo sana cha waislamu wanaoangalia dini ya mtu bila kujali anafanya nini. Kwa wao wanachotaka ni kiongozi mwislamu, atawasaidia au atawasahau hilo siyo swala kwao, kinachomata ni ile dini yake tu. Sidhani kama wakristu wana sensitivity kali kuhusu dini ya kiongozi wa kisiasa kwani najua kuwa baadhi yao waliwahi kusema kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu wao. Katika kundi lile la waislamu wasioamnini dinadamu mwingine yeyote asipokuwa mwislamu, isingewezekana kutamka hivyo kwa mgombea mkristo.

Hilo sio tatizo la waislamu tu, ata madhehebu mengine ya dini wapo watu kama hao. Please avoid stereotyping/prejudice, hizi ndio huleta discrimination
 
Kutumia udini kwa manufaa ya udini tu pekee ni vigumu sana kufahamu hasa kwa kuwa hilo ni jambo ambalo litaweza fanyika kwa usiri mkubwa sana kutokana na utwala wa nchi ulivyoundwa. Kama anatumia udini au sio, jibu ni open ended pia- ndio au siyo. Kwa kupima kiongozi kwa matendo yake ya kukumbatia mafisadi si kipimio tosha cha kusema yeye hatumii udini kwa manufaa ya udini pekee. Naamini kunaweza kuwa na some degree ya udini na hilo ni vigumu kujulikana maana hatuwezi kuona ya moyoni, au jinsi washauri wake wanavyompa ushauri. Na hili ni kugumu kulipima hasa ukiangalia historia ya nchi na kauli za hajo ya "kuredress religious imbalanceses" za kiuchumi zitolewazo na makundi yanayoamini juu ya "imbalancess" hizo.
 
Very technical article. Maana yake tusichague viongozi kwa kuangalia ni wa dini gani bali tuchague kiongozi kutokana na uwezo wake wa kuongoza na awe mtu ambaye atatutoa kwenye hiki kisima cha umaskini tulimo.
 
Nimekugongea thanks hapo juu. Huo ni ukweli kwamba jk kashikwa akashikika mikononi mwa mafisadi, na kamwe hatakuja kuweza kujinasua kwani hadi sasa wanaendelea kutumia pesa zao nyingi kumrudisha madarakani ili waendelee kutunyonya. Suala la udini ni kwa kiasi kidogo tu au tuseme uwingi wa watendaji walio dini moja na JK wanatokana na ugawaji madaraka kijamaa au kishkaji zaidi na kwa sababu wengi wa washkaji wa JK ni waislam ndio maana inaonekana hivyo. Kiukweli mimi binafsi kamwe simuhukumu JK kwa udini bali ni kwa utendaji mbovu wa yeye na serikali yake. Hata angeweka waislamu wote viongozi wakapaform the best sidhani kama kuna ambaye angelalamika kivilee.
 
Back
Top Bottom