Kikwete afanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri - Aprili 2012

Haya yalisemwa na Filikunjombe, Halima Mdee, Zitto hasa yalilenga viongozi vijana ndani ya CCM specifically Makamba kutotia saini ni dhahili aliyajua haya

Kwamba kwa vyovyotw anajiona kama. Serikali na atakuja tiwa fitina akipata nyazifa aliyo kuwa anaililia mda wote.

Alianzisha na Zitto mwisho akakimbia baada ya kutonywa na usalama wa CCM kuwa itakuwa waziri nawe utawekwa kitimoto.

Na dalili tosha za kulindana kuwa na hata makamba akuharibu hakuna wa kumwajibisha coz ye hakuwawajibisha walipokosa.

Ndani ya ccm ni kulindana kwanza wananchi baadae
 
Iliyoniacha hoi ni waziri asiye na wizara maalum. Is it necessary to have such kind of ministry?
 
Watanzania mna moyo; mmekaa, mmeombea, mmesubiria na hatimaye mmepewa mlichotaka. Na nyinyi wa kwenye mitandao ndio mtakiona cha mtema kuni kwa kuisababisha CCM hasara sana 2010... sasa kichaa kapewa sime sokoni..

Huyo "kichaa" ndio huyo ninayemfikiria au ni mwingine....?
 
Iliyoniacha hoi ni waziri asiye na wizara maalum. Is it necessary to have such kind of ministry?

Mwandosya kwa Wanyakyusa hawaambiwi kitu kwanza wanamtegemea aje kuwa rais kwahiyo wamepima upepo na kuona kuwa Mbeya kutakuwa hakuendeki kwa wana CCM kama wangemwacha kabisa.
 
Rais ameteua kwa kuangalia vigezo gani:baby: Mtu kama Hawa Ghasia ambaye hana uwezo wa kujibu hoja za maandamano ya wafanyakazi unamuweka wizara yenye matatizo makubwa kama TAMISEMI nini kitatokea, ushauri wa bure ulikuwa ni kumpandisha Agrey kuwa waziri kamili hilo ni Jembe.
Acha tuone hilo baraza lililosukwa kama litatusaidia.
 
Sina shaka kusema kwa muda mrefu watanzania tumekuwa na shauku ya kupata watu makini ambao bila shaka wanaweza kuondoa kero za mfumuko wa bei,na matumizi machafu ya fedha za umma na kuleta tija au amasa ya utendaji ndani ya serikali na nje ya serikali, Kwa baraza hili Je ni chombo salama cha kuwafikisha watanzania wanapotaka kufika?
 
Watanzania mna moyo; mmekaa, mmeombea, mmesubiria na hatimaye mmepewa mlichotaka. Na nyinyi wa kwenye mitandao ndio mtakiona cha mtema kuni kwa kuisababisha CCM hasara sana 2010... sasa kichaa kapewa sime sokoni..

Nilikuwa Nimelalala Zangu sikuwa na Muda wa Kufuatilia koz sikutegemea La Maana.
 
Nyalandu Maliasili .... nimechoka kabisa

Ni vigumu kuamini kama hili ndilo baraza la kufufua CCM! Nyalandu atakuwa na ubavu mbele ya yule Kamran wa Pakistan? Na akiungana na Pius Msekwa au Kinana huko maliasili kuna kitu kitabakia kweli? Adam Malima na Kilimo wapi na wapi kama sio utani? Makama ana ujuzi gani kwenye science & technology kama sio kulinda maslahi ya wakubwa-vodacom ili waendelee kukwepa kodi?

Kwenye wizara ya fesha ndio nimechoka kabisa. CHADEMA wajipange maana hii penalti iko wazi.
 
Híi kitu sikielewi, nini maana na lengo la kuwa na wazir asiyekuwa na wizara maalum? Anakuwa na kazi gan na ananguvu kivip katika utendaji? Ina maana yeyote ya kuwa na waziri huyo au ni kutoa lawama tu? Nimefikirai sijapata jibu!
 
Wizara ya kilimo imetajwa sana kwenye taarifa ya CAG lakini Maghembe kanusurika na msaidizi wake Chiza kapandishwa cheo kuwa bosi wizara hiyohiyo...........huu kama siyo usanii ni nini?


Vipi iwaje Ngeleja atimuliwe lakini malima ahamishiwe Wizara nyingine (Kilimo) kama siyo ubabaishaji huo?

Vipi Mkuchika anusurike na Wizara yake ya zamani imezungumziwa sana na taarifa ya CAG kama siyo sera za kulindana?

JK siyo serious anaendesha nchi kudikteta na wala hana nia ya dhati ya kuleta mageuzi ya kweli..................hata khoja ya kuwa mabadiliko haya yatashuka kufika ngazi za watendaji serikalini yanaonekana kama ni changa la usoni tumetupiwa.

Wabunge wanapaswa kuendelea kushinikiza PM ajiuzulu kwa sababu Mkuchika, Maghembe, Nyalandu na Malima bado wanaendelea kutesa sasa huu si ni utani kwenye zoezi zima la uwajibikaji?
 
Hivi timu ikiwa mbovu tena inafungwa kila mara je suluhisho ni kubadilisha nafasi za wachezaji? Na jekama hata rezevu nao niwabovu je timu itabadilika na kuanza kushinda?

Kama unabadilisha nafasi za wachazaji ni wazi unakubali ulikosea mfumo wauchezaji (game plan). Hivyo wewe sio kocha mzuri na pengine pia huna wachezaji wenye uwezo, ari na ujuzi.

Wako wapi waliokuwa wanashadadia na thread kibao kila siku hapa jukwaani, yaani hicho ndo kikosi kilichosukwa? Waje watueleze ubora timu hii tofauti na ile iliyoshindwa vibaya
 
Kama mlivyolisikia mabadiliko ya baraza la mawaziri,rais Kikwete amemteua Prof Mwandosya kuwa waziri asiye na wizara maalum,hivi kazi yake itakuwa ni nini kama sio kufuja kodi za watanzania,yaani rais wetu badala ya kupunguza wizara yeye anaongeza wizara.Sasa hivi nimeanza kukubaliana na wachambuzi mbali mbali wa mambo ya siasa kuwa JK ni janga la taifa.
 
Huyu waziri wa fedha ana historia gani,ana track record yeyote?Wizara ya fedha ni nyeti sana kupewa mtu asiye na track record yeyote,isije ikawa yale ya Zakhia Meghji...mwenye cv ya huyu waziri mpya wa fedha tafadhali aturushie.
 
Back
Top Bottom