Kikwete Anafanya Kweli

Hivi hatuyaoni au ni kuna ka siri gani kalichofichika? simply,

1) WAKATI WA NYERERE, Ufisadi ulikithiri tena wakutututia wa Tanzania umasikini usio kifani, mfano, tulikuwa hatuna hata chakula, katika nchi kama hii, ambayo muda mchache kabla nyerere hajaipokea toka kwa waingereza, ilikuwa ni nchi inayojitosheleza kwa kila kitu, nikimaanisha kulikuwa hakuna shida ya chakula, mazao yetu tulikuwa tukiuza mpaka nje, aina tofauti za vyakula kutoka nje vilikuwepo tena kwa bei nafuu.

Ilifikia wakati Tanganyika ilikuwa inachukuwa labourers kutoka nchi za jirani kuja kusaidia kazi za kilimo, jinsi kilivyo shamiri.

Yote hayo nyerere alifisadi mpaka ikawa hatuna hata chakula, na ni kwa muda mfupi tu, akatufanya masikini wa mwisho duniani. Na hakuna aliyethubutu hata kumsema wacha kukemea, ilikuwa watu hata wakitaka kujiuliza tuu kuhusu nyerere, basi wananong'ona wasisikike, jee, kuna ufisadi zaidi ya huo?

Watu walikufa hovyo, wengi tuu, walipokuwa wakihamishwa kutoka sehemu zao asili kulazimishwa kwenda kuanzisha vijiji vya ujamaa maporini, walioliwa na wanyama, waliogongwa na nyoka, waliokufa na njaa, waliokufa kwa kukosa huduma za afya maporini. Hayaelezeki ni mengi sana. Jee, ni nani alihukumiwa wakati wake na baada ya nchi kumshinda tukiwa kwenye lindi la umasikini, serikali iliyofuatia ilithubutu hata kumuuliza au kusema lolote baya? hakuna. serikali ilibaki kumsifu ki uwongo, kwani sijui hata moja la kumsifu dikteta aliyetowa roho za watu, ni nini cha kumsifu?

awamu ya pili ina dhambi zake nyingi tuu za ufisadi, nani aliyefichuliwa?

awamu ya tatu hali kadhalika, nani aliyefichuliwa?

Awamu ya nne, tunaona magavana, mawaziri, mabalozi na wengine wengi wapo njiani wakifichuliwa kwa ufisadi, kwa kipimo chenu cha kupigana na ufisadi ni awamu ipi bora? au hamuoni ukweli?

Mimi nasema, nikiwa shahidi wa kujaaliwa kuwepo awamu zote hizi, kuanzia ya kwanza hadi ya nne, bora kuliko zote ni awamu ya nne.

Ahsante JK kwa kazi nzuri unayoifanya na wasioliona hilo wana agenda ya siri! waiweke wazi tuu, lakini wasifunge macho na kujifanya hawaoni JK anapofichuwa mafisadi.

Hongera JK keep it up. Watasema tuu linalowakera siku moja, chuki yao kwako ni nini? Lakini kwa kazi, unaifanya na unastahili sifa kede-kede.
 
Tutajua kama anafanya kweli akija na mawaziri 10 badala ya 60

Tuacheni ushabiliki, this is not practical in our country,,, just b'se of information system and infrastructure...

Kwenye nchi zilizoendelea kujua what is happening Rukwa ni simple... kwetu ni tofauti... kwa sababu ya
--Elimu za viongozi wetu kwenye kutoa appropriate feedback... wakati mwingi viongozi wanadanganywa hivyo wanahitaji kwenda kuona wenyewe... sasa ikifikia hapa niambieni waziri ataumia njia gani kufika Mpanda vijijini na kurudi baada ya 24-32hours.

--tatizo ya reli, mabarabara, viwanja vya ndege linalazimisha uwe na watu wengi kufanya kazi fulani... sina muda lakini ningeelezea vizuri zaidi baadaye.

--the best you can do no kiwa na wizara kati ya 20-24... other than that ni utani utakuwa unafanya...
 
Kuna seemu nilisema kama Muungwana hafahamiki anaweza akazungumza na kukuvika kilemba cha ukoka ili akuone unavyozidi kuboronga alafu anajidai kama mwoga hawezi kukufukuza moja kwa moja anachimba chini kwa chini matendo yako ndio yatakayokukwamisha.
Hawa wezi wa Tanzania wapo wengi maana akishawaweka wote mkononi basi hata zile hasila zangu zitapungua na kuondoka kabisa maana nina hasila na Muungwana kwa zile njia za panya alizopita hadi kuibuka kidedea.
Mnajua wandugu huyu Muungwana alikuwa na malafiki rafiki wengi tu na aliwashirikisha katika timu yake ile ya kuwania Uraisi wakati kila mmoja alikuwa na lengo lake ,Muungwana akiwa na lengo la kuindeleza Tanzania wale wengine waliona akishinda Muungwana basi watajitafunia mali zote za Inchi hii.
Halafu Muungwana ametumia uungwana wake amewapa Uwaziri unaibu na kila aliyebahatika kukumbukwa alipatiwa mahali pa kushika,kumbe mwenzao alikwisha wajua hawafiki mbali na ndio utakuwa mwisho wa uswahiba ,mimi kwa akili yangu sitegemei kufungwa mtu katika hizo skendo ninachoaoona ni kwamba muungwana aliwapa nafasi wale mpaka wakamatwe na tumeona tayari wameshakamatwa na hivyo zaidi atawambia wakapumzike hakuna kesi walichopata ndio wamepata inategemea tu walikihifazi vipi.
Na naamini sasa ndio mkakati wa awamu ya pili umeanza na kutakuwa hakuna kulala kila mmoja analinda unga wake usimwagike kwani ukiteleza tu umewajibishwa na hivyo kujenga mhimili mzuri wa viongozi kutoogopana katika kutetea maslahi ya Wananchi,viongozi au mawaziri ikiwezekana hata Raisi aweze kuhojiwa juu ya shutuma mbalimbali na masuali yawe open zikiwemo Tv na Televisheni kuonyesha Mtu anavyowekwa kiti moto ,ndio maana yake tusiwe tunahusudu mambo ya Ulaya wakati kule sheria zao hazimwonei haya kiongozi ndio tunawaona viongozi wa Uingereza kupanda Baiskeli si jambo la ajabu hapa TZ Waziri akiukwaa tu Uwaziri basi hata baiskeli haijui inabidi umfahamishe maana ukimwambia unataka kitendea kazi atakuambia uwezo mdogo na mafuta ghali wakati baiskeli haihitaji mafuta ,yamenikuta.
 
Safi sana Bobby kwa kutupa huo mtazamo.By the way swali linakuja hivi nani kampa PM kazi yake?That person is accountable to whoever appointed him a'fu pia the one who appointed him needs to check on their performance ama?Kwa hivyo mtazamo wangu ni kua JK has a big level of responsibility on what happens in the country.Tuambiani ukweli na tuache uzalendo wa kipuzi.
Wacheni hizo,Muungwana anastahili pongezi nyingi tu ,mnajua mnakuwa na papala halafu kila kiumbe ana tabia zake japo nyote mna miguu miwili ,kwa mfano nikuambieni kama samaki ana miguu mtaniona natoka sayari nyengine kabisa ila samaki anayo miguu.
Zaidi mlitaka huyu mtu awe dictor kwa mambo ambayo mnadai..kwa nini eti hakuchukua hatua za haraka ,akili za wabongo ni maarufu na kama angeanza mtindo huo wa kila anaeburuga akamfukuza basi angekwisha lifukuza wengi tu na hakuna kitakacho kuwa na watu wataizoea hali hiyo jambo ambalo sio zuri,mtasema Chukua chako mapema au ponda mali kufwa kwaja ,what was needed ni timing ambazo ikiwa umekusudia kufanya kweli basi zitafika wakati wake na kuzichukua bila ya matatizo yeyote na ndio tuonavyo hatua zinachukuliwa na kila mmoja ameridhika kabisa hakuna anaeweza kumtetea mtu kwani ukiangalia utaona ni uzembe tu.
Huwezi ukakurupuka tu ukaanza kufukuza viongozi wenzio ,kama kuna kiongozi mmoja jina nimelisahau Muungwana alipelewa barua ya jungu na akamfukuza yule jamaa ,baadae alikuja kutambua kuwa alikuwa ametenda kosa la kuchukua hatua bila ya kufikiria sana kwani kuamini kila unachoambiwa kuna hasala zake.Ila alisikika akijutia uamuzi ule.Ndio wale wachezaji wanaofika kwenye lango na kupaisha mpira juu wakati hata golikipa hayupo ni kutaka kuonyesha usanii tu ,matokeo yake ni hasara.
Kama samaki hana miguu anatembeaje kwenye maji.Usije ukanambia anaogelea maana itabidi tuseme ana mikono.
 
Wacheni hizo,Muungwana anastahili pongezi nyingi tu ,mnajua mnakuwa na papala halafu kila kiumbe ana tabia zake japo nyote mna miguu miwili ,kwa mfano nikuambieni kama samaki ana miguu mtaniona natoka sayari nyengine kabisa ila samaki anayo miguu.
Zaidi mlitaka huyu mtu awe dictor kwa mambo ambayo mnadai..kwa nini eti hakuchukua hatua za haraka ,akili za wabongo ni maarufu na kama angeanza mtindo huo wa kila anaeburuga akamfukuza basi angekwisha lifukuza wengi tu na hakuna kitakacho kuwa na watu wataizoea hali hiyo jambo ambalo sio zuri,mtasema Chukua chako mapema au ponda mali kufwa kwaja ,what was needed ni timing ambazo ikiwa umekusudia kufanya kweli basi zitafika wakati wake na kuzichukua bila ya matatizo yeyote na ndio tuonavyo hatua zinachukuliwa na kila mmoja ameridhika kabisa hakuna anaeweza kumtetea mtu kwani ukiangalia utaona ni uzembe tu.
Huwezi ukakurupuka tu ukaanza kufukuza viongozi wenzio ,kama kuna kiongozi mmoja jina nimelisahau Muungwana alipelewa barua ya jungu na akamfukuza yule jamaa ,baadae alikuja kutambua kuwa alikuwa ametenda kosa la kuchukua hatua bila ya kufikiria sana kwani kuamini kila unachoambiwa kuna hasala zake.Ila alisikika akijutia uamuzi ule.Ndio wale wachezaji wanaofika kwenye lango na kupaisha mpira juu wakati hata golikipa hayupo ni kutaka kuonyesha usanii tu ,matokeo yake ni hasara.
Kama samaki hana miguu anatembeaje kwenye maji.Usije ukanambia anaogelea maana itabidi tuseme ana mikono.

Mwiba tutazidi kumhoji bila ya kumpa pongezi. Anacheza bado watu walipiga kelele sana akawa anacheka cheka hadi alipo ona kwamba Kenya moto na TZ yanaweza kutokea na watu wenye uchungu kusema ukweli akashindwa kufumbia macho ile report .Asingaliweza kukaa kimya maana ile report kwenye Tume walikuwepo wapinzani ambao pia waliandaa report yao so hakuwa na namna tungeliyajua yote haya .Ni kazi yake na wala si kumpa sifa .Tunangona kuja ya BOT na Madini .Maana BOT hakuna mpinzani na hapa ndipo atakapo tuchezea sana .Kwenye Madini Zitto is there atasema .JK hastahili pongezi afanye kazi aliomba kazi .Uache unazi hapa .
 
JK hahitaji sifa zozote. Yote yaliyofanyika naamini alikuwa anayajua kabla na anahusika. Isingekuwa upinzani (dr Slaa na Zitto) kulishupalia hili jambo kusingetokea lolote. Baada ya mawaziri na wabunge wa CCM kuzomewa ndio akashtuka anaweza kukoa 2010. Lakini ya tote tusubiri siku nikiona BOT na mikataba ya madini ambayo nina uhakika jina lake litakuwepo inaanikwa hapo nitampongeza.
 
Ansbert Ngurumo



KWA mara ya kwanza tangu serikali ya awamu ya nne iingie madarakani, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.

Baada ya yote yaliyojadiliwa kuhusu yeye, kabla na baada ya kujiuzulu kwake, inatupasa kukubali ukweli kwamba Lowassa ameondoka ili Rais Jakaya Kikwete abaki.

Vinginevyo, ilibidi waondoke wote, kama walivyoingia wote.

Sijui kama walikuwa wanajua kwamba kimsingi, lilikuwa limeanza vuguvugu – na bado lipo – kwamba Kikwete ajiuzulu ili ufanyike uchaguzi mpya kwa sababu ameshindwa kuongoza nchi.

Katika miaka miwili tu ya utawala wao, ufisadi umekithiri serikalini, huku yeye na mawaziri wake wakiutetea waziwazi, hata kwa kutumia mamilioni ya fedha zetu kuzunguka mikoani kuhadaa wananchi.

Vilio vya wananchi maskini na wanaharakati vimepuuzwa, huku rais mwenyewe akitoa kejeli na kuviita ‘kelele za mlango’, ambazo hazimzuii mwenye nyumba kulala. Na wengine wanasema kwamba katika miaka miwili ya Kikwete, umefanyika ufisadi mbaya sana kuliko wa miaka 10 ya Benjamin Mkapa, na kwamba ndiyo maana anawakingia kifua kina Mkapa.

Baadhi wameshaanza kusema: ‘Miaka miwili inawatosha. Kuwaongezea miaka mingine mitatu ni kuzidi kukaribisha uharibifu mkubwa kwa taifa. Waondoke sasa.’

Tuishukuru ‘Kamati ya Mwakyembe’ imewasaidia kuamua na kuondoka, wakiongozwa na Lowassa. Lakini bado amebaki mmoja. Je, kuondoka kwa Lowassa kutambadilisha Kikwete?

Wanaolitazama suala la Richmond kwa haraka haraka wanammwagia shutuma nyingi Lowassa kana kwamba alikuwa peke yake.

Tuseme ukweli. Lowassa alikuwa mtumishi mteule wa rais. Amekuwa akisisitiza si zaidi ya mara moja kwamba anatekeleza mambo mawili – Ilani ya CCM na maagizo ya rais.

Tunaijua katiba yetu. Waziri Mkuu hawezi kutekeleza suala lolote kitaifa ambalo hajaagizwa na rais, halafu rais asimfukuze kazi. Ni kweli, mchakato wa Richmond umeonyesha maagizo na shinikizo la Lowassa.

Lakini kwa muda wote huo, kama Lowassa angekuwa amejituma tu bila kutekeleza agizo au makubaliano, asingekuwa madarakani. Angefukuzwa kazi na rais mwadilifu.

Akiwa Waziri Mkuu, Lowassa alikuwa mtekelezaji wa maagizo ya wakubwa wake pia. Alikuwa anasimamia makubaliano, ambayo hata Rais Kikwete aliwaambia waandishi wa habari Ikulu mwaka 2006 katika kuadhimisha mwaka mmoja madarakani.

Rais Kikwete aliitetea sana Richmond, na akatamka kwamba alihusika moja kwa moja katika kuiteua kampuni hiyo baada ya kuridhika kwamba ilikidhi vigezo, hasa vya nafuu ya bei ya gharama ya umeme.

‘Ripoti ya Mwakyembe’ imeonyesha udhaifu mkubwa wa utawala wa nchi yetu. Imethibitisha kwamba viongozi wetu wanakurupuka. Wanadanganyika na kutudanganya sisi. Vinginevyo, wanatutumia kutekeleza mambo yao.

Utamu wa kashfa ya Richmond ni kwamba, wote wanaohusishwa na kampuni hiyo feki kwa karibu sana, ni marafiki wa karibu na washauri wa Rais Kikwete – ule utatu uliounda na kuongoza ‘mtandao wa Kikwete.’

Kama tungeweza kuwatania, tungesema kwamba kwa mujibu ya Kamati ya Bunge, Richmond ni kampuni feki ya vinara wa mtandao!

Yawezekana ndiyo maana rais alishindwa kuwachukulia hatua. Kwa bahati mbaya mambo yanapoharibika, anayewajibika ni waziri mkuu, si rais!

Huu ndiyo mzigo ambao Lowassa amelazimika kuubeba. Na kwangu mimi, huu ndio ushujaa wa Lowassa. Maana ilibidi ‘afe’ mtu. Amekubali ‘afe’ yeye ili mkubwa ‘aishi.’ Amejitoa kafara ili kumnusuru Kikwete na serikali yake. Mdogo lazima awajibike.

Vinginevyo, kama rais hakuhusika kabisa, angekwishamfukuza Lowassa kazi tangu zamani. Wala asingesubiri kamati ya Mwakyembe imueleze la kufanya.

Na asingesubiri Lowassa mwenyewe aandike barua ya kujizulu. Na kama Lowassa hakujiuzulu, hata Baraza la Mawaziri lisingevunjwa juzi.

Kuna sababu ya ziada. Tangu Serikali ya Kikwete ilipoingia madarakani, imesemwa mno kwamba Lowassa ndiye amekuwa ‘mkono wa kulia’ wa Kikwete na Rostam Aziz ni mkono wa kushoto wa Kikwete katika kuendesha serikali.

Makamu wa rais hazungumzwi. Kikazi, Lowassa amekuwa mtendaji, Kikwete msemaji, Rostam mshauri. Na inajulikana kwamba mengi ambayo Lowassa alikuwa anayasimamia na kuyatenda hayakuwa yake.

Na kwa jinsi ilivyo katiba yetu, hata makosa ya rais, kama lazima yatekelezwe, ni waziri mkuu anayeyasimamia; na ndiye atakayelaumiwa.

Haya haya yanayomkuta Lowassa leo, yaliwahi kumkuta mzee Rashid Kawawa katika kusimamia makosa ya Rais Julius Nyerere katika kutekeleza sera ya vijiji vya ujamaa.

Kwa hiyo, katika hili, Lowassa atazomewa, Kikwete atashangiliwa. Lakini lao ni moja, na walilitekeleza kwa kuliamini.

Kilichomponza Lowassa zaidi ni hulka binafsi. Si mwoga wa kuchukua uamuzi. Ni mtekelezaji – na mara nyingi amesifika kwa kutumia mabavu kuhakikisha anachoagiza kimetekelezwa.

Leo kuna mambo ambayo serikali inajivunia kwamba imeyafanya. Ni lipi lililofanyika bila usimamizi au maagizo ya Lowassa? Kama yapo, ni machache. Kama kuna mafanikio ambayo Serikali ya Kikwete inajivunia leo, tukubaliane kwamba hayawezi kutajwa bila kumhusisha Lowassa.

Kisa? Kwa wadhifa wake na kwa hulka yake, ni mtendaji, msimamiaji na mtekelezaji. Wanaomjua wanasema Lowassa halali hadi alichodhamiria kimetekelezwa.

Utekelezaji na usimamizi ni sifa binafsi inayomtofautisha Lowassa na Kikwete. Hata wale wanaompinga, linapofika suala la kufanya uamuzi na kuusimamia, wanakiri kwamba ‘Lowassa anaweza.’

Kwa hiyo, tunapomtazama na kumjadili Lowassa leo, ni vema tutambue kuwa alikuwa mtekelezaji tu; si mwamuzi pekee. Hili ni lao, si lake peke yake.

Katika kusisitiza hulka yake, wapo wengine wanaosema kwamba bahati mbaya ya Lowassa imetokana na tofauti nyingine kuu kati yake na rais; kwamba Rais Kikwete anapenda madaraka, Lowassa ‘anaijua’ pesa – ni mtafutaji.

Na kwa bahati mbaya amekuwa mmojawapo wa watu wanaotafunwa na ‘mzimu’ wa Mwalimu Julius Nyerere.

Zaidi ya hayo, Serikali ya Kikwete na Lowassa imemomonyolewa na mbinu walizotumia kuingia madarakani – zikiwamo kuchafuana majina, matumizi ya pesa zenye kutiliwa shaka, na mengine mengi yanayofahamika kama mbinu za kisiasa, lakini yanayofananishwa na ufisadi.

Leo hii, wapo watu wanasema wazi wazi kwamba watu hawa waliingia kwa ufisadi, wataondoka kwa ufisadi. Kundi hili hili ndilo lilitueleza ‘ufisadi’ wa Mkapa na Frederick Sumaye. Leo tunapolipima kundi lao na akina Mkapa, nani ni nafuu? Nani anaweza kumcheka mwenzake?

Hata wale waliokuwa wanamtetea Rais Kikwete kwamba ingawa amezungukwa na ‘watuhumiwa’ yeye ni mtu safi, sasa wanahoji sababu halisi za yeye kujiruhusu kuzungukwa na hao wanaotuhumiwa, ambao anawaamini sana.

Au ni yale yale ya Mkapa wa mwaka 1995, aliyeitwa Mr. Clean? Kilichomaliza usafi wa Mkapa kitauacha wa Kikwete huyu anayezungukwa na kundi hili?

Serikali ya Kikwete ilishazama kaburini. Lowassa ameisaidia kwa kujizulu. Nimesoma kauli yake. Amesikitika. Najua wapenzi wake hawana raha. Rais Kikwete hana raha.

Lakini naamini siku zinakuja ambapo Lowassa atagundua kwamba kitendo alichofanya juzi kujiuzulu, ni ukombozi kwake binafsi na kwa taifa.

Na kwa kiasi kikubwa – kwa vigezo vyangu – kitendo hicho, licha ya mazingira yaliyokisababisha, kinamvusha daraja na kumwingiza katika kundi la mashujaa wa kisiasa katika Tanzania ya sasa. Kimsingi, Lowassa ndiye aliyevunja Baraza la Mawaziri!

Kikwete aliyeshindwa mtihani wa kwanza, amepewa mtihani mpya. Amepewa fursa nyingine kujaribu. Akishindwa naye tunamtimua!

Hatutarajii atujazie sura zile zile katika baraza jipya. Tanzania haina upungufu wa watu wenye akili, ujuzi na uadilifu.

Hatutarajii rais atuteulie watu asiowafahamu vizuri, halafu baadaye ajiunge nasi kuwalaumu na kuwasimanga majukwaani kama alivyokuwa anafanya kwa hawa waliopita, huku akiogopa kuwatimua.

Rais ateue wachapakazi, si wapiga porojo na wachekeshaji. Wanaweza kuwa vijana au wazee, lakini asituletee wale wale wanaotuhumiwa kuharibu huko walikotoka.

Na asipoteze pesa zetu kuwapeleka Ngurdoto kuwapa semina elekezi. Imedhihirika kwamba licha ya kutumia mabilioni hotelini, mwalimu wao na wao wenyewe walipoteza pesa yetu hotelini. Hawakujifunza lolote Ngurdoto.

Tunatarajia baraza dogo la mawaziri wachache wachapakazi. Muda wa kugawiana vyeo na kupeana shukrani ya uchaguzi umepita. Kikwete ajisahihishe. Hasara za baraza kubwa zilikuwa nyingi kuliko faida alizotutajia wakati anaunda hili ‘lililovunjwa na Lowassa.’

Tayari tumeshaanza kumtazama Waziri Mkuu mpya, Mizengo Pinda. Tunamjua. Na huko alikotoka tunakujua. Hatuna sababu ya kumhukumu kabla hajaanza kazi.

Tutampongeza, lakini ajue kuwa tunajua matatizo ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) alikotoka – hasa kwenye halmashauri zetu.

Tumemsikia akiomba kura na kushukuru baada ya kuidhinishwa na wabunge. Tumemsikia akiwataja waliomlea kisiasa. Tunataka kuamini kwamba watu hao hawakumharibu!

Tumesikia ombi lake kwamba tumwambie ukweli kwa mambo yatakayokwenda kombo. Tunaamini limemtoka moyoni. Tutasema.

Amekiri kwamba yeye si mwanasiasa mzoefu. Tunajua. Lakini ni vema ajue kwamba humo alimoingizwa ndimo walimo wazoefu. Asipowashinda, atajiunga nao. Asipowabadili, watambadili yeye.

Napenda kumpongeza Mheshimiwa Mizengo Pinda kwa uteuzi wake. Namwambia kile anachokijua kwamba ameingia serikalini wakati mbaya. Tutampa muda wa kumpima, lakini hautakuwa mrefu.

Na tutaanza hivi karibuni kwa ripoti ya wakaguzi kuhusu ubadhirifu wa pesa zetu katika Benki Kuu. Huu ndio mtihani wake wa kwanza. Likimshinda hilo, tutajua naye ameanza kuwa mzoefu kama hao waliomfundisha siasa.

Anajua Bunge linataka ripoti. Hakuna cha ‘mashauriano na serikali’. Bunge likitaka ripoti serikalini, lipewe. Atuonyeshe umakini na ujasiri wake sasa, amwondolee Spika woga uliomfanya aanze ‘kujadiliana’ na serikali badala ya kuagiza apewe ripoti.

Pili, waziri mkuu amshauri rais sasa ateue watendaji wapya wizarani, hasa katika zile zinazoguswa moja kwa moja na hoja iliyovunja baraza lililokuwapo. Wasipoteuliwa sasa, Pinda ahesabu kwamba naye tayari kaingizwa mjini mapema.

Tatu, asimamie kwa kasi isiyo ya kawaida utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati ya Bunge kama yalivyotolewa na Kamati ya Mwakyembe. Utekelezaji huo uanze sasa kabla hajalewa madaraka na ‘kuharibiwa.’

Kama atatoa ushauri wake huo na rais akaukataa, Pinda ajiuzulu mapema, tujue anapinga ufisadi. Tutampongeza.

Ndiyo! Tunachojua kwamba kwa nafasi aliyopewa sasa, Pinda anakwenda kuwa mtekelezaji na msimamizi wa maelekezo ya rais. Na hapo kuna mawili.

Unapokuwa chini ya rais anayeogopa kuchukua uamuzi, huku wewe ukiwa na mamlaka ya kuchukua uamuzi, usipochukua uamuzi, hakuna kitakachofanyika.

Na ukiwa mtendaji, na katika mazingira tata kama haya ya Richmond, ujue yatakupata kama yaliyomkuta Lowassa. Pinda yuko tayari kwa lipi?

ansbertn@yahoo.com www.ngurumo.blogspot.com
 
I Think Muungwana Had No Choice On This Matter,as Much As He Wants Wananchi To Think That He's Deliberately Doing All This For Our Good!!
Mkono Ukibanwa Lazma Utaachia
 
Kama Anataka Pongezi Zaid Akamfwate Raisi Mwanawasa Ampe Siri Ya Kuachana Na Mafisadi Akamuulize Ex Presidaaaaaaa Chhiluba Nini Kinaendelea Hakika Fisadi Chenge Ahtokaa Asimame Na Kuongea Utumbo Kwa Jamii Yetu Akifwata Nyanyo Za Mwanawasa
Asikate Tamaa....kitu Kidogo Aondoe Kinga Zile Mzee
 
Back
Top Bottom