Kikao Kamati Kuu ya CCM Kimeitaka Serikali Kuwachukulia Hatua Haraka Waliotajwa ripoti ya CAG na TAKUKURU

Siungi mkono hayo maazimio. Mimi kama mwana CCM na mtaalamu, nilitegemea azimio la mwanza liwe kufanya forensic audit, then ndiyo hiyo report itumike kuwashitaki wahusika. Hii ni kwa sababu report ya CAG ni too general, na inawezekana tu mhusika alikosa muda wa kumuonesha CAG au document iko misplaced au tu eti hela ya kujenga shule ilijenga nyumba ya mwalimu au dakitari. So tusiwe washabiki.
Loopholes zinatafutwa hapo !!
 
Kimaigizoigizo ! Nakazia tu ! Wezi wa simu mtaani wanachomwa moto !! Hatari sana !
Hao wanaoteuana wataweza kuchomana? Hilo lingewezekana iwapo hizo nafasi wangekuwa wanazisotea watume maombi wananchi wawapigie kura ndipo wapewe, wanaoteuana wanalindana
 
Kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoketi hii leo tarehe 1 April 2023 chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kimetoa maazimio yafuatayo:

1. Ofisi ya CAG na TAKUKURU Zimepongezwa kwa kufanya kazi kwa weledi
2. Serikali imetakiwa kuchukua hatua thabiti kwa wahusika wote waliothibitika na kutajwa katika ripoti za CAG na TAKUKURU
3. Serikali kuwafuatilia watu wote wanaotumia dhamana na nafasi za umma vibaya na kwa maslahi binafsi na kushindwa kuweka maslahi ya nch mbele.

Tutegemee barua za utenguzi "soon" lakini kuna watu watapanda kizimbani,
Naomba kuuliza hapo,
Na kama mtu alishakufa tunafanyaje?
 
Hao wanaoteuana wataweza kuchomana? Hilo lingewezekana iwapo hizo nafasi wangekuwa wanazisotea watume maombi wananchi wawapigie kura ndipo wapewe, wanaoteuana wanalindana
Na hivyo ndivyo ilivyo !! Lakini kila chenye mwanzo kina mwisho wake !! Karma !
 
Kamati kuu ya chama inayoongozwa na mwenyekiti samia, imeitaka serikali inayoongozwa na samia kuwachukulia hatua hao wezi. Yani maana yake Samia kajipa maagizo yy mwenyewe. Nchi tamu sana hii. Mgeni akija anaweza fikiri hyo kamati ni tofauti na serikali.
Mzaha uliopitiliza
 
Samia (Raisi / Mkuu wa Nchi na Serikali) kaletewa Taarifa na Vyombo vyake, PCCB na CAG.

Samia (Mwenyekiti wa CCM) Kaitisha Kikao kuishauri Serikali kuwachukulia Hatua wote walitajwa Kwa Ufisadi kwenye Report zilizowakilishwa Kwa Samia ( Raisi / Mkuu wa Nchi na Serikali)
Kazi kweli kweli
 
Kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoketi hii leo tarehe 1 April 2023 chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kimetoa maazimio yafuatayo:

1. Ofisi ya CAG na TAKUKURU Zimepongezwa kwa kufanya kazi kwa weledi
2. Serikali imetakiwa kuchukua hatua thabiti kwa wahusika wote waliothibitika na kutajwa katika ripoti za CAG na TAKUKURU
3. Serikali kuwafuatilia watu wote wanaotumia dhamana na nafasi za umma vibaya na kwa maslahi binafsi na kushindwa kuweka maslahi ya nch mbele.

Tutegemee barua za utenguzi "soon" lakini kuna watu watapanda kizimbani,

Wale wezi wa fedha za ndege hadi Mh. Rais akawaumbua, wako wapi? TAKUKURU, mpo kimya, sijasikia bado watu walioachia ngazi, hivi Mkuu wa nchi akishasema si amri, sisi tulitegemea tuone haraka wahusika wakiachia positions zao kwa barua haraka zao wenyewe, sisi hatuoni bado.
 
Muda mwingine muwe mnaona aibu kukomenti upimbi

Hasara ya miaka 9 ya ATCL
Hasara ya miaka 7 ya NHIF
Hasara ya miaka 7 TTCL
Hasara ya miaka 7 ya Mchechu
Hasara ya miaka 6 ya Makamba
Hasara ya miaka 7 ya Tanesco
Weka Bandari hapo
Hasara ya Manyanga

Msitufanye Watanzania kuwa wajinga..Ukichukua hasara ya mashirika yote ya Umma kwa Miaka 10 inaweza kuwa sawa na nusu ya Deni la Taifa au hata zaidi yake.....

Muwe mnaona aibu enyi Wazalendo Uchwara..
Ni kweli kabisa Kama tukisimamia Mali zetu na mashirika yetu Vizuri Hatukua na sababu ya kuomba misaada ya Miswaki na dawa za Meno za mia Tano kutoka Kwa taifa ovu kama Marekani na Washirika wake.

Watanzania tuamke Sasa kuwakataa Mafisadi na Washirika wao.

Rais Ana mamlaka makubwa sana. Ateue watu makini kutoka Hata Vyama vya Upinzani. Mchawi mpe Mwana amlee.

CCM itadumu Kwa kulijenga taifa. Lakini Kwa Hali ya Sasa CCM inakula taifa na kulibomoa. Ni mchwa ndani ya nguzo ya MTU. Ni balaa tupu.

Oooh , TANU yajenga nchi , TANU Oooh TANU yajenga nchi. Tuliimba zamani hizo tukiwa wanafunzi Wa Shule ya Msingi na chipkizi .
Kwa Sasa ni CCM yabomoa nchi na kugawana Fito.

Tangu lini kampuni ya Simu ya Serikali inapata hasara. Hata kibanda Cha Mpesa kama MTU anamtakia mzuri hapati hasara bia Wizi.
Hasara ni matokeo ya Wizi na ufisadi.
Viwanda vya sementi eti vilipata hasara . Mameneja Badala ya kufungwa au kufukuzwa KAZI walihamishiwa wizarani na wengine kwenye Bodi na wengine kuwa Wakurugenzi . WEZI wakazawadiwa vyeo. WEZI wanatabia ya kuwa na mtandao Mkubwa kutokana na kutumia vibaya pesa za umma kuwahonga walioko juu na kuwakirimu wanapotembelewa nao ndio Maana Hata kamati za Bunge zinakua dhaifu kutokana na Rushwa.

Akija waziri au katibu Wa wizara Fulani kutembelea na kukagua shirika au mradi Fulani anapokelewa na zawadi kibao . Kama ni MTU anayependa uzinzi basi ataandaliwa na wanawake Wa kutosha . Hapo ni kubebana tu Hata akiona madudu na ufisadi akiondoka anakumbuka starehe alizokula kwenye ziara na SIO vinginevyo. Utasikia Nakuja Mbeya niandalie Mwanamke Wa kinyakyusa siajwahi kula mnyakyusa. Akienda Moshi mchaga ,akiendaa Kagera Mhaya. Anatengeneza safari za kijinga kijinga kutafuta pesa na starehe.Mashirika yanakufa ,anapata pesa anafanya starehe anajijenga na familia yake.

Hapa pia tutakubaliana wazi kuwa Hata Kukimbiza Mwenge ni kichaka Cha kumaliza pesa za umma Kisha watu kwenda kuomba Misaada ya miswaki.

Mwenge ukipita nchi nzima ukimulika Kila Sehemu lakini Halmashauri nyingi ni Wizi mtupu. Miradi mingi ni ubabaishaji na Wizi mtupu. Mwenge unamulika nini Sasa. Mwenge kama Mkurugenzi hajaandaa fungu la wakimbiza Mwenge basi atakaguliwa na kuibuliwa madudu na kuchaguliwa kuwa hafai kuendelea na KAZI.

Tuachane na Mwenge Wa Kila mwaka unaipa taifa hasara Kubwa. Hizi ni Zama za wapigaji na SIO Wazalendo . Enzi hizo mwange ulikimbizwa na Wazalendo Kwa gaharama ndogo sana.Mkuu Wa Wilaya alikua anapanda gari moja na wakuu Wa Idara mbalimbali Wilayani lakini kwa Sasa Wilaya moja inaweza ikatoa magari 40 ya Kukimbiza Mwenge . Yatatolewa Kila mkuu Wa Idara na gari lake na mengine ya KUKODISHA . Kwa Sasa gharama za kuwagharamikia wakimbiza Mwenge nchi nzima ni kubwa sana . Zinatosha Kununua miswaki na dawa za meno Kwa watoto mashuleni bila kutegemea Misaada ya mabeberu wenye agenda zao mbovu.

Mwenge uwekwe kwenye Nakumbusho na ukimbizwe Kila baada ya miaka Kumi ikiingia Awamu nyingine au Rais mwingine na SIO Kila mwaka .
 
Kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoketi hii leo tarehe 1 April 2023 chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kimetoa maazimio yafuatayo:

1. Ofisi ya CAG na TAKUKURU Zimepongezwa kwa kufanya kazi kwa weledi
2. Serikali imetakiwa kuchukua hatua thabiti kwa wahusika wote waliothibitika na kutajwa katika ripoti za CAG na TAKUKURU
3. Serikali kuwafuatilia watu wote wanaotumia dhamana na nafasi za umma vibaya na kwa maslahi binafsi na kushindwa kuweka maslahi ya nch mbele.

Tutegemee barua za utenguzi "soon" lakini kuna watu watapanda kizimbani,
Jambo la kutenguliwa na Mahakama sahau
 
Sijawahi kuukubali huu ujinga... uibe mwenyewe halafu ujiambie mwenyewe kujichukulia hatua. STUPID
 
CCM CHINI YA MWENYEKITI DR. SAMIAH NI YA TOFAUTI MNO, SUBIRINI KISHINDO CHAKE, NEVER UNDER ESTIMATE!, YATAFANYIKA YA HAKI AMBAYO HATA JPM HAKUYAWEZA, STAY TUNES....!
:ngoja tumalize mfungo, hata hao waliokimbia nje tutawaona kisutu!
Kichaka cha JPM kinaendelea kukauka,wajifunze kudeal na mistake zao bila JPM, kuna kipindi hiko kichaka kikikauka kabisa mtashindwa pakujificha.
 
Wakifanya haya kwa Mara ya kwanza nitaiamini CCM na Rais wake.
Kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoketi hii leo tarehe 1 April 2023 chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kimetoa maazimio yafuatayo:

1. Ofisi ya CAG na TAKUKURU Zimepongezwa kwa kufanya kazi kwa weledi
2. Serikali imetakiwa kuchukua hatua thabiti kwa wahusika wote waliothibitika na kutajwa katika ripoti za CAG na TAKUKURU
3. Serikali kuwafuatilia watu wote wanaotumia dhamana na nafasi za umma vibaya na kwa maslahi binafsi na kushindwa kuweka maslahi ya nch mbele.

Tutegemee barua za utenguzi "soon" lakini kuna watu watapanda kizimbani,
 
Iko hivi bosi. Serikali yetu inaongozwa na mifumo, sera, sheria, taratibu etc katika utendaji kazi na hatimaye repoti. Linapokuja suala la ukaguzi kinachoangakia je kama ni sera, sheria, utaratibu, mifumo ya kimaamuzi ilifuatwa. Chukulia tu mfano kwenye taasisi fulani unakuta mtia sahihi ya malipo fulani kikomo chake ni mil 50, ikizidi hapo labda anatakiwa atie sahihi mkuu wa taasisi na huo unaweza kuwa utaratibu upo, ila unakuta alitia sahihi huyo asiyeruhusiwa na CAG akija atasema utaratibu haukufuatwa. Mfano mwingine, unakuta labda serikali imepeleka hela kwa ajili ya ujenzi wa kitu fulani halafu wakabadili matumizi bila kikao cha bodi husika maana yake CAG akija hapo atasema kuna matumizi mabaya ya hela bil 5 etc. Wakati mwingine wakaguzi wanaomba documenti labda zimepotea au wahusika hawakuleta receipt na CAG asipoipata hiyo receipt tayari hiyo ni hela inahesabika haijulikani ilipo. Kwa ujumla serikalini kuna vitu vingi, tusikimbilie kulaumu
Mzee sawa sawa nipo huku beach bunju navuta upepo wa ulaya natafakari mambo yangu... Nimekuelewa sana mkuu, you're very good at explaining things man....ila mkuu kuna sehemu kitu hakipo sawa mkuu sio bure... Tunalipa kodi kubwa mzee... Hela zetu zinachezewa
 
Back
Top Bottom