Kijiji cha Lupaso, Kwanini umeniliza?

Kijiji cha Lupaso, Kwanini umeniliza?

Dr Mathew Togolani Mndeme

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
201
Reaction score
810
“KIJIJI CHA LUPASO, KWA NINI UMENILIZA?”

1595989836592.png


Lupaso Lupaso, wilaya ya Masasi.
Kijiji mkorosho, jimbo la Nanyumbu.
Kwako kuna korosho, zao la biashara.
Wamakonde wamekupenda, makazi kuyaweka.

Lupaso nina maswali, naomba unijibu.
Nani alikuchora, mipaka yako kuiweka?
Jinalo lilianzanje, Lupaso wakakuita?
Lini ulianzishwa, siku ya kuzaliwa?

Lupaso we mtata, mashambani kufijicha.
Sijui una nini, umekuzidi ukimya.
Pamoja na uzee, makuu umekataa.
Wenzako wa mjini, mashambani hawakupenda.

Lupaso una nini, nani kakubeba?
Koneksheni wazipataje, kuzalisha vipawa?
Kwa nini kupendelewa, wakati hatukujui?
Yapi uliyafanya, Mkapa ukapewa?

Lupaso Lupaso, mbona huniitiki?
Nina swali kukuuliza, kuhusu Benjamini.
Ninaomba unijibu, kwa nini kakutii?
Tulimtaka Masaki, kwako kuna nini?

Lupaso ujibu, nitoe mashakani.
Machozi yamenijaa, maana sikuelewi.
Kwa nini umemwita, Mkapa Benjamini.
Tena wamkataza, asirudi mjini?

Lupaso umetuliza, kumtwaa Benjamini.
Kushtukiza umetuweza, hakika hatuamini.
Ben umemwita, tunauliza kwa nini?
Umesahau kabisa, kwamba tulimwamini.

Lupaso Lupaso, kijini cha Benjamini
Nani ajua kwako, kuuliza ni kwa nini.
Umetuumiza wenzako, umetuacha hatuamini.
Hata kama hutupendi, tupe tumaini.

Lupaso ya Nanyumbu, naona tumekasona.
Hatuna kumbukumbu, ni lini tuligombana.
Kwa nini utuhukumu, bila kushauriana?
Wakati mwenye hukumu, alishakubaliana?

Umekosa huruma, Lupaso wa shambani.
Nani utamtuma, Mama Anna kumfariji?
Wataka aende wapi, Masaki hakukaliki.
Alimzoea Benjamini, walisheherekea themanini.

Niko na wenzake, nao wanalia.
Yuko pia kakaake, moyoni anaugulia.
Wajukuu ni wanyonge, wanakosa wa kumlalia.
Wamegubikwa upweke, wasijue pakulilia.

Lupaso huna huruma, utafakari sawasawa.
Ni kweli imeniuma, Magufuli umemliza.
Kwani kutomjulisha, ulichokua unawaza?
Nini ulishindwa, ambacho hukuweza?

Alikuja Masasi, wananchi kuwaona.
Alitamka ya lami, na wewe ulisikia.
Alisema ikufikie, fadhila analipa.
Kwa nini umemetenda, Ben kumwita?

Lupaso Lupaso, nimekuita mara mbili.
Nimekodoa na macho, kutazama siku mbili.
Kukiita tulichonacho, hukutazama mara mbili.
Sasa hatunacho, unakiweka ardhini.

Lupaso Lupaso, wivu umekuzidi.
Umeiga ya Mwitongo, Butiama uzanakini.
Walipomwitwa wa kwao, Kambarage aliyezidi.
Kwa nini waigapo, unadhani walifaidi?

Mwitongo alituliza, Ben akitufariji.
Sasa umemaliza, hatunaye mfariji.
Kwa nini hukuwaza, tunataka mfariji?
Angalau ungebakiza, afike alfajiri.

Nina hasira na Lupaso, nani anitulize?
Amefanya ya mipasho, nani aniliwaze.
Amechimba na shimo, Ben amfukize.
Nimegoma kwendako, kwa nini akanilize?

Ameninyima kumwaga, kaburini sikuenda.
Hata mwili sitaona, kwa kua sitokwenda.
Laiti angeniona, vile nilivyokonda.
Nimeacha vya kunona, kwa alivyonitenda.

Nitaongea na Magufuli, tuweke kumbukumbu.
Lupaso shuleni, aliposoma Benjamini.
Tupajenge vizuri, na chuo tujenge.
Tukiite Benjamini, urafiki tujenge.

Huenda atasikia, Lupaso mlizaji.
Awe na huruma, awe msikilizaji.
Ben atamlinda, asizame kwenye maji.
Na wazee kuwaita, tuweze kumhoji.

Lupaso umeniliza, sitaki kufarijika.
Mkapa ameniliza, naogopa kukasirika.
Siwezi kusikiliza, hamasa imekatika.
Kama nikiweza, nitakuja kuomboleza


Umeandikwa na Mathew Togolani Mndeme
mmtogolani@gmail.com
 
Lupaso na chato..two worlds apart
Huenda ulimaanisha 'Kilimani au Milimani' iliyopo Chato?

Ningependa kujua Milimani kukoje, ukilinganisha na mabadiliko yanayotokea Chato!

Na kwa hakika, Milimani itakuwa kama Geneva baada ya miaka mitano mingine.
 
Nadhani alienzi hulka za mwalimu.
Labda tu alisahau kupatengeneza kwao. Inasemekana mkewe ndiye alikuwa na kauli ya mwisho. Mbona alichacharika sana kutajirika?

Nyerere kimaadili na hasa kuhusu kuogopa ufisadi huwezi kumlinganisha na kiongozi ye yote wa Tanzania na hata Afrika kwa ujumla. Ujamaa wake ulishindwa na alikuwa na matatizo yake mengine lakini kabisa kabisa aliamini alichokuwa anakihubiri na hakufisadika. Ndiyo maana mpaka leo watoto wake wapo tu wanajaribu kugombea akina Madaraka wanaambulia kura 2 na wanaishi maisha ya kawaida.
 
Huenda ulimaanisha 'Kilimani au Milimani' iliyopo Chato?

Ningependa kujua Milimani kukoje, ukilinganisha na mabadiliko yanayotokea Chato!

Na kwa hakika, Milimani itakuwa kama Geneva baada ya miaka mitano mingine.
Mlimani kuna ma ekalu ya mabebari..wewe uliona wapi hapo hapo kuna ikulu na hapo hapo kuna hoteli ya nyota nne kama siyo tano? na still mkuu wa nchi anaishi hapo na watu from nowhere bado anapata chumba cha hoteli na kukubaliwa. Jiulize au big and complex it's?

Najua watu wa Chato wanawacheka wa Nanyumbu kimya kimya.
 
Back
Top Bottom