Chakaza
Platinum Member
- Mar 10, 2007
- 41,011
- 74,659
Mchungaji, amani ya bwana iwe nawe.M.M.
Mimi mgombea wangu ni Maximo!
Mchungaji, amani ya bwana iwe nawe.M.M.
Mimi mgombea wangu ni Maximo!
Tatizo ni je, huyo atakayekuja atafaa? Uwezo wa watanzania wengi kuchagua kiongozi mzuri bado unaathiria na mambo mengi sana kiasi kwamba mara nyingi, wanaishia kuchaguliwa viongozi na si wao kuchagua-kama ilivyotolea kwa Kikwete mwenyeweHata kidogo; utaratibu wa kumpata mgombea wa CCM utafanyika kama vile ni mara ya kwanza; mwana CCM yoyote ambaye anaamini ana uwezo wa kuliongoza Taifa letu atajitokeza na kuchukua fomu na kufuata mchakato ule ule. Hadi hivi sasa JK inaonekana ameshapigiwa debe na viongozi wetu; lakini miezi michache ijayo atapata upinzani wa kihistoria na mwamko huo utakapoiva atakuja na sababu ya kwanini asigombee kama nilivyodokeza karibu miezi kadhaa iliyopita.
Tunamshukuru kwa utumishi wake lakini naamini hatokuwa na kinyongo pale ambapo mtu mwingine atapitishwa badala yake.
Gombea wewe tutakuunga mkono!Na. M. M. Mwanakijiji
Kuna watu wanajaribu kuwafanya wengine wajisikie vibaya wanapotoa mawazo yao kuwa Rais Kikwete afikirie adhma yake ya kugombea ngwe ya pili. Wanajaribu kuwafanya watu wajisikie kama wasaliti au waonevu wanapotoa mawazo kuwa Taifa letu linahitaji uongozi mpya kabisa mwakani na siyo wa Rais Kikwete. Ukweli ni kuwa watu wengi wanampenda Kikwete kama mtu binafsi; ana sura nzuri, sauti nzuri, tabasamu n.k n.k lakini linapokuja suala la uongozi wapo wanaoona kuwa ana mapungufu makubwa mno kiasi kwamba kumpa nafasi nyingine mwakani ni kuendeleza kile ambacho tayari kimeshaonekana miaka hii minne.
Tunapoelekea mwaka huu mpya ambao ni mwaka wa uchaguzi kambi za "kikwete agombee" na "Kikwete asigombee" zitazidi kuibuka na kwa mara ya kwanza tutashuhudia mgongano wa wazi kati ya kambi hizi. Tatizo kubwa ni la wale ambao wanaamini kuwa kutaka Rais aliyemadarakani asigombee tena ni sawa na uhaini na kumtaka afikirie kutokugombea ni sawa na kumsaliti.
Hii si kweli. Rais wa Tanzania anachaguliwa kwa kipindi kimoja tu na akitaka nafasi nyingine basi anapitia mchakato ule ule na hawezi kutawala kwa vipindi zaidi ya viwili. Katiba haisemi kuwa vipindi hivyo viwili ni lazima viwe vimefuatana. Kutokana na ukweli huu ni lazima watu wakubali kuwa utawala wa demokrasia una gharama yake na gharama mojawapo kubwa ni wananchi kuweza kumkataa kiongozi wao na hata kutaka asigombee!
Lakini wazo hili ni gumu kwa watu ambao wanaongozwa na ushabiki wa mtu; watu ambao wanaona kuwa Kikwete ame"fika" hapo kwenye Urais na mtu yeyote anayetoa mawazo kuwa asigombee au hana sababu ya kutosha kugombea tena basi ni kama mhaini; tumewasikia watu wazima na ambao ni wanasiasa wakongwe wakianza kutukuza huu ubia wa Bw. Kikwete na Urais wa Tanzania.
Wanataka kumfanya Kikwete kuwa ni mfalme na kuwa yeyote atakayejitokeza kupingana naye basi ni msaliti wa aina fulani au mhaini. Haya ni mawazo potofu. Kama watu hawa wanataka Kikwete agombee milele na kuwa hakuna mtu mwingine yeyote mwenye uwezo kumzidi basi wajitokeze hadharani na wabadili Katiba ili wamtangaze Kikwete kuwa ni Rais wa Maisha na sisi wengine tutakaa kimya (kwenye njozi zao).
Mwaka 2005 kinyume na inavyosemwa Kikwete hakupitia kwenye tanuru ya moto; hakuwa na rekodi ya kusimamia lakini safari hii bila ya shaka tunayo rekodi yake ya kutosha na tunaweza kumpima kwa kile alichokifanya kama Rais. Na ni kipimo hicho tu ndicho ambacho kitatuamulia kama ana sababu ya kugombea tena au tutafute mtu mwingine.
Safari hii Kikwete kama anataka kuwa Rais wetu tena itabidi ajibithibitishe kwa kufanya midahalo na wagombea wengine, kusimamia rekodi yake na kujibu hoja zitakazotolewa dhidi yake. Safari hii Urais hauji kwa kuuza jina, sura, au tabasamu; safari urais utakuja kwa kuustahili.
Na wana CCM ambao wanaona Rais Kikwete hawezi kuwa chaguo lao wasijisikie vibaya wala kujiona kama wanasaliti chama; watambue kuwa wana wito mkubwa zaidi na sababu kubwa zaidi na kama wanaona kuwa Bw. Kikwete anahatarisha hata maslahi ya Chama basi ni jukumu lao kutokumpendekeza na yeye kama Mkapa atakaa pembeni na kula pensheni yake na kuendelea kufurahia ving'ora na saluti za hapa na pale. Kama Gen. Powell aliweza kumuunga mkono Obama wakati yeye ni Republican na mtu aliyefanya kazi na marais wa Republican kama Reagan, Bush na GW Bush basi mwana CCM yeyote anaweza naye kumpendekeza mtu mwingine zaidi ya Kikwete.
Kwa upande wetu tutaendelea Jumatano hii kwenye gazeti la Mwanahalisi na fungu la pili la sababu 51 za kwanini Rais Kikwete asigombee. Ni matarajio yetu kuendelea kuwakera watu wachache na kuwaudhi wengi.
Na wana CCM ambao wanaona Rais Kikwete hawezi kuwa chaguo lao wasijisikie vibaya wala kujiona kama wanasaliti chama; watambue kuwa wana wito mkubwa zaidi na sababu kubwa zaidi na kama wanaona kuwa Bw. Kikwete anahatarisha hata maslahi ya Chama basi ni jukumu lao kutokumpendekeza na yeye kama Mkapa atakaa pembeni na kula pensheni yake na kuendelea kufurahia ving'ora na saluti za hapa na pale. Kama Gen. Powell aliweza kumuunga mkono Obama wakati yeye ni Republican na mtu aliyefanya kazi na marais wa Republican kama Reagan, Bush na GW Bush basi mwana CCM yeyote anaweza naye kumpendekeza mtu mwingine zaidi ya Kikwete.
Tatizo watanzania wengi, wanafikiri na kuota kuwa eti kwasababu marekani upinzani ulishinda eti na sisi mwakani iwe hivyo.siasa zetu bado sana, na kama MMM unataka kuabadili KIKWETWE kawnini mbadala asiwe memba wa CCM? na kuutaka upinzani? we piga kelele tu baba kampeni hizo. angalia trend yote ya maraisi wetu, kwa vipindi vyote watu walipiga kelele, kuanzia huyo Nyerere, hoo rais hafai, ohoo mkapa kimeo ,ohoo mwinyi nae mbona hivyo. kwa mantiki hiyo hata akija mpya we wlii hear the same song. tazama kenya kibaki si katoka kafanya nini? hao wenyeviti wa vyama vya siasa wamefanya nini? zaidi ya kulia ifisadi majukwaani bila kuchukua hatua madhubuti kama wanaevidence si wawapeleke mahakani? wenyewe kwa wenyewe wanalumambana, wako self centered. huyo zito yuko wapi sasa bado kidogo atakwenda CCM. siasa za bongo ni kuganga njaa asikwambie mtu. hivi MM unatumiwa na nani vile?
Wenye Chama mnatuletea mtu safi - another 'Mr. Clean'?
Mwanakijiji:
Urais ni wa wananchi, JK kapewa dhamana tu.
Mwanakijiji:
Urais ni wa wananchi, JK kapewa dhamana tu.
Whaaaat... ? so haitaji kuukoa Urais wa wananchi?
Unaishi wapi wewe? Uraisi wa Kikwete ni wa kifamilia zaidi!
acha tu aendelee kuboronga maana tushamchoka !
Si ajabu ukimuuliza JK atakuambia hajui kinachoendelea. Ana digree za usahaulifu. Cheki ahadi anazotoa. Hawezi kutoa mtu mwenye kumbukumbu mzuri, kwani ataogopa kudanganya.
Launch the countrys biggest crackdown on corruption and declare a rule of law. Strip Mkapas immunity in order to be prosecuted of corruption practices and theft of public funds. Fire Lowassa and Karamagi, then prosecute them of stealing our national resources. Fire the least effective 30 ministers, replicate policies that prove effective, give people the material and guidance to better their lives.