Kikwete afanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri - Aprili 2012

kiparah

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,173
114
Hatimaye Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko katika baraza la mawaziri ambapo mawaziri kadhaa wameondolewa, wapya wameingizwa na wengine kuhamishwa wizara huku kadhaa wakiendelea kushika nafasi zao.



  • Rais amemteua mbunge mwingine mpya - Bi. Saada Mkuya Salum
  • Imeelezwa kuwa tukio hili litakuwa LIVE kwenye vituo vya televisheni na baadhi ya redio.
  • Wizara ya Nishati na Madini itaongezewa naibu waziri na ikibidi baadae itaweza kugawanywa...
  • Mawaziri watawajibishwa kisiasa lakini waliosababisha waziri awajibike hawataachwa!
  • Kuanzia sasa akiwajibishwa Waziri basi na watendaji wote walio nyuma yake watawajibishwa\

NAAM:

ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI


MAWAZIRI

1. OFISI YA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,


2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,


3. OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,


4. WIZARA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,

Waziri wa Ujenzi
Dr. John P. Magufuli, Mb.,

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,

Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,

Waziri wa Kazi na Ajira
Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,

Waziri wa Maji
Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,

Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Eng. Christopher Chiza, Mb.,


Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,

Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

Waziri wa Fedha
Dr. William Mgimwa, Mb.,

Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,


5. NAIBU MAWAZIRI


OFISI YA RAIS


HAKUNA NAIBU WAZIRI


6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,


7. OFISI YA WAZIRI MKUU

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,



8. WIZARA MBALIMBALI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,

Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu George Simbachawene, Mb.,

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,

Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,

Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,
 
Hili ndilo baraza lililokuwa linasukwa kwa week mbili? Unampaje unaibu waziri wa nishati na madini Steven Masele na kumuacha geologist Dr Peter Kafumu? Na Mwandosya afya yake inaendeleaje maana naona yumo kwa mtindo wa kizamani wa wizara isiyokuwa na kazi maalum?

Ukweli hili baraza litaharakisha kifo cha CCM. Limejaa wapambe na marafiki! Ni watu wachache sana watakaofanya kazi. Kwa mbunge yoyote wa CCM anayetamani kurudi bungeni 2015 basi aanze kufanya tararibu zingine. Hakuna namna, CCM itapata shida.

Pia, naomba ufafanuzi. Dr Hussein Mwinyi ni mbunge toka Zanzibar, sasa anasimamiaje wizara ya Afya ambayo sio ya muungano?
 
Hakuna jipya hapo ni yaleyale tu ametoa walioshiba na kuvimbiwa... Kaleta wenye njaa na ambao hawajala sana au walikula vikaiisha unamrudisha mtu kama kigoda unategemea nini, mtu kama mwandosya hana wizara maalumu wa nini kumuweka kama si kuzidisha umaskini tu... Hovyooo kabisa jk..... Nendea zako jk huna maana tulikuamini sana kumbe huna lolote... Subiri miaka yako iishe uondoke tu...
 
Tusubirie wafanye kazi jaman,,kuna wengine wanashindwa kufanya kazi kwa sababu ya uzibe wanaowekewa na wakubwa wao kumbe unakuta wapo sahihi km wangeweza kufanya kazi waliopewa lakin unakutwa wanabanwa na katiba au alie juu yao so km malima hafai itaonekana tu katika hii wizara aliyopewa sio kwamba hawezi kubadilishwa huyo sio waziri wa kudumu......tofauti na hapo basi hakuna msafi na mchapa kazi,,,....nawasilisha
 
Hili ndilo baraza lililokuwa linasukwa kwa week mbili? Unampaje unaibu waziri wa nishati na madini Steven Masele na kumuacha geologist Dr Peter Kafumu? Na Mwandosya afya yake inaendeleaje maana naona yumo kwa mtindo wa kizamani wa wizara isiyokuwa na kazi maalum?

Ukweli hili baraza litaharakisha kifo cha CCM. Limejaa wapambe na marafiki! Ni watu wachache sana watakaofanya kazi. Kwa mbunge yoyote wa CCM anayetamani kurudi bungeni 2015 basi aanze kufanya tararibu zingine. Hakuna namna, CCM itapata shida.

Pia, naomba ufafanuzi. Dr Hussein Mwinyi ni mbunge toka Zanzibar, sasa anasimamiaje wizara ya Afya ambayo sio ya muungano?

Mkuu hata mimi hilo la masele limenishangaza sana..

Huyu hajawahi onesha kufahamu lolote katika masuala hayo ya madini!!

Hapa sasa ndio muda wa ku-reload silaha zote!!

Namsikitikia Kigwangala!!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
edchali.jpg



Kubadilisha MaWaziri haitosaidia kitu Ufisadi upo pale pale. Kinachotakikana kuondoka kabisa Serikali ya Magamba ipatikane Serikali mpya
 
kwa upande wa nishati na madini kuna some change kwenye unaibu.Kuna manaibu2
Naibu 1 atasimamia madini na Mwingine nishati.
 
Jaman mie nalia na Nagu na malima..safari ya fikra za ukombozi ktk fahamu zetu bado sana
 
JK bana......mtu anapewa ubunge saa 9 mchana....saa kumi anaukwaa u-naibu waziri!! ni Tanzania pekee utakutana na hii kitu. Mwandosya waziri asiye kwua na wizara maalumu - what the **** is this??? Labda ni favour ili hospital bills zilipwe, akishapona tu, atatemeshwa uwaziri! Wassira, Malima, Sophia Simba.....tunalo!
 
Huyu jamaa inaelekea amechoka hata kuongoza, hataki kufikiria.

Sioni sababu ya kuwatoa watu kwenye recycle bin na kuwapa uwaziri tena. Hao akina Kidoga wana jipya lipi? Hawa akina Wasira kweli hakuna watu wengine Tanzania?

Hili siyo baraza jipya ni mabadiliko ndani ya serikali ile ile na mchezo unaendelea kuwa ule ule kupotezeana muda!!! The guy is not serious at all
 
In Tanzania life get better than this. Halafu hawa wabunge wa kuteuliwa ambao pia wameukwaa uwaziri wanaanza kazi mara moja tena bila ya kuapishwa kuwa wabunge kwanza?
 
nimeshajua kwa nini Makamba hakusaini ile karatasi ya Zito

Alisema wanaojua mchezo wamechuna ila wengine wasojua wanachonga sana!!

Mkuu ila hata Kigwangala naye hakusaini ila wamemsahau!!

Hahhahhahahahahahaha mzee wa MD, MPH, MBA!!
 
HILI NDO BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,
Hawa wawili wamepewa Ubunge bure jana na leo. Sasa JK kawapachika wote wizara moja, tena wizara nyeti. Kuna agenda gani hapa au just a mere coincidence?
 
TAMISEMI nayo ni kituko kabisa. Hawa Ghasia na Mwanri nani alifaa kuwa waziri? Prof Maghembe na Wassira wanarudi kwa ufanisi upi?

I think reshuffle to JK means only to maintain status quo..

Tuendelee kusota!

Mwenye CV ya waziri wa fedha atuwekee hapa!!
 
JK katuchoka Malima anamwogopa nini, Nagu jamani nchi hii sina wa kumwamuni ndani ya serikali ya Kikwete.

Makamba nae ni mnafiki tu mchumia tumbo tu.

kiongozi hana jipya jk.
hawa ghasi,malima makamba,kombani na kigoda aliyetupeleka kwenye mikataba mibovu ya madini anamrudisha..kero yangu kubwa hawa ghasia jamani huu ni kihiyo na kibonde tutapoteza fedha nyingi huko tamsemi.
nilifurahi sana pale aliposema wenzetu watakao chukua jukumu hili.kimaoni jk ameshaona vijana wa kaki(CHADEMA) WANACHUKUA NCHI 2015.....
 
Hahahaha. Ndio voda fasta hiyo. In Tanzania life get better than this. Halafu hawa wabunge wa kuteuliwa ambao pia wameukwaa uwaziri wananza kazi mara moja tena bila ya kuapishwa kuwa wabunge kwanza?

Rais akishasema amesema bwana.Alishawahi kusema ''Nyie watanzania mnataka kula tu bila kuliwa,lazima uliwe ili nawe ule''.
Hapa maharage maji mara moja hakuna kushangaa-shangaa watu hawakawii kuuliza maswali magumu.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
yani nakaaa kichwaa nengu nangoja kusikia mawaziri wapya kumbe mavi matupu malima kigoda mavi matupu ptuuuu...
 
Back
Top Bottom