Kikwete Anafanya Kweli

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,240
3,911
Baada ya kusikiliza kwa umakini saga linaloendelea sasa hivi, naona pongezi za dhati zimuendee pia JK, kwani bila yeye kuridhia sidhani kama haya yote yangetokea.

Utakumbuka kuwa kamati mbali mbali za uchunguzi za serikali ziliwahi kufanywa hapo kale, especially wakati wa Mkapa lakini zilikaliwa na hazikuufanyiwa kazi yeyote.

muda mfupi aliokuwepo JK madarakani tunaona matokeo ya kamati tofauti, na ijulikane kwamba, kuundwa kamati hii, kulitokana direct na muongozo wa JK kwa six. Nani asiyojuwa kuwa six kwa maamuzi yake binafsi asingethubutu kuunda kamati. kama ajulikanavyo ni mshabiki wa ccm hata inapokosea na kama ilivyodhihirika jana kuwa, alimtonya EL baada ya kupokea hiyo taarifa kutoka kwa kamati, na EL ndio akaona mambo mabaya na kumuandikia six kujitetea wakati ni too late. kwa misingi hiyo, ni uhakika kuwa six, alimtonya pia JK na akaambiwa weka mambo yote wazi. Na kutokana na matamshi ya JK katika hotuba zake za hivi kARIBUNI, huko pemba na Dodoma, ni wazi kabisa JK alikuwa anajuwa what is happening...

Nadhani kuna haja kubwa ya kumpongeza JK kwa ujasiri wa kubadilisha mambo haraka haraka. JK ieleweke, anamtihani mkubwa wa kuiweka sawa system. HONGERA JK, ni Rais wa kwanza Tanzania ambae tunaona kamati zake zikifanya kazi inavyotakiwa, ukianzia ya zombe, hii, tunangoja ya Buzwagi na BoT. Jee, unaijuwa system ni nini?
 
Mawaziri. wawe wawili au mia mbili si hoja, hoja ni Jee, wanafanya walilotakiwa walifanye?
 
Sjui kama kweli anastahili pongezi. Jamaa ametumia hii issue kujirudishia umaarufu wake baada ya kuona meli yake inaanza kuzama. Offcourse ana ujasili ambao nafikiri hata Nyerere hakuuonyesha wa kuweka mambo wazi namna hii. Tulifikia mahali ambapo hatukutegemea kuwa haya yanaweza kutokea Bongo. Nitamsifu pale atakapounda kamati kwenye ussues zote zenye utata kuanzia IPTL, BOT nk. na kuzifanyia kazi hizo ripoti. Kama mambo yataishia hapo bila hatua za kisheria kuchukuliwa itakuwa ni yaleyale mazingaombwe ya CCM chini ya uongozi wake JK!!!
 
JK hajafanya chochote hii ilikuwa ni nguvu ya umma ,ndio inalazimisha haya mambo kuwepo .

mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, kwani huu umma ulikuwa haupo wakati wa nyerere, mwinyi na mkapa? mbona hatukuona yakitokea haya yanayotokea sasa? Hakika anastahili pongezi na bado mengine mengi yanakuja systematically.
 
Baada ya kusikiliza kwa umakini saga linaloendelea sasa hivi, naona pongezi za dhati zimuendee pia JK, kwani bila yeye kuridhia sidhani kama haya yote yangetokea.

Utakumbuka kuwa kamati mbali mbali za uchunguzi za serikali ziliwahi kufanywa hapo kale, especially wakati wa Mkapa lakini zilikaliwa na hazikuufanyiwa kazi yeyote.

muda mfupi aliokuwepo JK madarakani tunaona matokeo ya kamati tofauti, na ijulikane kwamba, kuundwa kamati hii, kulitokana direct na muongozo wa JK kwa six. Nani asiyojuwa kuwa six kwa maamuzi yake binafsi asingethubutu kuunda kamati. kama ajulikanavyo ni mshabiki wa ccm hata inapokosea na kama ilivyodhihirika jana kuwa, alimtonya EL baada ya kupokea hiyo taarifa kutoka kwa kamati, na EL ndio akaona mambo mabaya na kumuandikia six kujitetea wakati ni too late. kwa misingi hiyo, ni uhakika kuwa six, alimtonya pia JK na akaambiwa weka mambo yote wazi. Na kutokana na matamshi ya JK katika hotuba zake za hivi kARIBUNI, huko pemba na Dodoma, ni wazi kabisa JK alikuwa anajuwa what is happening...

Nadhani kuna haja kubwa ya kumpongeza JK kwa ujasiri wa kubadilisha mambo haraka haraka. JK ieleweke, anamtihani mkubwa wa kuiweka sawa system. HONGERA JK, ni Rais wa kwanza Tanzania ambae tunaona kamati zake zikifanya kazi inavyotakiwa, ukianzia ya zombe, hii, tunangoja ya Buzwagi na BoT. Jee, unaijuwa system ni nini?

Zomba siyo kweli Kikwete maamuzi yake ni tofauti na ya zamani (ya mkapa), bali sasa hivi ni tofauti tu kwa kuwa wananchi hawawezi kudanganywa muda wote, na sasa imeshafikia kikomo; sasa hivi tanzania anything can happen! wananchi wamechoka na JK anataka urais 2010.
 
Mawaziri. wawe wawili au mia mbili si hoja, hoja ni Jee, wanafanya walilotakiwa walifanye?

Utendaji wa mawaziri wetu tunaujua wala hauwezi kubadilika leo. Watendaji wazuri ni wachache. Balaza likiwa kubwa gharama za uendeshaji vilevile ni kubwa. Bora aje na balaza dogo lenye watendaji wazuri. Safari hii Nasali mama Meghji asipewe wizara ya fedha. Mama hana uwezo. Wizara inhitaji mtu makini na mwenye ideas.
 
Mawaziri. wawe wawili au mia mbili si hoja, hoja ni Jee, wanafanya walilotakiwa walifanye?

Utendaji wa mawaziri wetu tunaujua wala hauwezi kubadilika leo. Watendaji wazuri ni wachache. Balaza likiwa kubwa gharama za uendeshaji vilevile ni kubwa. Bora aje na balaza dogo lenye watendaji wazuri. Safari hii Nasali mama Meghji asipewe wizara ya fedha. Mama hana uwezo. Wizara hii inahitaji mtu makini na mwenye ideas.
 
Mawaziri. wawe wawili au mia mbili si hoja, hoja ni Jee, wanafanya walilotakiwa walifanye?

eh!? :confused: hata akiwa na baraza la mawaziri 200 si hoja!!!? Duh! hajafanya lolote la kupewa hongera. Kulikuwa na ushahidi wa kutosha tangu mwanzoni mwa mwaka jana kuhusiana na ufisadi wa baadhi ya mawaziri wake lakini hakufanya lolote. Sasa tumpe pongezi ya nini? hata kuwafukuza kazi ameshindwa! kwa kuogopa hisani waliomfanyia ili aingie Ikulu.
 
Mawaziri. wawe wawili au mia mbili si hoja, hoja ni Jee, wanafanya walilotakiwa walifanye?

eh!? :confused: hata akiwa na baraza la mawaziri 200 si hoja!!!? Duh! hajafanya lolote la kupewa hongera. kulikuwa na ushahidi wa kutosha tangu mwanzoni mwa mwaka jana kuhusiana na ufisadi wa baadhi ya mawaziri wake lakini hakufanya lolote. Sasa tumpe pongezi ya nini? hata kuwafukuza kazi ameshindwa! kwa kuogopa hisani waliomfanyia ili aingie Ikulu.
 
Mawaziri. wawe wawili au mia mbili si hoja, hoja ni Jee, wanafanya walilotakiwa walifanye?

Je unaweza kunifafanulia mchanganuo wa kumaintain waziri mmoja?

Je VX moja ni kiasi gani?

Je anapata watumishi wangapi?

Je anapata kiasi gani?

Mlinzi analipwaje?

Analipiwa nyumba kiasi gani na kodi za wananchi?

Analipwa basic salary kiasi gani?

Posho zake kiasi gani?

TOTAL NI KIASI GANI KWA WAZIRI MMOJA

x 60 ni kiasi gani?

by the way hapo hatujaongelea makatibu wakuu

Bado tuu huoni umuhimu wa kupunguza baraza la mawaziri? Ama kweli kazi tunayo yaani humu humu JF bado tuna watu kama wewe ambao mnaona sawa kuwa na baraza la mawaziri 60!

whats wrong with you people? yaani hamuwezi kutofautisha mchele na pumba?
 
Safi sana Bugurunikwawanyama. Kitu watu hawaelewi ni kwamba hawa mawaziri kuwa wengi ni mojapo ya mbinu za ufujaji wa hela. Multiply hao mawaziri na manaibu wao na masekretari kisha reflect that on the dollar amount it will cost the people of Tanz.Figure utakayofikia inatisha nad those monies could be used in improving the welfare of the commoners.

Kisha pia hawa jamaa wakiwa wengi kutakua na duplication of duties na wengine watakua hawana la kufanya kabisa.We need a comopact cabinet that is bent on uchapaji kazi na kuweka maslahi ya wabongo mbele.Hizi ni ofisi za uma and not a private enterprise!
 
Zomba sorry are you serious kwamba tunapaswa kumpongeza Kikwete kwenye hili? Kama ndivyo unachomaanisha then I beg to completely differ with you.

In my very honest JK ndio mwenye kulaumiwa kwenye hili kwani yeye ndio mwenye serikali. Infact matarajio yangu ni kwamba kama kweli JK ni muungwana basi baada ya hili sakata kwisha atatuomba radhi wananchi kwa kitendo cha serikali yake kufanya kinyume cha yale tuliyowatuma kuyafanya. Kwani tuliwapa kazi ya kulinda rasilimali za nchi yeye wamekuwa wa kwanza kuzifisadi.

Namwangalia Rais kama ndio CEO (Chief Executive Officer) pamoja na kwamba PM ndio kiongozi mtendaji wa shughuli za kila siku za serikali lakini rais ndiye anayemteua PM.Kwenye taaluma ya management inaaminika kwamba CEO ndiye anayeshape organization sasa katika hili Rais ndiye anayeishape serikali. Kwa msingi huo usipokuwa na rais makini usitarajie pia kuwa na serikali makini ni ngumu sana. JK tulimweleza sana kuhusu urafiki kazini,tulipinga sana kumteua EL kama PM kwa hofu hiyo ya urafiki kufanywa kichaka cha maouvu na haya ndio yaliyotokea sote tu mashahidi dhahiri.Waingereza wana msemo wa o 'Show me your friends then I will tell you who you are' Kwa maoni yangu kwa katiba kama hii yetu ni sahihi kabisa kusema 'Show me your government then I will tell you the kind of president you have'Matendo ya serikali yetu yanaeleza aina ya rais tuliyenaye,hawezi kupinga hili kwani ni yy ndiye anayeteua na kufukuza. Tumepiga sana kelele kuhusu EL JK akaweka pamba masikioni so kwa hili JK anahusika pia kwa kutochukuwa hatua.
 
eh!? :confused: hata akiwa na baraza la mawaziri 200 so hoja!!!? Duh! hajafanya lolote la kupewan hongera. kulikuwa na ushahidi wa kutosha tangu mwanzoni mwa mwaka jana kuhusiana na baadhi ya mawaziri wake lakini hakufanya lolote. Sasa tumpe pongezi ya nini? hata kuwafukuza kazi ameshindwa! kwa kuogopa hisani waliomfanyia ili aingie Ikulu.

True...kama ni pongezi labda kwa kukubali uamuzi wa besti wake kutema mzigo,lakini ile tume iliundwa na Spika,na ikawasilisha report bungeni...matokeo ye report ni kuwa PM ni mwizi na kalitia taifa hasara,yeye PM akaamua kuachia ngazi,raisi alikuwa na kazi ya kukubali tu uamuzi wake,sasa pongezi zikae wapi hapo?
 
Zomba sorry are you serious kwamba tunapaswa kumpongeza Kikwete kwenye hili? Kama ndivyo unachomaanisha then I beg to completely differ with you.

In my very honest JK ndio mwenye kulaumiwa kwenye hili kwani yeye ndio mwenye serikali. Infact matarajio yangu ni kwamba kama kweli JK ni muungwana basi baada ya hili sakata kwisha atatuomba radhi wananchi kwa kitendo cha serikali yake kufanya kinyume cha yale tuliyowatuma kuyafanya. Kwani tuliwapa kazi ya kulinda rasilimali za nchi yeye wamekuwa wa kwanza kuzifisadi.

Namwangalia Rais kama ndio CEO (Chief Executive Officer) pamoja na kwamba PM ndio kiongozi mtendaji wa shughuli za kila siku za serikali lakini rais ndiye anayemteua PM.Kwenye taaluma ya management inaaminika kwamba CEO ndiye anayeshape organization sasa katika hili Rais ndiye anayeishape serikali. Kwa msingi huo usipokuwa na rais makini usitarajie pia kuwa na serikali makini ni ngumu sana. JK tulimweleza sana kuhusu urafiki kazini,tulipinga sana kumteua EL kama PM kwa hofu hiyo ya urafiki kufanywa kichaka cha maouvu na haya ndio yaliyotokea sote tu mashahidi dhahiri.Waingereza wana msemo wa o 'Show me your friends then I will tell you who you are' Kwa maoni yangu kwa katiba kama hii yetu ni sahihi kabisa kusema 'Show me your government then I will tell you the kind of president you have'Matendo ya serikali yetu yanaeleza aina ya rais tuliyenaye,hawezi kupinga hili kwani ni yy ndiye anayeteua na kufukuza. Tumepiga sana kelele kuhusu EL JK akaweka pamba masikioni so kwa hili JK anahusika pia kwa kutochukuwa hatua.

Safi sana Bobby kwa kutupa huo mtazamo.By the way swali linakuja hivi nani kampa PM kazi yake?That person is accountable to whoever appointed him a'fu pia the one who appointed him needs to check on their performance ama?Kwa hivyo mtazamo wangu ni kua JK has a big level of responsibility on what happens in the country.Tuambiani ukweli na tuache uzalendo wa kipuzi.
 
Mawaziri. wawe wawili au mia mbili si hoja, hoja ni Jee, wanafanya walilotakiwa walifanye?

Utendaji wa mawaziri wetu tunaujua wala hauwezi kubadilika leo. Watendaji wazuri ni wachache. Balaza likiwa kubwa gharama za uendeshaji vilevile ni kubwa. Bora aje na balaza dogo lenye watendaji wazuri. Safari hii Nasali mama Meghji asipewe wizara ya fedha. Mama hana uwezo. Wizara hii inahitaji mtu makini na mwenye ideas.
 
mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, kwani huu umma ulikuwa haupo wakati wa nyerere, mwinyi na mkapa? mbona hatukuona yakitokea haya yanayotokea sasa? Hakika anastahili pongezi na bado mengine mengi yanakuja systematically.

Mimi kwa upande wangu siwezi kumpa JK pongezi kwa hili,kwa kuwa hakuna alichofanya.Saana nitampa Zitto na Watanzania na Mwakyembe na kamati yake.Issue ya baada ya Zitto ndo imewafanya CCM waakubali ukweli baada ya wananchi kuonyesha wazi kuanza kuwakataa CCM hadharani kwa kuwazomea.Hii ilikuwa SMS tosha kwa CCM kuwa Wananchi wanafahamu mengi zaidi kuliko wao wanavyofikiria.
Nyerere Mambo yake mengi alikuwa muwazi na alikuwa hasubiri kuunda vikamati kila kukicha hata kwenye masuala ambayo yapo wazi.Yeye alikuwa mtu wa kuchukua hatua. mf.Jumbe na Seif wote walitolewa mara moja.

Huwezi linganisha wakati wa Nyerere na Sasa. Sasa hivi Viongozi wamekuwa majambazi mno, hata viongozi wakuu na wamekuwa hawachukui hatua kiasi cha kutufanya wananchi tufungue macho na masikio zaidi. Umma wa Tanzania umewalazimisha kufanya haya.Jk hana ubavu wa kuamua EL achunguzwe ni mnafiki anatumia migongo ya watu.
 
Baada ya kusikiliza kwa umakini saga linaloendelea sasa hivi, naona pongezi za dhati zimuendee pia JK, kwani bila yeye kuridhia sidhani kama haya yote yangetokea.
QUOTE]

Namuunga mkono Zomba. JK anastahili pongezi katika hili. Sina shaka nguvu ambayo Mwakyembe alikuwa nayo kwa kuweka ripoti kama hiyo hadharani na kwa staili ile kulikuwa na blessing ya JK. Hiyo ilikuwa nafasi nzuri kwake vilevile kuondoa uozo bila mikwaruzo na swahiba wake (Uso umeumbwa na aibu, wametoka mbali, alichangia vilivyo kuwepo kwake madarakani).

Vilevile tu-acknowledge kwamba sytem nzima aliyoikuta kikwete (ya BWM) ilikuwa imeoza kwa ufisadi, rushwa na ubabe na abrupt changes zingeweza kuleta matatizo makubwa (Wakati huo). Sasa atakuwa kajipanga sawa. Ana system yake (At leat backup portion). Ni mategemeo yangu ataleta baraza dogo la utendaji na uadilifu. Sitarajii tena kuwaona Kingunge, Mungai, and the like.
 
Bobby, Nakubaliana na wewe kwa kokoti mmoja ya taarifa hizi
"Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais, Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.

Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika." Source, http://www.chadema.net/habari/2007/orodha1/ukurasa10.php ,Kama hii ni kweli kuna haja gani ya kuwa na imani na Mhe. JK ikiwa hata yeye pia ni Fisadi.
 
Back
Top Bottom