Kijana mkoani Kilimanjaro auawa kwa panga kwa madai ya kutaka kushiriki tendo la ndoa na mke wa mtu

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Mkazi wa kijiji cha Kibaoni wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, Juvenal Claudi (20) ameuawa kwa kukatwa katwa na mapanga baada ya kufumaniwa akitaka kufanya mapenzi na na mke wa mtu.

Taarifa zinadai kuwa kijana huyo aliyeuawa alikuwa akichati na mke wa mtu ambapo baadaye mume wa mwanamke huyo, Riziki Shirima (22) alidaka simu ya mkewe na kukuta meseji za mapenzi.

Baada ya kukuta meseji hizo, mwanaume huyo aliweka mtego kwa kuendelea kumtumia meseji kijana huyo aliyeuawa, akijifanya yeye ndio mwanamke huku akimtaka kuja nyumbani jambo ambalo alifanya hivyo.

Baada ya kijana huyo kufika nyumbani alianza kushambuliwa kwa kukatwa mapanga na baadaye kufariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoani wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio ambapo amesema tukio lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 4 na kusema baada ya mwanaume huyo kufanya mauaji alijisalimisha mwenyewe polisi.

"Ni kweli hili tukio limetokea katika kijiji cha Kibaoni wilaya ya Rombo ambapo mwanaume alimfumania mkewe nyumbani kwake akiwa na huyu kijana aliyeuawa wakitaka kufanya mapenzi," amesema Kamanda Maigwa

Kamanda Maigwa amesema jeshi la polisi linaendelea kumshikilia muuaji baada ya kujisalimisha mwenyewe polisi.

Chanzo cha Habari ni Mwananchi online
 
Dah jamaa ni katili sana hata hajafumania mbususu ikiliwa na wala hakumuonya yeye ni kufanya appointment ya kumuingiza mtegoni na kumuua tu. Dah Dunia hii ina watu makatili sana
Chanzo cha hayo ni polisi kumkamata Mbowe kabla hajakata miti na kuchoma vituo vya mafuta, zuia uhalifu kabla haujatendeka; wakili wa serikali njoo huku jaji amekwishafika.
 
Back
Top Bottom