Kilimanjaro: Mfanyakazi wa ndani auawa kwa kipigo

Abby Uladu

JF-Expert Member
Dec 16, 2022
2,031
4,236
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, linamsaka mkazi wa Kijiji cha Uswaa, wilayani Hai (jina linahifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi), akidaiwa kuhusika kifo cha msichana wake wa kazi 'house girl' ambaye ni mwenyeji wa Mkoa wa Kigoma.

Mtoto Zuwena Bihumo, (14) ambaye ndiye alikuwa akifanyia kazi kama mtumishi wa ndani kwa mama huyo, anadaiwa kuwa Oktoba 23, 2023; alifariki dunia baada ya kupigwa viboko na bosi wake, ambavyo vinadaiwa kumsababishia majeraha mbalimbali mwilini, ambayo ndiyo kiini cha kifo chake.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 26, 2023 na Jeshi hilo, huku likisema kuwa baada ya kifo hicho, mwanamke huyo anadaiwa kutoroka na kwamba juhudi za kumtafuta zinaendelea, japo mumewe yuko mikononi mwa Polisi.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Simon Maigwa amesema: "Tunamshikilia mtuhumiwa mmoja mwanaume (Jina limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi) kwa kudaiwa kusababisha kifo cha binti aitwaye Zuwena Bitaliho Bihumo, (14) mfanyakazi wa ndani mwenyeji wa Kigoma."

"Mtuhumiwa huyo na mke wake walikuwa wakimfanyia ukatili binti huyo kwa kumchapa na kitu kinachodhaniwa ni fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake na kupelekea majeraha makubwa yaliyosababisha kifo chake," ameongeza Kamanda Maigwa.

Kamanda huyo amesema baada ya kutenda unyama huo, ‘waajiri’ hao walimfikisha marehemu Hospitali ya Wilaya ya Hai kama mgonjwa huku wakitambua kuwa alishafariki muda mrefu.

#GAZETI LA MWANANCHI LEO
 
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, linamsaka mkazi wa Kijiji cha Uswaa, wilayani Hai (jina linahifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi), akidaiwa kuhusika kifo cha msichana wake wa kazi 'house girl' ambaye ni mwenyeji wa Mkoa wa Kigoma.

Mtoto Zuwena Bihumo, (14) ambaye ndiye alikuwa akifanyia kazi kama mtumishi wa ndani kwa mama huyo, anadaiwa kuwa Oktoba 23, 2023; alifariki dunia baada ya kupigwa viboko na bosi wake, ambavyo vinadaiwa kumsababishia majeraha mbalimbali mwilini, ambayo ndiyo kiini cha kifo chake.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 26, 2023 na jeshi hilo, huku likisema kuwa baada ya kifo hicho, mwanamke huyo anadaiwa kutoroka na kwamba juhudi za kumatafuta zinaendelea, japo mumewe yuko mikononi mwa Polisi.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Simon Maigwa amesema: "Tunamshikilia mtuhumiwa mmoja mwanaume (Jina limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi) kwa kudaiwa kusababisha kifo cha binti aitwaye Zuwena Bitaliho Bihumo, (14) mfanyakazi wa ndani mwenyeji wa Kigoma."

"Mtuhumiwa huyo na mke wake walikuwa wakimfanyia ukatili binti huyo kwa kumchapa na kitu kinachodhaniwa ni fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake na kupelekea majeraha makubwa yaliyosababisha kifo chake," ameongeza Kamanda Maigwa.

Kamanda huyo amesema baada ya kutenda unyama huo, ‘waajiri’ hao walimfikisha marehemu Hospitali ya Wilaya ya Hai kama mgonjwa huku wakitambua kuwa alishafariki muda mrefu.

#GAZETI LA MWANANCHI LEO
Huzuni kubwa aisee
 
Kuna watu ni makatili sana, unaanzaje kumuadhibu mtoto ambaye hunaye nasaba, si bora kumrudisha kwa wazazi wake, nimeishi na house girl watatu, hakuna hata mmoja nimewahi mpiga, mmoja alikuwa mwizi sana, nilichomwambia ni kujiaandaa aende kwao kwani wanamhitaji, hadi Leo hii anapiga simu akitaka kurudi
 
Kuna watu ni makatili sana,unaanzaje kumuadhibu mtoto ambaye hunaye nasaba,si bora kumrudisha kwa wazazi wake,nimeishi na house girl watatu,hakuna hata mmoja nimewahi mpiga ,mmoja alikuwa mwizi sana,nilichomwambia ni kujiaandaa aende kwao kwani wanamhitaji,hadi Leo hii anapiga simu akitaka kurudi
Hawa watu huwa sijui wanaakili gani kama unaona huendani na mfanyakazi wako si umrudishe kwao.. angalia pengine ndiye alikuwa tegemeo kwa ndugu zake washazima ndoto zake.... hakika damu yake itamlilia saba
 
Wachaga wana roho mbaya sana
Unaweza kukuta ni wahamiaji WA mkoa huo, Tanzania ni moja na Hawa maharamia yapo pande zote!! By the Way huyo baba namwonea huruma Kwa kushindwa kumkanya huyo mke wake dhalimu!! Watu wengi wanachukulia suala la mtoto WA kazi WA kike ni jukumu la mama house, nooo wanawake Kwa mabinti wasio wao ni madhalimu kweli, tujitafakari kama wanaume, hopefully Police watamuona ni innocent, Nina uhakika huyu baba hakushiriki Kwenye huu udhalimu
Unajua machozi yananitoka, unakuta huyo mtoto anatoka kwao alikuwa na wadogo zake na kuaga naenda kutafuta kazi niwaletee zawadi, na wao kumuaga Kwa huzuni, halafu wewe unakuwa chanzo Cha kukatisha furaha za hawa malaika!!??
 
Kuna watu ni makatili sana,unaanzaje kumuadhibu mtoto ambaye hunaye nasaba,si bora kumrudisha kwa wazazi wake,nimeishi na house girl watatu,hakuna hata mmoja nimewahi mpiga ,mmoja alikuwa mwizi sana,nilichomwambia ni kujiaandaa aende kwao kwani wanamhitaji,hadi Leo hii anapiga simu akitaka kurudi
Nimeishi na bint miaka 14 mpaka anakuja kuposwa akiwa kwangu
Wazazi wake wakabariki nisimamie harusi ya bint na ifanyikie kwangu na mahari wakanipa 65% mpana Leo bint ana watoto 4 huwa anakuja kwangu
Kama kwao kwa jinsi tulivyoishi naye
 
Back
Top Bottom