hata hazihitajiki kufika hamsini, watu ni kufikiri kitu kidogo tu..toka 2005 mpaka leo kuna nini mtanzania anaweza akasema kafaidika au kaona impact ya utawala huu?.tumeona Obama kaja tu juzi unaona kaanza kuweka health care reforms na mambo mengine mengi. Kwa JK hakuna jipya nchi ipoipo tu.....
Haya mambo muulize Nkapa! JK anajitahidi kurekebisha uozo wake..sasa contract iliyofanyika kisheria huwezi kuzivunja bila kufuata taratibu za kisheria...labda kama unataka awe dicteta...na huo si ushauri mzuri ndio hajishughulishi na watu kama nyinyi
Usisahau kwamba JK aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Fedha,..., kwa hiyo Mkataba ya Madini sio migeni kwake!
ha ha ha ... dicteta
mkataba wa barrick buzwagi nao uliandikwa na mkapa!!!!!
Baada ya kutafakari sana, nimepata sababu 51 za kwanini Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama chetu Cha Mapinduzi aamue kutoshiriki kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu mwakani. Ninajua kwamba ni "mtaji" kwa upande wa kina Makamba na vile vile ana "sura nzuri" na bla bla bla..
Sasa kati ya hizo 51 nitaanza na zile mbili za mwisho yaani ya 50 na 51. Bila ya shaka na wewe unaweza kuwa na za kwako.. hivyo nawakaribisha wale ambao wanaweza kukisikia au kuchangia sababu zile nyingine 49!
51: Alisema kuwa akichaguliwa tena ataleta vijana na kuwa watu wa rika "lake" waanze kuachia ngazi. Well, kwa vile yuko rika moja nao basi na yeye aungane nao!
50: Hajui kwanini Tanzania ni maskini licha ya kuwa kwenye utumishi wa serikali kwa karibu miaka 30 sasa! Kiongozi asiyejua chanzo cha tatizo ataweza vipi kuliondoa isipokuwa kuziba tu dalili zake.
49: Aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania. Ahadi hii haionekani kutekelezeka. Inaonekana ametimiza ahadi ya maisha bora kwa kila muwekezaji wa kigeni!
48:Alitangaza kuwa wizi umefanyika Benki Kuu kwa kukombwa mabilioni; badala ya kuacha uchunguzi wa jinai akaunda Kamati kuchunguza jinai. Matokeo yake ni kucheleweshwa kwa upatikanaji wa haki.
47: Serikali yake imeshindwa kutekeleza maazimio yote ya wananchi wa Tanzania kama yalivyoanishwa na wawakilishi wao Bungeni katika maazimio kufuatia Kamati Teule ya Kuchunguza Richmond. Matokeo yake ni kuchochea mgawanyiko mkubwa kabisa wa kimaslahi katika historia ya taifa letu.
46: Aliahidi kupitia mikataba yote mikubwa ya madini ili kutengeneza hali ya "win win win". Hadi hivi sasa hakuna mkataba hata mmoja uliopitiwa na kusahihishwa na badala yake serikali yake imetangaza kuwa mabadiliko ya sheria ya madini yataendelea kuwanufaisha wawekezaji wa sekta hiyo.
45: Akiwa ni Mwenyekiti wa Chama Tawala ameshindwa kuleta nidhamu ndani ya chama na matokeo yake wanachama wake mashuhuru wanatukanana na kuitana majina hadharani. Kile kilichoitofautisha CCM miaka ya nyuma sasa hakipo tena.
44: Aligawa fedha za walipa kodi wa Tanzania kwa kile kilichojulikana kama "mabilioni ya Kikwete" Hadi hivi sasa haijaoneshwa ni kiasi fedha hizo zimeweza kubadilisha maisha ya waliozipata na kurudisha faida.
43: Aliahidi kuunda Baraza dogo la Mawaziri lakini matokeo yake Baraza lake limekuwa kubwa na lenye ufanisi mdogo.
42:
Mzee Mwanakijiji, kwanza nimefurahi kutuweka wazi kuhusu 'chama chenu'. Taratibu za chama chenu kutoa malalamiko unazijua, wewe kama mwanachama mtiifu, kwanini unamvua nguo Mwenyekiti wako wa Chama na rais wako kulikopelekea kumuacha utupu na hivyo kupata matukano, kubezwa, kuchekwa na hata kudhihakiwa hivi?.Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama chetu Cha Mapinduzi.
[/SIZE][/FONT][/B]
Kwa maoni yangu, CCM is a gone case, kwa upinzani huu legelege tulionao, bado ni CCM tuu itaendelea kutuswaga mpaka watu wenye uelewa na uono wa type ya Mwanakijiji, watakapokubali to have a look outside the box.
Baada ya kutafakari sana, nimepata sababu 51 za kwanini Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama chetu Cha Mapinduzi aamue kutoshiriki kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu mwakani. Ninajua kwamba ni "mtaji" kwa upande wa kina Makamba na vile vile ana "sura nzuri" na bla bla bla..
Sasa kati ya hizo 51 nitaanza na zile mbili za mwisho yaani ya 50 na 51. Bila ya shaka na wewe unaweza kuwa na za kwako.. hivyo nawakaribisha wale ambao wanaweza kukisikia au kuchangia sababu zile nyingine 49!
51: Alisema kuwa akichaguliwa tena ataleta vijana na kuwa watu wa rika "lake" waanze kuachia ngazi. Well, kwa vile yuko rika moja nao basi na yeye aungane nao
50: Hajui kwanini Tanzania ni maskini licha ya kuwa kwenye utumishi wa serikali kwa karibu miaka 30 sasa! Kiongozi asiyejua chanzo cha tatizo ataweza vipi kuliondoa isipokuwa kuziba tu dalili zake.
49: Aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania. Ahadi hii haionekani kutekelezeka. Inaonekana ametimiza ahadi ya maisha bora kwa kila muwekezaji wa kigeni!
48:Alitangaza kuwa wizi umefanyika Benki Kuu kwa kukombwa mabilioni; badala ya kuacha uchunguzi wa jinai akaunda Kamati kuchunguza jinai. Matokeo yake ni kucheleweshwa kwa upatikanaji wa haki.
47: Serikali yake imeshindwa kutekeleza maazimio yote ya wananchi wa Tanzania kama yalivyoanishwa na wawakilishi wao Bungeni katika maazimio kufuatia Kamati Teule ya Kuchunguza Richmond. Matokeo yake ni kuchochea mgawanyiko mkubwa kabisa wa kimaslahi katika historia ya taifa letu.
46: Aliahidi kupitia mikataba yote mikubwa ya madini ili kutengeneza hali ya "win win win". Hadi hivi sasa hakuna mkataba hata mmoja uliopitiwa na kusahihishwa na badala yake serikali yake imetangaza kuwa mabadiliko ya sheria ya madini yataendelea kuwanufaisha wawekezaji wa sekta hiyo.
45: Akiwa ni Mwenyekiti wa Chama Tawala ameshindwa kuleta nidhamu ndani ya chama na matokeo yake wanachama wake mashuhuru wanatukanana na kuitana majina hadharani. Kile kilichoitofautisha CCM miaka ya nyuma sasa hakipo tena.
44: Aligawa fedha za walipa kodi wa Tanzania kwa kile kilichojulikana kama "mabilioni ya Kikwete" Hadi hivi sasa haijaoneshwa ni kiasi fedha hizo zimeweza kubadilisha maisha ya waliozipata na kurudisha faida.
43: Aliahidi kuunda Baraza dogo la Mawaziri lakini matokeo yake Baraza lake limekuwa kubwa na lenye ufanisi mdogo.
Kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, haki ya raia kushiriki politics haipo, imemezwa na sheria kwamba lazima upitie kwenye chama cha siasa.Jamani tuseme kwamba CCM hatuiwezi kuifukuza madarakani, tusilete visingizio.Hivi ni ulegelege gani huo ambao upinzani unao ambao CCM hawana?
Okay, kama wapinzani ni legelege, vipi makundi mengine? Walio wanachama wa vyama vya siasa Tanzania hawazidi milioni 6, kati ya wapiga kura milioni zaidi ya 18, vipi makundi mengine yanafanya nini, au na yenyewe ni legelege? Kote huko ambapo vyama tawala viling'olewa havikung'olewa na vyama vya upinzani pekee. In fact vyama vya upinzani viltumika kama tu'vehicles'; waliongoza mapamabano (Kenya, Zambia, Malawi, etc) walikuwa ni vyama vya kiraia, mashirika ya dini, wafanyakazi, wanafunzi, wasomi na vyama vyao vya kitaaluma, n.k. Kwetu vipi haya makundi yanafanya nini?
Sisi tumebaki kulaumu vyama vya upinzania kama vile ndivyo vyenye jukumu pekee la kuleta ukombozi katika nchi hii.
Hapa tulipofikia, anybody can be better than CCM. Hawa jamaa wameperform at the lowest level you can imagine. Sasa kama tunaona hawa bado ni bora kuliko mtu mwingine, then inabidi tukiri kwamba sisi kama nchi tupo hoi kabisa kiuwezo. then we need to shut up!
But I don't believe so; Tuache woga, CCM inang'oleka, play your part!