Kwanza nawataka radhi wadau wa JF kwa kuchelewa kutoa maoni yangu. Hat hivyo, pia napenda kumpongeza mwanakijiji kwa kufafanua kwa ufasaha kabisa sifa zinazoonyesha mapungufu ya Kikwete kushiriki uchaguzi mkuu ujao kama mgombea kwa kiti cha Urais.
Sifa kubwa inayoonyesha Kikwete kutofaa kuwa mgombea wa Urais uchaguzi wa mwakani ni "KUKOSA DIRA YA KULIONGOZA TAIFA". Hayo yote aliyoyataja Mkjj yamemezwa ndani ya hili lililoandikwa kwa maandishi makubwa. Mfano, utamuona anapoenda nje ya nchi (Kikwete), hotuba zake kwanza ni ndefu pasipo sababu maana zinaongelea upuuzi tu. Haziongelei kile Watanzania wanachokihitaji ili kujinasua na umasikini ambao ni takribani miaka 50 sasa imekaribia tangu Uhuru. Juzi nilikuwa nachangia hoja moja nikatolea hotuba zake za Cuba na Italia alizozitoa mwaka huu! Hakika ni kutuaibisha sisi anaotuwakilisha kutosema vitu ambavyo Tanzania inavihitaji vifanyike ili watu wake waendelee kiuchumi, kijamii na kisiasa. Vyote vinavyosemwa havina dira kabisa. Ni kule kujaribu kutatua tatizo kumbe hujui tatizo lenyewe ni nini na badala yake unaishia tu kukata majani na kuacha mizizi ikinawilisha mti kama kawaida.
Tunahitaji mtu anayefahamu matatizo ya nchi yetu ili hata akiwa anasikiliza ushauri wa kitaalamu naye aweze kupima kama ushauri husika unafaa au haufai kulingana na matatizo menyewe. Wewe utaona wapi kusema mataifa waje kuwekeza nchini wakati nchi iko gizani? Wawekeze, je bidhaa zao zitanunuliwa na akina nani wakati watanzania waliowengi wanaishi chini ya dolla maja kwa siku?
Kwa Kikwete kuwa na matatizo haya yote, ndiyo maana sasa hivi hata mfumko wa bei umefikia 18%, hebu linganisha na kipindi kabla hajaingia! Hivyo, mfumko wa bei kuwa juu, maana yake ni kwamba watanzania waliowengi sasa wameathirika zaidi na kipato chao duni maana uwezo wa kununua sasa umekwenda chini zaidi kwa kipato kilekile cha awali. Hajui hilo, kwamba ni tatizo! Inabidi tupate mtu mbadala, sasa ili kufanikiwa katika hili ni Kumuomba MUNGU kwa nguvu zetu zote zilizobaki kabla ya uchaguzi mkuu ujao.