Lupaso, Mtwara: Kulikoni Rais Magufuli? Haonekani kwenye ibada ya kumuaga mpendwa wetu Hayati Benjamin Mkapa

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,498
3,465
Salaam Wakuu,

Je, MwanaJF gani yupo Lupaso? Rais wetu Mpendwa yupo hapo? Naomba Aje PM nimuuize maswali Mawili.

Mimi nafuatilia Mazishi ya Marehemu Mkapa kupitia Online Youtube Channel ya JamiiForums.

Lakini Kilichonitia Wasiwasi na Mambo yanayoendelea pale Kanisani Lupaso. Kiti alichotakiwa Kukaa Rais Maguli ambacho Kilikuwa wazi muda Mrefu amekuja Dr, Shein(Kwa kuchelewa sana) akakaa. Pia kiti alichotakiwa kukaa Dr. Shein akakaa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi . Na baadae akaja Mwinyi akakaa. Je, Mwinyi alichelewa wapi na nani?

Ninachohisi ni kwamba Rais Magufuli alitakiwa awepo Kanisani kwani kiti chake kimeandaliwa, hivyo lazima alienda Kusini mwa Tanzania
1596014302356.png

Ratiba inaonesha saa tatu dakika kumi asubuhi hadi saa tatu na nusu, ulikuwa ni muda wa rais Magufuli kutoa salaam za pole, lakini haikufanyika wala hajawakilishwa na mtu.

TUONGEE KIBINADAMU

Katika hotuba yake ya Jana, Rais Magufuli ambaye alikuwa mara kadhaa anatulia, akilengwa lengwa na machozi akisema kifo cha Mkapa ni pigo kwani ilizoeleka katika matukio makubwa anaungana na marais wenzake wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Mrisho Kikwete ‘lakini leo hapa hayupo.” “Mzee Mkapa alinilea kama mtoto wake, alikuwa ni shujaa wangu, alinionyesha upendo. “Saa nyingine machozi yanakuja tu msinishangae sana, hata Mzee Kikwete nilimuona juzi anadondosha machozi tena Kikwete ni Kanali ila alitoa chozi kwahiyo msinishangae mimi,” alisema Rais Magufuli. Je, kwa hali hii, tuseme uvumilivu umemshinda kushuhudia kuingizwa kaburini kwa Swahiba, rafiki, Baba yake Mlezi?

Nakumbuka Baba wa Taifa Julius Nyerere alipofariki, watu walikuwa wanaanza kwa Kulia kisha wanadondoka na kuzimia hata kukimbizwa Hospitalini. Kuna baadhi Baba wa Taifa anazikwa walikuwa hawana fahamu Wakaenda kushuhudia Kaburi na kuangalia Mkanda wa Video wakiwa wamejifungia Chumbani.

Hakika rais Magufuli alikuwa na Mapenzi ya dhati kwa Benjamini William Mkapa. Popote alipo namtakia kila ka heri na Mungu ampe Moyo wa Uvumilivu. moyo wa Ushujaa..

Biblia inasema hivi:

Hata Yesu alipofiwa na Rafiki yake Lazaro alilia sana, hivyo hata Rias wetu Kulia sio Tatizo. Bali tumuombee Mfariji wa wote ampe ahueni na arudi katika Maisha yake ya kawaida kwani Kifo ni safari yetu sote na wote tumetoka Mavumbini na tutarudi Mavumbini.

Yohana 11:32 Maria alipofika mahali alipokuwa Yesu na kumwona, akaanguka miguuni pake na kumwambia: “Bwana, kama ungekuwa hapa, ndugu yangu hangekufa.”Yesu alipomwona akilia na Wayahudi waliokuja pamoja naye wakilia pia, akaugua moyoni* na kutaabika. 34 Akauliza: “Mmemlaza wapi?” Wakamjibu: “Bwana, njoo uone.” 35 Yesu akatokwa na machozi.

Kiti 2.PNG

Picha Hii ya Kwanza, Hii ndio sehemu Rais Magufuli alitakiwa akae. Upande wa Kulia baada ya Viti vyeupe, Wamekaa Wafiwa, kwa vyovyote hakuna nafasi ya Rais.
Kiti 3.PNG

Baadaye akaja Rais wa Zanzibar akaa, na Sehemu alipotakiwa kukaa Dr. Shein Akakaa Seif ali Idd( Wa kwanza kushoto Mwenye Mvi)
Kiti 4.PNG

Seif Idd amejaza nafasi, na Kiliti kilichobaki Wazi akaja kukaa Mzee mwinyi Baadae hata Sadaka ilikuwa imeshatolewa.
Kiti 5.PNG

Kilichonishitua ni kwamba tangu Mzee Mwinyi afike amekuwa mtu wa Mawazo sana. Kuna nini kimetokea hadi rais asifike?
Kiti 6.PNG

Picha kutoka Kushoto: Rais Msitaafu Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu Mzee Hassan Mwinyi, Makamu wa Pili Zanzibar Seif Ali Iddi, Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein, Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu
Kiti.PNG

Hiki kiti kilicho wazi, Kaenda wapi? Kachelewa wapi hadi Ibada imempita?​

Stay Tuned.

UPDATES:
1596018975169.png

1325hrs: Rais Magufuli afika Lupaso na kwenda kanisani ambapo watu wanaendelea kuaga. Amefika na kukaa. Ratiba ya Mazishi inaendelea
 
Mimi nilijua tangu majuzi kuwa hatakuwepo huko. Nyie mnashangaa nini huku jana alishatimiza wajibu wake!
Kaanza safari asubuhi toka Mtwara kwenda Lupaso, kwa hiyo akienda na chopa anawahi ila akienda na gari atachelewa maana kuna kaumbali Mtwara Masasi, na kutoka Masasi Lupaso.
 
Nyie mnashangaa nini huku jana alishatimiza wajibu wake!
Si jambo baya kuuliza ni RAIS wetu ambaye tunampenda na tulitangaziwa alishafika Mtwara kwa kwa ajili ya kumzika mpendwa wetu. Kwa upendo binafsi lazima tujiulize why haonekani. Kwa nia njema. Yeye ni binadamu anaweza kupata dharura, lakini yeye ni kiongozi wetu si vibaya tukaambiwa.

RIP BWM tutakukumbuka daima
 
Naona hata jukwaa kuu hawajamwekea nafasi yake, labda majonzi yamemzidi na uchovu.

Kama hayupo, labda ni kwasababu nyingine lakini sio uchovu. Huwa tunamuona akiwa na ziara za karibia wiki nzima, hufanya mikutano na huwa kuna maigizo kuwa kasimamishwa, hatujaona kachoka. Labda isije kuwa ni yale yale kuwa huko kusini kwake sio sehemu salama.
 
Back
Top Bottom