HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, AKIFUNGUA RASMI BUNGE JIPYA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DODOMA, 30 DESEMBA 2005
Nanukuu...
Mheshimiwa Spika:
Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 imetamka bayana majukumu mawili ya msingi ya Serikali ya Awamu ya Nne:.
· Kwanza, kuitoa Tanzania kutoka kwenye dimbwi la uchumi ulio nyuma na tegemezi na kuiingiza katika mkondo wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea.
· Pili, kuwashirikisha wananchi wote kwa njia ya uwezeshaji katika ujenzi wa uchumi na kuutokomeza umaskini.
Mheshimiwa Spika:
Kwa kuzingatia majukumu haya ya msingi, na mbinu na mikakati mbalimbali ya kuyatekeleza, Watanzania watarajie mambo kumi yafuatayo katika miaka mitano ijayo:
· Kwanza, Serikali ya Awamu ya Nne itahakikisha kuwa Amani, Utulivu na Umoja wa nchi yetu na watu wake vinadumishwa;
My opinion: hakuna Utulivu wala Umoja kitaifa
· Pili, Serikali ya Awamu ya Nne itadumisha na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza hadi leo;
My opinion: hakuna kilichodumishwa
· Tatu, Serikali ya Awamu ya Nne itaendeleza vita dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi, tena kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya;
My opinion: Tena hapa ndio amefeli kabisa
· Nne, Serikali ya Awamu ya Nne itatimiza ipasavyo wajibu wake wa utawala na maendeleo, na itaendesha dola kwa misingi ya utawala bora na uwajibikaji; utawala wa sheria unaoheshimu na kulinda haki za binadamu; itaendeleza mapambano dhidi ya rushwa bila ya woga wala kuoneana muhali.
My opinion: hivi kweli alikua anajua anachokisema..???
· Tano, Serikali ya Awamu ya Nne itaimarisha uwezo wake wa kulinda maisha na mali za raia wake. Tutapambana na uhalifu wa kila aina, na majambazi hayataachwa yatambe yatakavyo;
My opinion: hapa kachemsha vibaya sana
· Sita, Serikali ya Awamu ya Nne itahakikisha mipaka ya nchi yetu ipo salama. Hatutamruhusu mtu au nchi yeyote kuchezea mipaka ya nchi yetu na uhuru wetu;
My opinion: hivi suala la silaha zinazopita bila serikali kujua na bado mipaka yetu ipo salama??? kafeli tena hapa
· Saba, Serikali ya Awamu ya Nne itafanya kila iwezalo kuhakikisha Tanzania ina mahusiano mazuri na mataifa yote duniani, pamoja na mashirika ya kimataifa na kikanda;
My opinion: Pengine hili kalifanikisha kwa gharama kubwa sana,lakini vipi hii ripoti ya silaha haiwezi kutuweka kwenye nafasi mbaya ya kimahusiano na majirani zetu? nampa nusu maksi
· Nane, Serikali ya Awamu ya Nne itajali sana maslahi na mahitaji ya makundi maalum katika jamii kama vile wanawake, vijana, watoto, wazee, walemavu na yatima;
My opinion: Kashindwa kuwalinda maalbino na vikongwe
· Tisa, Serikali ya Awamu ya Nne itaongoza mapambano mapya ya kuhifadhi mazingira ili vizazi vijavyo virithi nchi nzuri, na msingi imara wa maendeleo endelevu;
My opinion: Jitihada haziridhishi...!
· Kumi, Serikali ya Awamu ya Nne itaendeleza michezo, na shughuli za utamaduni na burudani.
My opinion: Kwenye burudani sioni! utamaduni ndio unazidi kupotea! michezo hakuna kitu, watetezi wake watazungumzia soka! soka sio mchezo pekee!
Mwisho wa kunukuu.