Kijana wa kiume unakuwaje chawa? Kuna shida mahala

100 others

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
4,299
14,381
Chawa ni zaidi ya mpambe.
Napenda kuzungumzia hawa chawa wa kiume, kuanzia kwenye siasa, music industry hata mtaani.

Chawa wanapenda lifestyle la wanaume wenzao wenye pesa, ili kuweza na yeye kufika pale na aishi yale maisha atatengeneza ukaribu na boss ili kumfurahisha kwa maneno ama vitendo, hii ni sifa ya kina dada, mwanamke anavutiwa sana na lifestyle ya mwanaume fulani hivyo hufanya juu chini na yeye aweze kuishi hayo maisha, utakuta dada wa 20's anatoka na mzee wa miaka 70 ambae ni tajiri, kikubwa si mapenzi bali amevutiwa na lifestyle ya kifahari.

Ugomvi wa chawa kwa chawa huwa ni maneno na mdomo mwingi sana, mipasho, majungu, hapa utakuta wanagombania matajiri, hii sifa ni ya wanawake wakiwa wanagombania mabwana, utakuta kijana wa kiume na kengele zake mbili anamwambia chawa mwenzake ambae wana uadui "tajiri yangu ana rolls royce we huyo wako anayo... blah...blah...blah".

Haya ni mambo ya kike tulishazoea lakini hivi sasa vijana wa kiume ndio kazi mjini kugombania wanaume wenzao kutwa kwenye social medias.
Nielewavyo wanaume huwa hawana maneno mengi hata wakigombana.

Ukichunguza tabia nyingi za chawa zinaingiliana na mambo ya kike sasa ndio najiuliza hivi hawa chawa ni wazima?

Wengine wapo humu anatoa nyuzi ya kusifu na kuabudu akimaliza anatoa na namba ya simu ili matajiri wamtafute..

Kwa jinsi chawa wanapenda kitonga naamini katika utafutaji wao kuna raia wanawashika kalio.

Mtoto wa kiume uliye lelewa katika malezi bora huwezi kubali kuwa chawa , ni kujidhalilisha na kujiondolea utu, uchawa ni barabara ya kuelekea kuwa msosi wa watu.

Hapa jf wapo wengi sana kwenye siasa.
 
Hakuna taifa limeendelea kwa kuwa na chawa wengi.
Uchawa unasaidia nini kwenye uchumi wa nchi?
mimi mwenyewe sio chawa ila hakuna nilichosaidia kwenye uchumi wa nchi,,ila mimi ni (KE),,ila nmetoa mfano.
Acha walishe familia zao,nchi ina watu wake wa kuipa faida sio lazma wote.
sema watasaidia kwa kulipa kodi,tozo,bili za maji,kununua umeme........nk.
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Sema hata mi ni chawa wako kwa kweli...
Sio kwa kukufata hivi ms R
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ni mjinga sana wewe๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚usitegemee malipo apa
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ni mjinga sana wewe๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚usitegemee malipo apa
Why sasa mbona najitoa sana mimi ๐Ÿฅบ๐Ÿฅบ๐Ÿฅบ๐Ÿฅบ๐Ÿฅบ๐Ÿฅบ๐Ÿฅบ
 
Back
Top Bottom