Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,484
Kwa kadiri mambo yanavyokwenda na kwa kadiri siku zinavyokwenda ndivyo mzigo wa Matumaini ambao Rais Kikwete alichutuma kuubeba ndivyo unavyozidi kuwa mzito na unaozidi kumuelemea.
Kwa mtu yeyote ambaye anafuatilia hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi bila ya shata atatambua kuwa Rais Kikwete hawezi kuwa mwenye furaha. Bila ya shaka manung'uniko yanamkera na zaidi ya yote yale yanayoendelea kwenye Chama "chake". Mgongano wa mawazo unaoendelea kwenye vyombo vya habari, masuala ya mikataba ambayo watu walifikiria yameisha na Mkapa, siyo tu vimetia doa bali vimepaka rangi mbaya kabisa kwenye utawala wake.
Kikwete sasa hivi hana jinsi bali kucheza "pata potea". Anao uamuzi wa kuendelea na timu ile ile ya watu 60, na kutarajia mabadiliko kwa kutumia makaripio na barua za maonyo na uelekezaji, au anaweza kubadili mwelekeo wa utawala wake. Vyovyote vile atakavyofanya, Rais Kikwete anakabiliwa na mtihani mkubwa kabisa wa utawala wake hadi sasa.
Je, atakuwa ni Rais ambaye atashuhudia kumeguka kwa CCM? Je atakuwa ni Rais ambaye ameshindwa kuwadhibiti watu aliowateua na kusababisha kambi siyo kwenye chama tu bali pia kwenye utendaji?
Ana uchaguzi wa kuona ni jinsi gani anaweza kuokoa Urais wake, CCM na hatimaye yeye mwenyewe kutoka katika historia ambayo imeanza kuandikwa?
Afanye nini Rais Kikwete ili auokoe Urais wake, aiimarishe CCM, na zaidi ya yote aweze kutimiza ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania?

Fuatilia sababu 51 za kwanini Kikwete asigombee tena 2010 hapa